-
Kheri ya mwaka mpya 2022
Huu ni mwaka ambao kwa hakika ulikuwa umeusubiria kwa hamu kubwa sana. Sasa hatimaye umefika. Wakati unajipongeza kwa mwaka mpya hakikisha1. Umeweka mipango dhabiti kwa ajili ya huu. Usiishi mwaka huu bila malengo. Ongozwa na malengo 2022. 2. Hakikisha unachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa nguvu zako zote bila kuchoka mwaka 2022. Binafsi nimechagua…
-
Kama hujui unachotaka sasa hivi, ukikiona kesho hutakifahamu pia
Kuna watu huwa hawaweki malengo kwa kisingizio kwamba kitu chochote wanachotaka wakikiona watakifahamu. Ila ukweli ni kwamba, kama kitu unachotaka hukijui, hata kesho ukikiona hutakifahamu. Ndiyo maana inashauriwa uwe malengo kwa sababu yanakufanya uone unachotaka. Na chochote kile ambacho akili yako inaweza kuona, basi inaweza kukifikia. Tembelea blogu yangu kupitia SONGA MBELE BLOG
-
ANZA KIDOGO
Kama kuna kitu nimekuwa nasisitiza kila siku ni kuanza kidogo, kuanza na kile ulichonacho, kisha kuendelea kukuza hicho kidogo ili kutengeneza kikubwa zaidi. Ebu leo jiulize ni kitu gani kikubwa nimekuwa nataka kuanza kufanya ila sijaanza. Anza leo kidogo.
-
Masomo Matano Kuhusu Fedha Unayopaswa Kuyafahamu Katika Maisha
Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine. Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu. 1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako. 2. Fahamu kuwa…
-
Kitu Kinachoashiria Kuwa Hutafika Mbali Kimafanikio
Kuna vitu vingi ambavyo vinaashiria kuwa hutaweza kufika mbali kiuchumi, hata hivyo kimoja kikubwa sana kati ya vyote ni KUTOJIFUNZA. Kama hupati muda wa kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu , jua hicho ni kiashiria cha wewe kuja kuanguka siku moja. Hili litatokea bila kujali unafanya kazi kwa bidii sana au una mtaji mkubwa, kwa…
-
Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia
Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao. Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni…
-
Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!
Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene. Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha. Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki…
-
KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?
Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza? Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangaliaWatu uliowalenga. Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza. Kwa hiyo badala ya kujiuliza…
-
Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki
Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane. Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa…
-
Majadala Mzito Kuhusu Kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI//GODIUS RWEYONGEZA
Siku moja nilishiriki kwenye mjadala kwenye kundi la KITABU CHAT. ambapo mada kubwa ilikuwa ni KILICHOMO NDANI KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nilianza kwa kutoa utangulizi mfupi kuhusu kitabu hiki hapa cha kipekee sana. baada ya utangulizi na mae lezo machache, yalianza kuulizwa maswali. swali la kwanza kuulizwa lilikuwa ni hili hapa chini. “…mtu akifanya kazi…
-
KUZA KIPAJI CHAKO
Kipaji ni mauwezo fulani hivi ya asili ambayo mtu unazaliwa nayo na yanakuwezesha kufanya vitu kwa namna ya upekee sana. Mauwezo haya yanakutambulisha kwa watu kwa sababu hakuna mwingine ambaye anakuwa nayo. Na wala ya kwako hayawezi kulinganishwa na ya mtu mwingine. Sasa nikuulize wewe, kipaji chako unakifahamu? Ni kipi? Na je unakifanyia kazi? Hakikisha unakitumia…
-
Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi
Siku kadhaa zilizopita nilipokea simu ya mtu aliyekuwa anataka nimwambie chuo kizuri kinachonoa Waandishi Wa Vitabu. Nilimjibu vizuri tu, ila hakuridhika na majibu yangu kwa maana yalipingana na kile alichokuwa anaamini kwa asilimia 100. Yeye alitaka kwenda chuo, asomee uandishi na apate cheti. Cheti cha nini sasa? Najua, jamii yetu imezoea kwamba ukiwa na cheti…
-
FANYA UAMUZI SASA
Bila kujali upo katika hali gani, Kuna wakati unapaswa kufanya UAMUZI kwamba sasa mimi nitaanzia hapa na nitaendelea mbele Kataa kabisa kuendelea kusema kwamba sina mtaji Kataa kuendelea kulalamikia ugumu wa maisha. Chagua kuanzia hapo ulipo, miaka 10 ijayo utajishukuru kwa uamuzi huu. Amua Sasa kupata vitabu vitano kwa elfu kumi tu. Hii ofa mwisho…
-
Kinachotokea Unapokuwa Na Ndoto Kubwa
Jana niliandika makala yenye vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya. Mmoja wa wasomaji wa amkala hiyo alinibu kwa kusema hivi Nami nikawa nimemjibu pia kwa ujumbe huu hapa chini Ni kweli unapokuwa unapambania ndoto kubwa watu watakuona mtu wa ajabu sana. Watakuona kichaa, utaambiwa umechnganyikiwa na mambo mengine mengi. Na hili linawatokea watu wote wenye…
-
Vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya
Katika maisha Kuna vitu hata iweje huwezi kusema umechoka kuvifanya. Huwezi kusema nimechoka kupumua, maana ykiacha kupumua tu huo ndio mwisho wako. Huwezi kusema nimechoka kula, wala huwezi kusema nimechoka kulala, kuanzia leo sitalala tena. Ni vitu vya asili ambavyo mwili wako unahitaji ili uendelee kuwa imara zaidi. Wewe pia Kuna vitu unapaswa kujiwekea utaratibu…
-
FANYA UNACHOPENDA
Mara nyingi watu hupenda kufanya kazi fulani kwa sababu aidha ya kifedha au kutafuta umaarufu au pengine kwa kulazimishwa na wazazi. Lakini kazi hizi huwa hawazifanyi kutoka moyoni au Wala huwa haziwapi motisha. Ni muhimu sana ufanye kitu unachopenda kuliko kulazimisha au kulazimishwa kufanya kitu usichopenda. Kama ni fedha au umaarufu utaupata kwa kufanya…
-
Kitu hiki lazima tu kitokee maishani mwako
Kuna vitu katika maisha lazima tu vitokee. Vinatokea uwe unavipenda au huvipendi. Vyenyewe vinatokea tu. Jua linachomoza na kuzama, bila kujali unapenda au hupendi.Dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, bila kujali una chuki nayo au unaipenda. Ukiruka juu, sharti utarudi chini bila kujali unapenda au hupendi. Mojawapo ya kitu kingine ambacho lazima kitokee kwenye maisha…
-
Madhara Ya Kuwa Na Mahusiano Na Mtu Zaidi Ya Mmoja
Kama una ndoto kubwa na umekuwa na mpango wa kuja kuwa na mahusiano na watu wawili, au tayari una mahusiano na watu wawili ni bora ukauhairisha au kuondoa kabisa huo mpango. Yafuatayo ni mdhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja. Kwanza utapoteza nguvu zako nyingi kwa watu hao ambao umeingia nao…
-
Kitabu cha KUTOKA UMASIKINI MPAKA MAFANIKIO CHA ERICK SHIGONGO.
Kwenye kitabu hiki Erick Shigongo ameeleza historia ya maisha yake na kutoa mafunzo kadha kadha kuhusu maisha Kitabu hiki ni kizuri sana, nashauri kila mwenye kiu ya mafanikio makubwa akisome. Utajifunza mengi kuhusu kutoka umasikini mpaka mafanikio makubwa kupitia stori ya Erick Shigongo ambaye maisha yake yalikuwa duni sana, kuliko hata wewe ila akaweza kupasua…
-
Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21
Madalali ni watu ambao wamekuwepo kwa siku nyingi sasa. Kazi yao kubwa imekuwa ni kuunganisha eneo moja lenye bidhaa na jingine lenye uhitaji. Kama una uhitaji wa chumba cha kupanga unamwona dalali anayekuunganisha kilipo. Kiufupi wenyewe wamekuwa wanaingia katikati ya mlaji na mzalishaji. Kwenye karne ya 21 udalali ndio umetengeneza mabilionea kwa wingi. Mtandao…
