Month: March 2022

  • Ushauri: Mbinu Za Kuuza Kitabu Kwa Mafanikio Makubwa

    Unaendeleaje rafiki yangu. leo hii ninaenda kuwa najibu swali nililoulizwa na mmoja wetu ambaye anapitia kwenye changamoto baada ya kuwa amezindua kitabu chake na hakijafanya vizuri. Ebu kwanza tuone anachosema; Habari yako kaka kwa mara nyingine!!! Pole na hongera kwa kuendelea na wajibu ulokuleta duniani. Ni takribani wiki 1 toka nitoe kitabu changu kiitwacho “THAMANI…

  • Gharama Sita Unazopaswa kulipa ili kufikia ndoto zako.

    Ukiwa na ndoto kubwa unapaswa kuwa tayari kulipa gharama. Ni vigumu kufikia ndoto kubwa bila ya kulipia gharama ndoto zako. Na linapoongelewa suala zima la gharama basi watu wengi wanadhani gharama ni pesa peke yake. Hapana. Hizi hapa ni gharama sita unazopaswa kulipa ili kufikia ndoto zako

  • Uhuru wa kifedha ni nini?

    Uhuru wa kifedha ni pale ambapo unakuwa na fedha za kukutosha kwa kutumia kipindi fulani. Kama wewe matumizi yako kwa siku ni shilingi elfu tano. Ukiwa na milioni moja maana yake utakuwa na uhuru wa kifedha wa  siku 200. Ila ukiwa na shilingi milioni moja na matumizi yako kwa siku ni laki moja maana yake…

  • KWA NINI UNAPASWA KUANZISHA BIASHARA

    1 zama zimebadilika Mambo yanabadilika aisee! Zamani ulikuwa hivi, ulitakiwa kwenda shule, kusoma kwa bidii ma baadaye ulikuwa na uhakika wa kupata ajira. Siku hizi mambo yamekuwa tofauti. Kuna watu wengi ambao wamehitimu na wapo mtaani ila kazi hawana. Kwa hiyo je, tuendelee kuwambia wanetu na washikaji zetu kuwa waende shule wasome kwa bidii ili…

  • Ndoto siyo ile unayoota ukiwa umelala, ndoto ni ile unayoona ukiwa macho

    Kama kuna kitu ambacho utapaswa kufanya maishani mwako na kikawa ni kitu chenye manufaa makubwa kwako ni kukaa chini na kuandika ndoto yako chini. Unaweza kuona kukaa chini kupanga vitu ambavyo ungependa kufikia maishani mwako kama ujinga, ila ukweli ni kwamba ukishindwa kupanga unakuwa unapanga kushindwa. Kiuhalisia muda ambao unatumia kupangani mdogo ukilinganisha na manufaa…

  • UPO TAYARI KUJIANDAA KWA MIAKA MINNE IJAYO?

    Mashindano ya olympiki ni miongoni mwa mashindano yenye nguvu sana. Yanapendwa na watu lakini pia washiriki wake huwa wanajiandaa kwa kipindi kirefu kabla ya mashindano yenyewe. Washiriki wa mashindano hayo wanajiandaa kila siku kwa kipindi cha miaka minne kwa ajili ya shindano ambalo linadumu kwa dakika kadhaa kisha kupotea. Na ndani ya dakika hizo ndipo…

  • Kwa nini unapaswa kuanzisha biashara

    1 zama zimebadilika Mambo yanabadilika aisee! Zamani ulikuwa hivi, ulitakiwa kwenda shule, kusoma kwa bidii ma baadaye ulikuwa na uhakika wa kupata ajira. Siku hizi mambo yamekuwa tofauti. Kuna watu wengi ambao wamehitimu na wapo mtaani ila kazi hawana. Kwa hiyo je, tuendelee kuwambia wanetu na washikaji zetu kuwa waende shule wasome kwa bidii ili…

  • KITABU:MAAJABU YA KUWEKA AKIBA: Jinsi Tabia ya Kuweka Akiba Inaweza Kukufanya Uwe Tajiri

    Mwaka juzi (2020) niliandika kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kwenye kitabu hiki niliandikabutangulizi huu hapq chini ambao Leo hii bado una nguvu kubwa aawa na nilipouandika. “Tangu umezaliwa mpaka leo hii, ni unaposhika kitabu hiki mikononi mwako ni wazi kuwa fedha nyingi tayari zimepita mikononi mwako. Hivi laiti ungekuwa umeweka utaratibu wa kuwa unatoa…

  • Hakuna mwenye kipaji cha kila kitu

    Hakuna mwenye kipaji cha kila kitu na wala hakuna anayeweza kila kitu. Usitake kujihangaisha na kuonesha kuwa wewe ndiye wewe kwenye kila kitu. Kuna vitu vichache unaweza kuvifanya vizuri Weka juhudi zako hapo. Vingine waachie wengine. kupata ebook ya KIPAJI NI DHAHABU tuma elfu tano kwenda 0755848391 ili utumiwe ndani ya dakika tano bila kuchelewa.

  • Jinsi ya kupata chochote unachotaka

    Rafiki yangu habari ya leo. Bila shaka unaendelea vyema kabisa. Zig Ziglar aliwahi kunukuliwa akisema kuwa unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile wanachotaka. Yaani, kauli hii fupi laiti ingefahamika kwa watu vizuri basi kila mtu alipaswa kufurahi maana kauli hii imebeba siri kubwa. Kama hujajua siri iliyobebwa kwenye kauli hii naomba utulie…

  • Kipaji ni dhahabu-4: Kipaji Hakifanyiwi Kazi Kwa Siku Moja

    Najua kuna wengi wangependa wagundue kipaji chao Leo hii na kesho yake wawe tayari wamekuwa mabingwa. Hapana. Inachukua muda. Unahitaji muda kukinoa kipaji chako. Kifanyie kazi kipaji chako kila siku. Wewe wa leo hapaswi kuwa sawa na wewe wa jana na wiki ijayo. Kila wiki iwe wiki ya tofauti kidogo. JIFUNZE kuitumia kanuni ya asilimia…

  • Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Mtandaoni

    Moja ya swali ambalo niliwahi kujiuliza miaka mingi iliyopita, lilikuwa ni namna gani naweza kutengenwza fedha mtandaoni? Kiukweli swali hili lilipa shauku ya kutaka kujua mengi. Kipindi hicho nilikuwa nasikia habari kuwa akina Millard Ayo wanalipwa kupitia mtandao.Sasa swali langu lilibaki, na mimi nawezaje kulipwa mtandaoni. Swali hili lilinifanya niianze kujifunza kupitia kusoma maandiko mengi…

  • Vyeti Vya Hisa Vinaenda Kusitishwa Kutolewa

    Unaendeleaje rafiki yangu. Leo nina taarifa muhimu kwako ambayo unapaswa kuifahamu kama mwekezaji. Kama umesoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE na umeanza uwekezaji, basi utakuwa unajua kuwa kila ukiwekeza fedha yako huwa unatumiwa Cheri. Hata hivyo, utaratibu mpya unaenda kuanza tarehe 1 mwezi ujao (April) Ni kwamba utakuwa hutumiwi cheti…

  • Mafanikio yanachukua njia ndefu

    Ndio inachukua muda, lakini sasa hakuna jinsi. Hii ndio njia nzuri ya kufika kule tunapotaka. Njia nyingine fupi zipo ila sasa siyo za kuaminika na wala hazikupi matokeo ya kudumu. Kwa hiyo njia pekee ya kufika mbali ni kuhakikisha unachagua njia sahihi na kuifuata hata kama inachukua muda. Njia fupi zina matokeo ya haraka yasiyodumu.…

  • Kipaji ni dhahabu-3 njia ya kuwa gwiji

    Njia pekee ya wewe kuwa gwiji kwenye kufanyia kazi kipaji chako ni kufanya mazoezi mara kwa mara bila kuacha. Kadiri unavyofabya mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa imara zaidi na kubobea. Usichoke kukifanyia kazi kipaji chako.

  • Kafanyaje nini huyu?-2

    Mwaka wa tatu jamaa yupo mtaani Hana ajira Ebu fikiria hili. Unaenda shule, unasoma kwa bidii huku ukiwa unategemea upate ajira ya maana, mara unamaliza chuo na ajira haipo! Unasubiri mwaka wa kwanza unapita huku ukiwa umetuma maombi ya kutosha. Unataka kuanzisha biashara, unakuta kwamba mtaji huna! Hiki kitu tu, lazima kitakupa pressure. Usiwaze. Mtaji…

  • Kafanyaje huyu?

    Kapata pressure baada ya biashara yake kutofanya vizuri! Tafiti zinaonesha kuwa Kati ya biashara 10  zinazoanzishwa biashara tano hufa ndani ya mwaka mmoja na nyingine ambazo hubaki huwa hazifikishi miaka 10. Hili wewe mwenyewe lifuatilie mtaani kwako. Utakuta kwamba kuna biashara nyingi zinazoanzishwa  baada ya muda kidogo zinapotea. Hii ndio kusema kwamba usipokuwa makini wakati…

  • Kinachokwamisha wewe kufika mbali.

    Umekuwa unakwama kufika mbali kwenye maisha na kushindwa kufikia ndoto zako kwa sababu tu hujawa na ndoto  kubwa kiasi cha kutosha. Maneno ya busara yanasema hivi, unapaswa kulenga kuifikia nyota kiasi kwamba hata ukishindwa uufikie mwezi. Sasa ebu fikiria hili, wewe ndoto yako siyo kubwa kiasi cha kulenga kuifikia nyota badala yake umelenga kufika kileleni…

  • Usidharau fedha hata kama ni kidogo

    Leo nataka ni kwambie kwamba fedha siyo kitu ambacho unapaswa kudharau. Unaweza kukuta mtu ana fedha kiasi fulani ila akawa anakidharau. Na hata akakitumia hovyo, ila unachopaswa kufahamu ni kuwa usidharau fedha. Hivi hujawahi kujiuliza kwa nini Mo Dewji na utajiri wake wote kwa nini bado anaendelea kutengeneza hadi viberiti? Kiberiti kimoja huku mtaani tunakinunua…

  • KIPAJI NI DHAHABU-2: wekeza kwenye uwezo wako na siyo kwenye udhaifu wako

    Kila mtu kuna eneo ambalo yuko vizuri.  Ukishaligundua hilo eneo ndilo sasa unapaswa kulipa nguvu na kuachana na udhaifu wako. Ukikazana kuboreaha udhaifu wako huwezi kufika mbali hata kidogo kwenye maisha. Ukiwekeza kwenye uwezo wako zaidi na kuufanyia kazi, utakuwa bora zaidi. Hakikisha unapata Ebook ya KIPAJI NI DHAHABU pamoja ebook ya MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA…

X