Month: May 2022

  • Hakuna mtu Ambaye Anaenda Kupiga Kazi Kwa Ajili Yako

    Ngoja nikwambie kitu, hakuna namna ambavyo wewe unaweza Kuepuka kazi katika suala zima la kufanikiwa. Kama unataka kufanikiwa sharti uwe tayari kuweka kazi itakayokufikisha kule unapotaka kufika. Usije unategemea kwamba MTU yeyote atafanya kazi kwa ajili yako. Nakumbuka siku za nyuma niliwahi kuandika Makala hapa nikasema kwamba hakuna MTU ambaye anaweza kupiga Push-Up kwa ajili…

  • Siku 30 Za Kushinda Kwa Kishindo (Juzuu 1)

    Katika moja ya semina ambazo Zig Ziglar alikuwa anatoa kuna mtu mmoja ambaye alihamaki siku moja na kumwuliza, “hivi kwa nini hizi hamasa zenu huwa hazidumu?” Huku akiwa ametulia, Zig Ziglar alijibu kwa kusema kuwa hamasa ni kama kuoga, ukioga leo unapaswa kuoga na kesho. Tena wakati mwingine ukioga asubuhi utapaswa kuoga mchana na jioni…

  • Utapata Kile Unachotaka Kama Utawasaidia Watu Kiasi Cha Kutosha

    Utapata kile unachotaka kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile wanachotaka-Zig Ziglar. Ili wewe kupata kile ambacho unataka maishani unapaswa kuwa tayari kuwasaidia watu kupata kile wanachotaka wao. Kadiri unavyowasaidia watu kupata kile wanachotaka, ndivyo na wewe unakuwa kwenye njia ya kupata kile unachotaka. Kwa hiyo, kazi yako kubwa unayopaswa kufanya ni kutafuta kujua…

  • Jinsi Ya Kufanyia Kazi Ndoto Zako Wazazi Wanapokuwa Wanakupinga

    Karibia kila wiki huwa naandika makala moja inayohusu ndoto na jinsi ambavyo unaweza kufiki andoto zako kubwa ulizojiwekea maishani. Kwenye makala ya jumapili ya leo ninaenda kuandika kuhusu tena kuhusu hii mada ya kipekee. Ambayo kila nikishika kalamu kuandika basi najikuta nahamasika zaidi kufanyia kazi ndoto zangu mwenyewe. Halafu eti nikishika kalamu wakati natumia kibodi…

  • Historia ya Kiswahili

     Ukisoma historia ya Kiswahili  unaona kwamba kilianza kimasihala tu. Kilianza kutumiwa maeneo ya Pwani na baadaye kikasambaa kuja bara na mpaka leo hii, kina wazungumzaji zaidi ya milioni 150. Ni lugha pekee barani afrika ambayo siyo ya kigeni ila watumiaji wengi. Ninataka kusema nini sasa hapa.Ninataka niseme kwamba, kitu chochote kikubwa huwa hakianzi kwa ukubwa wake.Mbuyu…

  • IJUE NJIA YA KUFUATA

    Kama haujui njia ambayo unapaswa kuchukua basi njia yoyote ile itkupeleka Ebu fikiria kitu kama hiki hapa, umeenda stendi ili kukata tiketi, halafu unampa mkata tiketi pesa yako. Na unamwambia kwamba unaomba akupe tiketi unadhani atakuwambiaje? Au au nadhani swali gani atakuuliza? Unaelekwa wapi?  Ebu fikiria unamjibu kwamba sijui. Atakwambia kwamba kama haujui basi rudi…

  • Matendo yako, Ndio matendo yako

    Miongoni mwa ukweli ambao unapaswa kuufahamu ni kwamba matendo ndiyo yanapaswa kutangulia matokeo na siyo matokeo yatangulie matendo.Yaani, huwezi kuwa na afya njema kwanza, halafu eti ndio ukaja kuanza kula vizuri. HapanaUnakula vizuri ndio maana una afya njema.Unafanya mazoezi ndio maana una afya njema.Unaweka akiba benki ndiyo maana una fedha ya kutosha.Unawekeza ndio maana utajiri…

  • Nyakati Ngumu Hazina Ukomo

    Leo nimekumbuka mwaka 2018 na 2019 jinsi watu walivyokuwa wanalalamika kwamba vyuma vimekaza. Kuna watu wengi walikuwa wanasema kwamba hawawezi kufanyia kazi malengo yao kwa sababu tu vyuma vimekaza. Nakumbuka kila nilipokuwa nikiongea na watu, kitu muhimu nilichokuwa nikiwasisitiza kilikuwa ni kwamba, USISUBIRI VYUMA VILEGEE. Badala yake katika kukaza hukohuko, wewe mwenyewe pambana kuhakikisha kwamba…

  • Je, Kuna Namna Na Kutengeneza Fedha Kupitia Affiliate Marketing Ukiwa Nchini Tanzania?

    Habari ya huko upande wa pili. Mimi kutokea hapa mkoani Morogoro naendelea vizuri tu. Siku ya leo napenda kujibu swali la mmoja wetu hapa kwenye jukwaa ambaye ameniuliza kama kuna namna ya kutengeneza fedha kupitia affiliate marketing ukiwa hapa nchini Tanzania. Na mimi kwa ufupi napenda kusema kwamba INAWEZEKANA. Ila naomba usome ujumbe huu mpaka…

  • Songambele

     Rafiki yangu, muda wote na mara zote unapaswa kuwa mtu wa kusonga mbele. Usikubali kukwama na wala kubaki eneo lile bila ya kusongambele. Vitu ambavyo vinakaa sehemu moja bila ya kusongambele huwa vina sifa mbaya kweli.Maji yaliyotuama, ndio huwa yanazalisha mbu wa malaria. Hata mdomo wako ukiufunga bila kuongea kwa muda mrefu unatoa harufu mbaya.…

  • Fedha Chanzo Chake Ni Thamani

    Wachezaji Lionel Messi na Ronaldo wanacheza dakika 90 uwanjani na wanalipwa kiasi kikubwa Cha fedha kuliko wachezaji wengine. Unadhani kwa nini wanalipwaa kiasi kikubwa hivyo? Ni kwa sababu ya thamani yao wanayotoa. Kitu chenye thamani kubwa kinauzwa kwa bei kubwa ukilinganisha na kitu chenye thamani ya ndogo. Kama unataka kupata fedha basi unapaswa kuwa tayari…

  • Fanya Yafuatayo Kuepuka Kuwa Miongoni mwa Walalamikaji

    Moja ya kitu rahisi sana ni kulalamika. Kila mtu anaweza kukifanya. Lakini kitu kigumu kufanya ni vitendo na kuonesha matokeo. Sasa siku ya leo, nataka uepukane na malalamishi ili mwisho wa siku uwe mtu wa kuleta matokeo ambayo wewe mwenyewe unayatamani Unajua kwa Nini Watu wanalalamika? Kwa sababu kuna matokeo mazuri wanayataka ila  wanataka mtu…

  • Usikubali Kuendelea Kubaki Hivyo hivyo

    Kuna mtu mwaka 2010 alikuwa analalamika kuwa hana mtaji, mwaka 2015 alikuwa bado analalamika kwamba hana mtaji, mwaka 2020 bado analalamika kwamba hana mtaji. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba mwaka 2025 atakuwa bado analalamika kwamba hana mtaji. Hivi ni kweli kwamba huyu hana mtaji au hayuko makini? Leo ninachotaka kuongea na wewe ni kwamba usikubali kubaki hivyohiyo.…

  • Njia Mpya Ya Kutengeneza Utajiri Tanzania

    Kwa kila sekunde inayopita, mtandao wa google unapokea maombi 40,000. Hawa ni watu mbalimbali wanaotafuta majibu ya maswali yao kwenye mtandao huu. KWA NINI WATU WANATAFUTA MAJIBU GOOGLE?Moja ni kwa sababu majibu waliyonayo hayatoshelezi hivyo wanatafuta suluhisho jipya. Pili, kwa sababu hawajawahi kupata suluhisho la swali hilo kabisa maishani mwao. Hivyo njia pekee ni kukimbilia Google…

  • Leo ikiwa Ni siku ya Idd napenda kutoa ofa kwa mtu mmoja tu ambaye atajiunga na kozi yangu ya UANDISHI

    Eid Mubarak Kwako rafiki yangu Kozi ya kipekee ambayo inadumu kwa siku 30 Ina Mambo mengi ndani yake. Kwa kawaidaa gharama ya kozi hii huwa ni laki mbili (200,000). Ila kwa ofa ya leo. Mtu mmoja tu ambaye atalipia 120,000/- nitamuunganisha kwenye hii kozi. Ukiwa ndani ya hii kozi utapata Utajifunza mbinu za kitabu chako…

  • MAISHA YA NYOTA TANO

    Leo nimesikiliza audiobook ya kitabu cha Oprah Winfrey. Nimejifunza mengi sana ila hapa kuna kimoja tu ambacho ningependa na wewe ukijue.Oprah anasema kwamba, unaweza kuishi maisha ya nyota tano hata   hauna pesa sasa. Sio lazima ulale kwenye hoteli zenye viyoyozi ndio uanze kuishi maisha ya aina hii. Ebu ona ukiamka asubuhi na mapema. Basi jipe…

  • VITENDO VIZIDI MANENO

    Dunia ina tabia ya kukupatia kitu kama utaonesha nia, kuwa wewe ungependa kupata hicho kitu. Huwa ninapenda kuwaambia watu kuwa, hata kama ni bahati itakukuta njiani unatembea wala sio chumbani kwako ukiwa umelala. Kwa hiyo, wewe kama unahitaji kupata bahati maishani mwako basi kuwa tayari kuweka kazi inayoendana na bahati unayotaka. Bahati unaitengeneza wewe mwenyewe…

  • Leo najisikia kutoa ofa. Sema Toa Ofa basi 😂😂😂

    Hii ofa ni ya kipekee kwa ebooks zangu ambazo watu wanapenda sana. Ebooks hizi ni MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi ya kugundua, kunoa na kuendeleza Kipaji NGUVU YA WAZO (The power of an idea): How An Idea Can Change The World. Jinsi Wazo kinachoweza kubadili Dunia Thamani ya ebooks,…

  • THE SIMBA MENTALITY

    Karibu sana kwenye makala ya leo. Ni makala ndefu kidogo. Kwa wale wasiopenda kusoma vitu virefu sana hii ya leo inaweza isiwe makala ya aina yako. Ila wale ambao wanapenda kuzama ndani na kujifunza vitu kwa kina vilivyotafitiwa na kutafitika, basi vuta kiti maana unachoenda kujifunza hapa ni kitu kikubwa sana. Kwa siku nyingi sana…

  • Je, Kuna Haja Ya Kuendelea Kusoma Wakati Ajira Hakuna?

    Jana kupitia Temino ya Clouds FM niliongea na wanachuo wote hapa nchini, huku nikiwasisitiza juu ya umuhimu wa kutumia bumu lao la chuo vizuri maana kuna maisha baada ya chuo. Waendeshaji wa kipindi hicho ambao ni Harris Kapiga pamoja na Advovate Henry Mwinuka nao walisisitiza pointi muhimu sana kwa kusema kwamba kila mwaka kuna wahitimu…

X