Category: Uncategorized

 • Ni Vigumu Sana Kupata Mafanikio Makubwa Bila Ya Kuwa Na Sifa Hii Moja Muhimu

    Kwenye vitabu vitakatifu wanaeleza wazi kuwa mlango wa kuingia mbinguni ni mwembamba. Muda mwingine watakuambia kwamba wanaoitwa ni wengi ila wanaochaguliwa ni wachache. Sasa kitu hiki pia huwa kinajitokeza kwenye maisha ya kawaida ya mafanikio. Ni vigumu sana kupata mafanikio makubwa kirahisi, wengi wanapenda mafanikio makubwa ila wachache ambao wanaweza kufanikiwa na kufika mbali.…

 • Huu Ni Upande Ambao Ni Marufuku Kwako Kuuchagua

    Rafiki yangu, najua unafahamu kuwa una uhuru wa kuchagua chochote kile unachotaka kuwa. Unaweza kuchagua kuwa mwalimu, mchekeshaji, mshereheshaji, dereva, mkulima, mwanamichezo, mwanasiasa, mwanaharakati au chochote kile. Huo uhuru unao na wala hakuna mwenye uwezo wa kukuzuia wewe kwenye hilo. Hata hivyo, kuna kitu kimoja tu ambacho ningependa kukutahadharisha, na kitu hiki siyo kingine…

 • Hiki Kitu Tu,Kitakufanya Uwe Na Maisha Ya Kawaida

  Imewahi kukutokea ukaangalia labda igizo au ukasoma kitabu na kuona ni cha kawaida sana na wewe ungeweza kabisa kuigiza hilo igizo au ungeweza pia kuandika kitabu husika? Unajua kitu gani kinakutofautisha wewe na huyo aliyeigiza hilo igizo au aliyeandika kitabu husika? Kinachokutofautisha ni kuchukua hatua. Mwenzako anachukua hatua na kuigiza igizo alilo nalo ndani yake,…

 • Kwa Nini watu wengi husahau malengo ya mwaka mpya Mapema Sana

    Juzi tarehe 19 ilikuwa ni siku rasmi ambapo watu wengi huwa wanaacha kufanyia kazi malengo yao na kuanza kuishi maisha ya kawaida. Hii siyo siku ambayo nimeibuni bali ni kutokana na tafiti kuntu zilizofanywa na watafiti wanaoaminika duniani. Na siyo kwamba zimefanywa kwa watu kumi au ishirini, bali zimefanyika kwa watu zaidi ya milioni…

 • Usidharau vitu vidogo vina uwezo wa kukufikisha mbali Sana

  Mwaka 1969 binadamu kwa mara ya kwanza aliingia mwezini. Unaambiwa kompyuta iliyotumika kipindi hicho kumwingiza mtu mwezini ilikuwa na uwezo mdogo sana, uwezo wake ulikuwa mdogo mno kiasi cha kuzidiwa na simu janja tunazotumia sasa. Ila iliweza kutumika kutufikisha mwezini. Ndiyo maana nimekuwa nakushauri kuwa makini na vitu vidogo, kutokana na madhara au matokeo yatokanayo…

 • Leo ndiyo Siku Ambayo Watu Wengi Husahau Malengo Yao Ya Mwaka Na Kuanza Kuishi Kwa Mazoea

    Leo ni tarehe 19 jnuari 2022.  Ukiangalia tangu tuuanze mwaka huu, hata hatuna siku nyingi. Ila cha kushangaza ni kwamba kuna watu ambao tayari wameshasau malengo yao. Zimefanyika tafiti na imethibitishwa  kuwa tarehe 19 ya kila mwaka mpya, ni tarehe ambayo watu wengi huwa wanasahau malengo yao na hivyo kuendelea kuishi kimazoea. Swali langu…

 • Hakuna shida katika kupenda fedha…

  Mara nyingi sana huwa nasikia watu wananiambia kuwa unaipenda sana fedha wewe? Au wengine huwa wanasema “unaijua hela”! Na Mimi huwa nawajibu kuwa “ ndiyo naipenda fedha ndiyo maana na yenyewe inanipenda”. Au huwa nawaambia nilizaliwa nayo. Ninachotaka ufahamu ni kwamba kitu ambacho hukipendi hakiwezi kukupenda wewe. Kama huipendi fedha, ndiyo maana wewe ni masikini…

 • Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa

  Leo napenda kumtambulisha kwako mwajiriwa mtiifu kuliko wote duniani,  anafanya kazi kwa saa 24 siku saba za wiki. Hadai mshahara wala marupurupu yoyote. Yeye anachojua ni kufanya kazi kwa bidii kila wakati na kutoa matokeo kadiri unavyomwelekeza. Nimekuwa namtumia mwajiriwa huyu kwa siku nyingi sasa na hizi ndizo sifa nilizobaini kwake. Anaweza kusalimia wateja, Anaweza…

 • Kitu Kimoja Ambacho Hujawahi Kuambiwa kuhusu Kufanya Makubwa

    Kama unataka kufanya makubwa, unapaswa kuwa tayari kuishinda hofu na uoga unaokukabili unapoanza kufanya kitu hicho mwanzoni. Nakumbuka Kuna wakati nilikuwa naogopa na  kujiuliza kwamba nitaongea nini nikukutana na mtu fulani. Ila cha kushangaza muda kidogo baada ya kukutana na mtu huyo mazungumzo yalikuwa yanajiendesha yenyewe kiasi kwamba nilikuwa sijiulizi nitaongea nini. Hapo ndipo…

 • USHAURI MUHIMU: Kama una ndoto ya kuwa mwandishi na unawaza nani ATAHARIRI, ATACHAPA na jinsi utakavyouza kazi zako Basi Soma hapa.

  Siku ya leo najibu swali nililoulizwa na mmoja wa wasomaji wangu. Anasema; Hi Godius.Naitwa Juma Mazengo Malale, kwa sasa nipo Shinyanga, ndoto yangu nikuwa mwandishi wa vitabu. Mpaka sasa nipo kwenye mchakato, changamoto ipo kwenye mambo kama haya.1. Nani atahariri kazi yangu.2. Nani atachapa.3. Wapi nitauza.4. Nitamudu gharama5. Kitabu kibebe page ngapi?   Habari yangu…

 • USIPOJITAMBUA, KUNA WATU WACHACHE WANAOJITAMBUA WATAKUTUMIA WANAVYOTAKA

  Kuna stori moja ya mchungaji huko Nigeria, ambayo nimelazimika nikushikirishe kwa lengo la kukwambia kitu. Na stori hii ni ya mchungaji Dr. JS Yusuf wa Nigeria ambaye yeye ameanzisha utaratibu wa kuuza chupi kwa wanawake. Chupi hizi zina picha yake na anasema kwamba, mwanamke yeyote atakayevaa chupi hizi, atakuwa na mvuto kwa wanaume na ataweza…

 • Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?

  Jana nilienda kumtembelea mwalimu wangu wa shule ya msingi ambaye kwa sasa ni mstaafu. Kama ilivyo kawaida ya watanzania wengi, nilipofika alifungulia runinga ili tuburudike kwa kuangalia manjonjo ya kimambele. Alifungulia channel ya Clouds na nilipoangalia tu kwenye kioo cha runinga nilikutana na swali lililosema,  *Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio…

 • Kheri ya mwaka mpya 2022

    Huu ni mwaka ambao kwa hakika ulikuwa umeusubiria kwa hamu kubwa sana. Sasa hatimaye umefika. Wakati unajipongeza kwa mwaka mpya hakikisha1. Umeweka mipango dhabiti kwa ajili ya huu. Usiishi mwaka huu bila malengo. Ongozwa na malengo 2022. 2. Hakikisha unachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa nguvu zako zote bila kuchoka mwaka 2022. Binafsi nimechagua…

 • Kama hujui unachotaka sasa hivi, ukikiona kesho hutakifahamu pia

    Kuna watu huwa hawaweki malengo kwa kisingizio kwamba kitu chochote wanachotaka wakikiona watakifahamu.  Ila ukweli ni kwamba, kama kitu unachotaka hukijui, hata kesho ukikiona hutakifahamu. Ndiyo maana inashauriwa uwe malengo kwa sababu yanakufanya uone unachotaka. Na chochote kile ambacho akili yako inaweza kuona, basi inaweza kukifikia. Tembelea blogu yangu kupitia SONGA MBELE BLOG

 • ANZA KIDOGO

    Kama kuna kitu nimekuwa nasisitiza kila siku ni kuanza kidogo, kuanza na kile ulichonacho, kisha kuendelea kukuza hicho kidogo ili kutengeneza kikubwa zaidi. Ebu leo jiulize ni kitu gani kikubwa nimekuwa nataka kuanza kufanya ila sijaanza. Anza leo kidogo.

 • Masomo Matano Kuhusu Fedha Unayopaswa Kuyafahamu Katika Maisha

    Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine. Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu. 1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako. 2. Fahamu kuwa…

 • Kitu Kinachoashiria Kuwa Hutafika Mbali Kimafanikio

   Kuna vitu vingi ambavyo vinaashiria kuwa hutaweza kufika mbali kiuchumi, hata hivyo kimoja kikubwa sana kati ya vyote ni KUTOJIFUNZA. Kama  hupati muda wa kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu , jua hicho ni kiashiria cha wewe kuja kuanguka siku moja. Hili litatokea bila kujali unafanya kazi kwa bidii sana au una mtaji mkubwa, kwa…

 • Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia

  Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao.  Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao  unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni…

 • Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!

    Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene. Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha. Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki…

 • KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?

  Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza? Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangaliaWatu uliowalenga. Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza. Kwa hiyo badala ya kujiuliza…

X