Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Audiobook vs Ebook

    Audiobook ni kitabu kimesomwa kwa sauti (kitabu kinaweza kuwa kimechapwa au hakijapachwa, ila kikisomwa kwa sauti kinakuwa audiobook)

    Audiobook.ni neno la kiingereza ambalo linaundwa maneno mawili.
    Neno la kwanza ni
    audio=yaani sauti

    Na neno la pili ni book yaani kitabu.

    Kwa lugha nyingine tunaweza kusema audiobook ni KITABU SAUTI. Mfano wa kitabu sauti hiki hapa

    Kwa upande mwingine
    EBOOK ni kitabu cha kimtandao. Yaani, kitabu unachoweza kusoma kwa kutumia simu, kompyuta au tablet.

    Wengine hukiita kitabu hiki softcopy au kwa kiswahili nakala laini au nakala tepe.

    Ebook ni kifupisho cha ELECTONIC BOOK

    Ambapo
    Electronic maana yake ni ya kidigitali au ya kimtandao
    Na book ni kitabu.

    Hivyo ebook ni kitabu cha kimtandao au kidigitali😊😊

    Mfano, unaweza kupata kitabu cha kidigitali hapa

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Hii Ndiyo Fursa yako ya Kupata Nakala ya Kitabu cha The School of Money (Hardcopy) Bure Kabisa!

    Rafiki yangu mpendwa, ninaamini kuwa kila mmoja wetu anapenda kuwa na maisha bora zaidi, yenye uhuru wa kifedha na utulivu wa kiakili.

    Leo, nataka kuzungumza na wewe kuhusu kitabu cha kipekee ambacho kimekuwa kikisaidia watu duniani kote kufikia mafanikio ya kifedha. Kitabu hiki ni “The School of Money” ambacho kinaandikwa na mmoja wa wataalamu wa mafanikio ya kifedha, Olumide Emmanuel 

    Kama wewe ni mtu unayetaka kufikia mafanikio ya kifedha na kubadilisha maisha yako, basi hiki ndicho kitabu unachohitaji. Kitabu hiki kimejaa maelezo muhimu na ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kufanikiwa katika maisha yako ya kifedha.

    Hata hivyo, nimepata taarifa kuwa kitabu hiki ni adimu sana na kimekuwa kikiuzwa kwa bei kubwa sana sokoni. Hivyo, nimeamua kutoa ofa maalum kwako ambayo itakusaidia kupata kitabu hiki kwa bei nafuu sana.

    Kwa kununua nakala halisi za vitabu vyangu sita kwa bei ya laki moja (100,000/-), utapata zawadi ya kitabu cha The School of Money bure kabisa. 

    Vitabu hivi ni pamoja na 

    1. Nguvu ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa, 

    2. Jinsi ya Kufikia Ndoto Zako, 

    3. Maisha ni Fursa: Zitumie Zikubebe, 

    4. Jinsi ya Kuongeza Thamani Yako, 

    5. Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni, na 

    6. Kipaji ni Dhahabu.

    Hii ni nafasi ambayo hupaswi kuikosa. Unachotakiwa kufanya ni kulipia kiasi cha laki moja (100,000/-) kupitia namba ya simu 0684408755 kwa jina la Godius Rweyongeza.

    Nunua vitabu vyangu sasa na upate zawadi yako ya kitabu cha The School of Money bure kabisa! Hii ni fursa yako ya kipekee ya kufanikiwa na kuwa mtu bora zaidi. Usikose nafasi hii!

    Kujifunza kuhusu fedha na uwekezaji ni jambo muhimu katika kufanikiwa kifedha. Kitabu cha “The School of Money” ni chanzo bora cha kujifunza mbinu bora za kifedha na uwekezaji. Kwa kusoma kitabu hiki, utapata mwanga wa jinsi ya kuanza kuwekeza, kupanga bajeti, kudhibiti matumizi, na kufikia malengo yako ya kifedha.

    Kama ilivyojadiliwa katika makala hii, kununua nakala ya kitabu hiki kunaweza kuwa ghali. Hata hivyo, kwa kutumia ofa hii ninayotoa kwa mtu mmoja, unaweza kupata nakala yako ya “The School of Money” bure kabisa.

    HATUA za kuchukua:

    1. Jifunze zaidi kuhusu uwekezaji na mbinu bora za kifedha kwa kusoma “The School of Money.”

    2. Pata nakala yako ya kitabu hiki kwa kutumia ofa hii ambayo ataipata mtu mmoja, ofa hii itakupa nakala yako ya “The School of Money” bure kabisa.

    3. Fuata maelekezo kwa kulipia kiasi cha laki moja (100,000/-) kupitia namba ya simu 0684408755 kwa jina la Godius Rweyongeza.

    4. Baada ya kupata nakala yako ya “The School of Money,” kisome kwa umakini ili kujifunza mbinu bora za kifedha na uwekezaji.

    5. Tumia maarifa yako ya kifedha kuanza kuwekeza, kupanga bajeti, kudhibiti matumizi, na kufikia malengo yako ya kifedha.

  • Uchambuzi wa kitabu cha NO excuses

    Kitabu: No Excuse
    Mwandishi: Brain Tracy
    Mchambuzi: Hillary Mrosso

    Utangulizi

    Mwandishi wa kitabu hiki anataka tuwe watu wa matokeo na sio watu wa kutoa sababu kwanini hakuna matokeo. Maneno kidogo kazi zaidi, matokeo zaidi. Karibu tujifunze mambo 100 niliyoyaona ndani ya kitabu hiki kizuri.

    1. Kuna sababu zaidi ya 1000 kwa nini umeshindwa kufanya jambo fulani, lakini hakuna sababu nzuri kati ya hizo za kwanini umeshindwa.
    2. Kanuni ya kwanza ya mafanikio ni kujitoa kwenye kundi la wanaolalamika na kutoa sababu nyingi za kushindwa kufikia malengo yako na kuingia kwenye kundi la watendaji.
    3. Usiwe tena na visingizio vya kwanini hujafanya hiki au kwanini hujaweza kufikia malengo yako. Ondoa sababu na visingizio, maneno kidogo matokeo zaidi.
    4. Usitumie ubongo wako wa thamani kuunda au kujaribu kujitetea kwanini hujachukua hatua kufikia malengo yako, au kukamilisha mambo muihimu kwenye maisha yako.
    5. Mwandishi anataka tujiulize, je kuna mtu yeyopte duniani mwenye sababu na visingizio kama mimi na amefanikiwa? Usikubali sababu zikwamishe kufikia malengo yako.
    6. Fanya kitu na maisha yako, fanya tu jambo fulani muhimu na maisha yako, acha kutoa visingizio na sababu, sababu hazitakuletea mafanikio, just do something.
    7. Jishangaze wewe mwenyewe kwa kuwa mtendaji na kuondoka kwenye kundi la watu wa visingizio na maneno mengi. Maneno mengi hayatakuletea mafanikio, matendo na kuchukua hatua ndio huleta mafanikio.
    8. Unatakiwa kuwa na nidhamu ili uweze kuchukua hatua kufikia ndoto zako, bila nidhamu utakuwa mtu wa maneno meeengi, utakuwa na visingizio vingi na sababu zisizoisha.
    9. Ndidhamu binafsi ni ile hali ya kufanya jambo fulani ulilotakiwa kufanya kwa wakati ulioupanga, bila kujali unajisikia kufanya au hujisikii.
    10. Nidhani binafsi ndio huwafanya watu wa kawaida wasio na vipaji wala kudhaniwa kuwa na uwezo mkubwa kufanya mambo makubwa kwa ufanisi mkubwa.
    11. Mwandishi Brain anasema jambo la muhimu kwenye maisha yetu ni kuwa na nidhamu binafsi, anashauri tujidhibiti, tujiweze, tujitawale.
    12. Mafanikio yatakuwa yako pale ambapo utaweza kuthibiti hisia zako, hamu au matamanio yako na mitazamo yako.
    13. Watu wenye mafanikio makubwa ni wale wanaofikiri kwa mapana na kwa miaka mingi ijayo yaani long-term thinkers.
    14. Watu waliofanikiwa kwenye maisha wanafanyia kazi sana eneo lao la nidhamu binafsi kila mara.
    15. Kuwa na nidhamu kali ya kufanya kile ambacho ni sahihi.
    16. Watu waliofanikiwa wana tabia ya kufanya yale ambayo watu wasiofanikiwa hawafanyi.
    17. Tabia mbaya ni rahisi kuzitengeneza lakini ni ngumu kuishi nazo, lakini tabia njema ni ngumu kuzitengeneza lakini ni rahisi kuishi nazo.
    18. Kila tabia inafundishika na inawezkeana kujifunza na kuwa na tabia hiyo. Hivyo amua kuingiza na kujifunza tabia unazozitaka kwenye maisha yako.
    19. Kila unapojitahidi kutengeneza nidhamu kwenye eneo fulani la maisha yako, unatengeneza na kuimarisha eneo lingine la maisha yako.
    20. Kila unapokazana kutengeneza nidhamu kubwa kwenye maisha yako, ndio unavyoongeza Kiwango cha kujipenda na kujikubali. Watu wanaojipenda wanatenga muda wa kutengeneza mambo muhimu kwenye maisha yao.
    21. Kuna amani, furaha, hali ya kujiamini na kujipenda pale unapoongeza nidhamu kwenye maisha yako. Usikubali maisha yako yaende tu bila muongozo maalumu, dhibiti na amua vitu unavyosimamia kwenye maisha yako.
    22. Nidhamu itakufanya uishi maisha bora, maisha ya uhuru na salama, nidhamu itakuepusha na mambo mengi magumu, nitamu itakuvusha kwenye milima na mabonde ya maisha.
    23. Mwanafalsafa mahiri wa siku nyingi Plato aliwahi kusema, ushindi wa kweli ni ushindi unaopata dhidi yako mwenyewe. Maana yake pata ushindi kwenye mambo yaliyoko kwenye maisha yako ambayo yanakupa changamoto. Pata ushindi dhidi ya tabia mbaya zilizopo kwenye maisha yako.
    24. Inapofikia suala la kufanyia kazi ndoto zako, mawandishi anasema kuwa tayari kufanya kazi kwa muda mwingi zaidi kuliko mtu mwingine. Jitoe zaidi ya wengine kufanya kazi bora kwa muda wa kutosha.
    25. Utayari wa kuendelea kufanya kazi zako kwa muda mrefu zaidi unaupata pale unapokuwa na nidhamu kwenye maisha yako.
    26. Usipokuwa na nidhamu kwenye maisha yako, maana yake umewaachia wengine kazi ya kukusimamia, kukutawala, kukuongoza nk. Nidhamu itakufanya uwe kiongozi, maneja na bosi wa maisha yako.
    27. Kuna kanuni ya mafanikio inasema, kama utafanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya mara kwa mara bila kuachaa, hakuna kitakachokuzuia kufikia mafanikio unayaoyatafuta.
    28. Kila kilichopo kwenye maisha yako ya sasa ni matokeonya mambo uliyoyafanya siku za nyuma. Maana yake kila unachokivuna ni matokeoa ya kila ulichopanda siku za nyuma kwenye maisha yako.
    29. Mafanikio ni kujua kile unachokitaka kwenye maisha yako, kujua gharama ambazo utaingia kufikia mafanikio hayo, na kunuia au kudhamiria kulipa gharama hizo ili kufikia mafanikio yako.
    30. Upo tayari kiasi gani kulipa gharama za kufikia mafanikio unayoyataka? Fikiria tena kwa upya kama upo tayari ili uchukue hatua mara moja.
    31. Lipa gharama zote, na sio ulipe nusu nusu, lipa gharama zote kufikia mafanikio yako, hakuna njia ya mkato kwenye mafanikio ya kweli.
    32. Gharama za mafanikio zinalipwaga zote na zinalipwa kwanza kabla ya kuyapata mafanikio, maana yake inahitaji zaidi dhamira ya kweli kwenye safari ya mafanikio, hutaweza kufikia mafanikio unayotaka kama utakosa uvumilivu kwenye mchakato.
    33. Mwandishi anasema kuwa mbobezi kwenye eneo lako, maana yake kuwa mtaalamu uliyebobea kwenye jambo unalolifanya kama ni taaluma, kazi, Sanaa, biashara, au ujuzi ulio nao.
    34. Kuwa na mipango ya muda mrefe ya kuboresha ujuzi ulio nao, noa ujuzi ulio nao kila mara ili uwe mbobezi na uweze kuleta mafanikioa makubwa yatakayoacha alama.
    35. Faya yale yaliyo magumu lanini ni ya muhimu zaidi, kuliko kufanya vitu vyepesi visivyo na umuhimu, Brain Tracy anasema tumia nidhamu kali kwenye kufanyia kazi jambo hili maana sio rahisi.
    36. Ili uwe mtu ambaye hujawahi kuwa kabla fanya vitu ambavyo hujawahi kuvifanya kabla, maana yake kama unataka kuwa mtu wa tofauti fanya vitu tofauti, kama unataka kubakia yule yule miaka yote fanya yale yale uliyofanya maiaka yote.
    37. Zawadi kuu ya maisha ya mafanikio sio fedha utakazozipata, bali ni aina ya mtu bora utakayekuwa baada ya kufikia mafanikio.
    38. Wajibika kwa viwango vya juu sana kwenye maisha yako, ingia kwenye majukumu makubwa ya kuboresha maisha yako kuliko matarajia ya watu kwako.
    39. Shika hatamu ya maisha yako, usimpe mtu mwingine Jukumu hili, wajibika asilimia 100, hakikisha unakuwa na udhibiti wote wa maisha yako.
    40. Itakuhitaji utumie nguvu ya zaida kubadili maisha yako kuwa bora, itakugharim sana nguvu na nia ya kweli ya mabadiliko.
    41. Itakuchukua nguvu ya ziada ili kufanya kitu sahihi kila mara na kwenye hali zote.
    42. Tengeneza uaminifu na kuaminiwa kwenye maisha yako, na ukishatengeneza ulinde uaminifu wako kwa gharama zote.
    43. Maisha yanakuja kwetu kama mitihani na majaribio ili kutupima kama tupo tayari au tuna maanisha kwenye safari yetu ya mafanikio, kila hatua itakutaka kufanya maamuzi sahihi na kufanya kitu sahihi.
    44. Kila maamuzi utakayofanya yaaonysha thamani yako na hadhi yako. Hivyo chukulia kwa uzito maisha yako.
    45. Kila kitakachokuwa kinachukua muda na guvu zako kwa muda mrefu ndio kitatokea kwenye maisha yako. Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwenye maisha yako.
    46. Kumbuka changamoto hazitufanya kuwa watu fulani, bali zinatuonyesha sisi ni watu wa aina gani, hivyo zitumie changamoto kwa faida ya kuboresha zaidi.
    47. Mwanadamu mwenye hadhi ya chini sana hapa duniani ni yule ambaye hana maadili, hana tabia njema na hana misingi bora anayosimamia, yupo yupo tu, hana lengo lenye maana analotaka kukamilisha.
    48. Linda maadili na thamani yako isichafuliwe na mienendo ya maisha yako, linda jina lako lisichafuliwe na kashfa au sifa mbaya, linda sana hadhi yako isihusishwe na mambo mabaya.
    49. Jinsi unavyojipenda mwenyewe zaidi ndio jinsi utawapenda na wengine zaidi, na kwa kufanya hivyo upendo mwingi unarudi kwako.
    50. Fikiria tungekuwa na dunia gani kama kila mtu angekuwa anafanya na kufikiri kama wewe? Fikiria dunia ingekuwaje kama wote tungekuwa kama wewe.
    51. Dhamiria kuwa mtu bora kabisa kuwahi kuishi hapa duniani, kwa kufanya kazi bora, kuishi kwa nidhamu na kuacha kulalamika.
    52. Tathimini maisha yako, na ukiona hayakuridhishi yabadilishe ili yakuridhishe na yakufurahishe, kumbuka hakuna anayekuja kukusaidia kubadili au kukupa maisha mazuri, ni wewe mwenyewe unatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kuyafanya maisha yako yawe bora.
    53. Usiishi kwa mkumbo, jifanyie upembuzi yakinifu kila mara, jikague kila mara, na jisemee moyoni mwako, kweli haya ndio maisha ninayoyataka? Haya ndio maisha niliyochagua kuishi? Kicha chukua hatua mara moja kuyafanya maisha yako kuwa mazuri.
    54. Jiwekee utaratibu wa kujisomea vitabu bora kabisa ili uweze kuwa na mawazo, fikra bora za kukusaidia kufanya maamuzi mazuri kwenye maisha yako, jizoeshe kuwa msomaji wa vitabu.
    55. Mwandishi anasema kila mtu anayetaka kufikia kilele cha mafanikio kwenye jambo lolote, anatakiwa kwanza kuwa na mtaji wa tabia bora za kumsaidia kufikia lengo hilo kubwa, pia amesema awe tayari kuvunja tabia zinazokinzana na mafanikio unayoyataka.
    56. Hakuna atakayefanya kwa ajili yako, kumbuka jambo hili kila siku, ni wewe unatakiwa kubeba Jukumu la kuishi maisha yako kwa asilimia 100.
    57. Jitolee maisha yako kama sadaka ili ujifunze bila kukoma, jitoe bila kujibakiza ili upate maarifa na ujuzi unaoutaka kwenye maisha yako. Jifunze bila huruma, fanya jambo hili la kujifunza kuwa ni jambo la maisha yako yote, kamwe usiache.
    58. Jifunze ujuzi mgumu ambao unahitajika sana kwenye jamii, tumia muda wako na nguvu zako kujifunza ujuzi mgumu wenye thamani kubwa ambao ukiujua sio tu utakuletea mafanikio bali utakufanya kuwa mtu bora kabisa.
    59. Mwandishi anasema itakugharimu nguvu kubwa sana ili uache kutoa visingizio, kutoa visingizio ni rahisi sana, mwandishi anasema kata kabisa kutoa visingizio na sababu, toa matokeo.
    60. Tabia hazitakiwi kuwa kikwazo kufikia mafanikio yako, tabia zinatakiwa kuwa ni nyenzo muhimu za kufikia mafanikio, zifanye tabia zako zikusaidia na sio zikuharibie.
    61. Dawa ya kuua malalamiko, visingizio na sababu ni kukubali majukumu, sema nakubaliana na majukumu yote ya maisha yangu.
    62. Kuwa na muda wa kutosha wa kufanyia kazi mambo yako ya maana nay ale muhimu, hii itakufanya ukose muda wa kaunza kutengeneza hisia hasi na kufuatilia maisha ya watu wengine.
    63. Katika maisha tunafanya kazi kukamilisha malengo yetu au tunafanya kazi kukamilisha malengo ya mtu mwingine. Kuwa na malengo yako binafsi unayoyafanyia kazi kila siku.
    64. Kila siku chukua kalamu na karatasi uandike malengo yako makubwa ya maisha yako, hii itakufanya ukae kwenye msitari na ukumbuke una majukumu muhimu kwenye maisha yako.
    65. Mwandishi anasema hakuna malengo yasiyofikiwa, bali kuna muda wa kukamilisha malengo usiofikiwa, maana yake malengo yako yanatakiwa kufanyika ndani ya muda maalumu, usiweke malengo yasiyo na muda, weka muda wa kufikia malengo yako.
    66. Kughairisha mambo kunaiba sana muda wako na maisha yako. Usighairishe mambo muhimu kwenye maisha yako, kama jambo ni muhimu kwenye maisha yako usiliache bila kufanya.
    67. Washindi ni wale wanaochukua hatua hata kama hawana uhakika na mafanikio watakayopata.
    68. Kuchukua hatua na kuanza utekelezaji maana yake kuna vitu unatatua, kuna hatua unapiga, hii ni bora kuliko kuacha kuchukua hatua.
    69. Brian Tracy anashauri tuandike kila njia ambayo tunafikiri ni suluhisho kufikia malengo yetu, kuwa na utaratibu wa kuandika mawazo yako unayodhani ni njia za kukusaidia kufikia malengo yako.
    70. Pangilia majukumu yako kwa vipaumbele, la muhimu zaidi ndio lianze kisha lifuate ambalo ni muhimu nk. Weka vipaumbele kwenye majukumu yako, hii itakusaidia kukamilisha mambo muhimu itakuondolea matumizi mabaya ya muda.
    71. Ukishaweka vipaumbele vyako usianze kusubiria hali iwe nzuri ndio uanze utekelezaji, anza utekelezaji mara moja, usipoteze muda, wala usitengeneze visingizio au sababu.
    72. Kila siku uwe na kitu unakifanya kinachokusukuma kuyafikia malengo yako, hata kama ni jambo dogo kiasi gani usidharau, endelea mbele.
    73. Kumbuka siku zote za maisha yako kuwa, uwezo wako wa kujifunza hauna kikomo, uwezo wako wa kujua mambo mapya hauna kikomo; hivyo usijiwekee ukomo kwenye fahamu zako.
    74. Kwasababu kuna wengi waliofanikiwa na kuwa matajiri ni ushahidi mkubwa kuwa hata wengine wanaweza kufikia mafanikio na utajiri mkubwa.
    75. Mwandishi anasema amua kuwa bingwa na mbobezi kwenye kile unachokifanya, kuwa na msaada na mchango tegemezi, watu wakutafute kwasababu unajua na unaweza kuwasaidia.
    76. Soma angalau dakika 60 kila siku kwenye kila kitu unachokifanya, boresha ujuzi wako kila siku kwa kusoma mawazo mapya.
    77. Sikiliza mafunzo yanayoelimisha kuhusu kile unachokifanya au ule utalaamu wako; kamwe usihitimu elimu yako.
    78. Hudhuria semina, kozi au mafunzo mbali mbali kwenye kuboresha ujuzi wako. Usiache kujifuza na kukua kila siku.
    79. Kama haukui maana yake unakufa, hakikisha unaongeza vitu vipya vya kukufanya kuwa bora, kukua na kuwa mtu bora na wa kipekee kwenye kazi yako, biashara, Sanaa, nk
    80. Mwandishi Brain anasema TV yako inaweza kukufanya kuwa tajiri endapo utaizima, maana yake usitumie muda mwingi kuangalia vipindi vya TV au kufuatilia mitandao ya kijamii, itakupotezea muda wako wa thamani kubwa.
    81. Lisaa la kwanza kwenye siku yako ni rada yako ya kukupa uelekeo wa siku yako, hivyo tumia vizuri lisaa la mwanzo wa siku yako.
    82. Ujasiri sio kukosekana kwa hofu, bali ni kuidhibiti hofu, kuitalwala hofu. Katika safari ya mafanikio tunahitaji sana ujasiri ili kuzuia hofu zisiturudishe nyuma.
    83. Ili utengeneza ubora ambao huna, unatakiwa kufanya kila kitu kwenye maisha yako kwa ubora unaotamani hadi ufikie ubora huo.
    84. Hakuna anayeweza kukufanya ukajihisi au kujisikia mnyonge na duni bila ya wewe kuruhusu kujisikia hivyo, usiamue udhaifu ndio utawale maisha yako.
    85. Kwenye maisha unahitaji ujasiri kila mahali, ujasiri wa kuchukua hatua, ujasiri wa kukataa kutoa sababu, ujasiri wa kuwa mvumilivu na kuendelea kuvumilia.
    86. Kuwa na ujasiri wa kuikabili hali inayokutia hofu, zikabili nyakati na hali unazoziogopa.
    87. Chukua hatamu ya kuzikabili na kuzithibiti dhoruba za moyo wako, maisha yametawaliwa na nyakati ngumu nyingi. Hivyo chukua uongozi wote wa maisha yako ili uzikabili bila uoga.
    88. Mark Twain aliwahi kusema, aliogopa vitu vingi sana kwenye maisha yako, na kati ya vingi alivyoogopa hakuna vilivyotokea kweli.
    89. Tegemea mabaya yanaweza kutokea kwenye maisha yako, usiogope na tengeneza ujasiri wa kukubali kila matokeo utakayoyapata.
    90. Anza mara moja kufanyia kazi mabaya au changamoto zilizotokea kwenye maisha yako, tafuta suluhisho la changamoto hizo.
    91. Kuwa kinganganizi kwenye safari yako, usiyumbishwa na kukosa muelekeo, kuwa buzi na majukumu yako, maana ndio yana maana sana kwako.
    92. Uvumilivu utakujengea misuli ya kusubiria na kukaa kwenye mchakato kwa muda mrefu, tengeneza na kubali kukaa kwenye mchakato wa mafanikio.
    93. Tengeneza nidhamu kubwa ya kukaa kwenye mchakato, hii itakufanya ujione mwenye heshima na kuongeza ujasiri na kujikubali.
    94. Kabla ya kuanza kufanya jambo kubwa na la muhimu kwenye maisha yako unaweza kujiambia kauli hii “sitakata tamaa, mimi sizuilike”.
    95. Hatakama utanguka chini na kuvuja damu mara nyingi, inuka tena uendelee na mapambano, hadi ufikie malengo yako.
    96. Jione wewe ni mtu mwenye nguvu, na una nguvu ya kustahimili magumu na changamoto zitakazokuja kwenye maisha yako, jikubali kuwa unaweza kuvuka kila changamoto itakayotokea kwenye maisha yako.
    97. Kamwe, kamwe usitumie nguvu na muda wako wa thamani kubwa kufanya mambo yasiyo muhimu, fanya mambo muhimu na ya maana sana kwenye maisha yako na kwenye jamii yako.
    98. Wewe ni kiongozi wa maisha yako, na kiongozi mzuri lazima awe na nidhamu kubwa na kali kwenye maisha yake, kupanga, kujiandaa, na kuwa na malengo yanayofikiwa.
    99. Usisema kitu chochote kuhusu mtu fulani ambacho haupo tayari kukisema mbele yake, maana yake usimsema mtu mwinge vibaya.
    100. Dhamiria kufanya vizuri kwenye siku za maisha yako zilizobakia. Nguvu zako na siku zako zilizobakia hapa duniani zitumie kuboresha maisha yako yaliyosalia. Hata kama umebakiza siku chache za kuishi hapa duniani. Kuwa mtu bora.

    Asante kwa kusoma uchambuzi wa kitabu hiki, hiki ni kitabu kizuri sana, nashauri kila mtu akisome, ni kitabu kifupi na chepesi sana kukisoma. Usiache kumshirikisha mtu mwingine uchambuzi wa kitabu hiki. MANENO KIDOGO, KAZI ZAIDI, MATOKEO ZAIDI.

    @Hillary Mrosso_30th April, 2023

  • Unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato, la sivyo utakuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko

    Rafiki yangu mpendwa Salaam

    Sina shaka unaendela vizuri kabisa

    Siku ya leo nataka kukwambia kwamba unapaswa kuwa na vyanzo vingi vya kipato la sivyo utakuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko. Hata hivyo, kabla hujaishia hapa na kwenda kukimbizana kuanzisha vyanzo vingi vya kipato. Ningependa tu uwe na subira, nasema uwe na subira kwanza ili usome makala hii mpaka mwisho ndiyo uende kufanyia kazi kile utakachojifunza.

    Kuwa na maarifa nusu ni hatari sana. Hivyo kusoma makala nusunusu ni hatari na kunaweza kusiwe na manufaa kwako kama kuisoma makala yote kamil.

    Namaanisha nini ninaposema vyanzo vingi vya kipato

    Vyanzo/chanzo kwa umoja ni chimbuko la kitu fulani. Vyanzo vya kipato ni chimbuko la fedha ambazo unakuwa unapata. Hivyo ninaposema kwamba uwe na vyanzo vingi vya kipato, maana yake uwe na machimbuko mengi yanayokuingizia kipato kwenye akaunti yako ya benki.

    Chanzo maarufu ambacho kimezoeleka kwa watu wengi, ni chanzo cha mshahara. Hata hivyo, kwenye ulimwengu wa leo, kuwa na vyanzo vingi siyo tena ombi. Ni lazima

    Na ukweli ni kwamba siyo vigumu kiviiile kutengeneza vyanzo vingi vya kipato kwenye ulimwengu wa leo. Lakini pia siyo rahisi kama unavyoweza kufikiria.

    Changamoto iliyopo unapokuwa na chanzo kimoja cha kipato

    Unapokuwa na chanzo kimoja cha kipato ni kwamba chanzo hicho kinaweza kukwama kipindi fulani na hivyo kukufanya usiweze kuingiza pesa kama ambavyo unakuwa unataka. Au pale chanzo hicho kinapochelewa kuingiza kipato na kama ulivyokuwa unategemea basi moja kwa moja unakuwa unaenda kugonga mwamba.

    Jinsi ya kuondokana na changamoto ya chanzo kimoja cha kipato

    KWENYE biashara na kwenye maisha, hakuna namba mbaya kama sifuri na moja. kitu chochote kile unachozidisha na mojakinabaki kuwa vilevile. Wakati ukizidisha kitu chochote na sifuri kinabaki kuwa sifuri.

    Hivyo rafiki yangu, ninachotaka kukwambia hapa ni kwamba unapaswa kuepuka kitu hiki kwenye maisha yako rafiki yangu. Epuka kuwa na chanzo kimoja cha kipato kadiri uwezavyo. Usiwe mtu ambaye unasema kwamba hauna kitu cha kufanya (Yaani 0) na wala usiwe mtu ambaye unategemea chanzo kimoja cha kipato. Badala yake kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Yaani, walau kuwa na vyanzo vinne au vitano na zaidi vya kipato.

    Usipokuwa na vyanzo zaidi ya kimoja cha kipato, ni suala la muda tu utaanza kuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko. Unajua kwa nini? kwa sababu utaanza kujiingiza kwenye kukopa,  utaanza kujiingiza kwenye vikoba, utaanza kufanya vitu vingi ambavyo siyo sawa na mwisho wa siku utakuta kwamba umeanza kuwa na vyanzo vingi vya mahangaiko.

    Suluhisho la hili rafiki yangu ni kuhakikisha kwamba unakuwa na vyanzo vingi vya kipato. Vyanzo vingi vya kipato vitakusaidia wewe kujiondoa kwenye majanga kama hayo ya mikopo lakini pia kukupa kipato pale unapokuwa unakihitaji.

    Kuhakikisha kwamba unapata mwongozo wa kukutosha kwenye kutengeneza vyanzo vingi vya kipato. Nimeandaa ebook. Ebook yenyewe hii hapa

    Kwenye ebook hii unaenda kujifunza yafuatayo.

  • NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA: Na Kwa Nini UnAHITAJI Kumaliza Kile Ulichoanza

    pata kitabu hiki kwa shilingi 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy
    pata kitabu hiki kwa shilingi 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy

    Rafiki yangu mpendwa, Salaam

    Juzi tumezindua kitabu kipya cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Na kwa nini unapaswa kumaliza kile ulichoanza. Hiki ni moja ya kitabu kizuri sana ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba umepata nakala yake mapema.

    Najua, umekuwa unataka kufanya makubwa.

    Lakini changamoto yako kubwa imekuwa aidha ni kuchukua hatua ya kwanza. Au la umekuwa unachukua hatua ya kwanza lakini umekuwa humalizi kile ulichoanza.

    Ukisoma hiki kitabu, siyo tu kwamba utaanza kuchukua hatua ya kwanza. Bali pia utakuwa na uwezo wa kumaliza kila unachoanza.

    Hiki ni kitabu kwa watu ambao wako tayari kuchukua hatua. Lengo la hiki kitabu siyo kwamba usome na uanze kujisifia kwamba umesoma kitabu. Bali ni kitabu cha vitendo zaidi.

    Yaani, ukisome, uchukue hatua na ukamilishe kile ulichodhamiria kufanya.

    Najua umekuwa unapata changamoto kwenye hilo suala. Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kulipia hiki kitabu ili uweze kukipata mikononi mwako.

    Gharama ya hiki kitabu (softcopy) ni 10,000/- ila tuna ofa ambayo inaisha kesho jioni.

    Kwa ofa hii unaenda kupata kitabu hiki kwa shilingi elfu saba 7,000/-

    Changamka sasa ili uweze kupata kitabu chako. Leo hii.

    Lipia 7,000 ili upate nakala laini (softcopy) yako sasa hivi. Tuma fedha yako kwa namba ya simu 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Kumbuka, Hii ni nguvu ya kuchukua hatua ya kwanza na kwa nini unapaswa kumaliza kile ulichoanza.

  • Leo siku ya kitabu duniani…..

    Frederick Douglass alizaliwa akiwa mtumwa kwenye mashamba ya huko Maryland nchini Marekani. Akiwa na umri wa mwaka 1 alitenganishwa na mama yake, ambapo hiki kinasemekana kilikuwa ni kitu cha kawaida sana kufanyika miongoni mwa watumwa.

    Hivyo, Frederick Douglass alikuja kukutana mama yake mara nne zaidi kwenye maisha yake kabla mama yake hajaaga Dunia.

    Akiwa kama mtumwa na miaka 8 aliepelekwa Kwa mmiliki wake mpya. Akiwa huko mke wa yule mmiliki wake akawa ameanza kumfundisha kusoma na kuandika. Hata hivyo, kabla masomo ya kusoma na kuandika hayajachanganya, yalisitishwa baada ya mmiliki wake kugundua kuwa mke wake alikuwa anamfundisha Frederick Douglass kusoma na kuandika.

    Yule bwana alisema kwamba kisheria watumwa hawaruhusiwi kufundishwa Wala kuandika. Na isitoshe mtumwa akifundishwa kusoma atakuwa hashikiki. Kitu hiki kiliachavalama kubwa kwenye kichwa Cha Frederick Douglass. Kuanzia hapo akaanza kutafuta kila namna ya kujifunza kusoma maaana alishaona NJIA pekee ya yeye kutoboa kimaisha ilikuwa ni kujua kusoma na kuandika.

    Ilimchukua Frederick Douglass miaka saba mpaka kujua kusoma na kuandika. Akawa ameanza kusoma vitabu, hasa vile vilivyokuwa vinahamasiha kukomesha utumwa

    Baadaye kwenye maisha yake Frederick Douglass alikuja kuwa mtu mkubwa sana. Mshauri mzuri Kwa Marais wawili wa Marekani. Abraham Lincoln na rais Andrew Johnson

    Ebu pata picha mtu ambaye alikuwa mtumwa, hakusoma shule Wala chuo chochote alivyoweza kufikia HATUA ya kufanya makubwa kiasi hicho.

    Nimeamua nianze na stori hii ya Frederick Douglass Leo hasa ukilinganiaha kuwa Leo ni siku ya kitabu duniani.

    Tunaishi kwenye zama zenye vitu vingi sana, ila kitu ambacho Bado hakijapoteza nguvu yake ni kusoma na kujifunza.

    Kusoma siyo tu kwamba kilikuwa muhimu enzi za akina Frederick Douglass, Bali mpaka Leo hii.
    Kwenye kitabu Cha Future shock, mwandishi Alvin Toffler

    Anasema mjinga wa Karne ya 21 siyo yule ambaye hajui kusoma na kuandika. Bali mjinga wa Karne ya 21 ni yule anayejua kusoma na kuandika ila hasomi wala kuandika….

    Sasa basi Leo ikiwa ni siku ya kitabu duniani. Nipende kukusisitza sana juu ya umuhimu wa kusoma vitabu, kama ambavyo nimewahi kuandika na kusisitiza juu ya umuhimu huu kwenye kitabu changu Cha MAAJABU YA KUSOMA VITABU

    Hiki ni kitabu hiki Huwa nakitoa Bure kama zawadi Kwa watu wangu wa nguvu kama wewe. Kama hujawahi kusoma kitabu hiki, Sasa huu ndiyo muda wako wa kukisoma.
    Kipate hapa.
    Au unaweza Kusikiliza kilichosomwa Kwa sauti hapa.👇🏿👇🏿

    Aidha Kwa upande mwingine siku ya Kimataifa ya kusoma vitabu au International Book Day inaadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Aprili. Lengo la sikukuu hii ni kusherehekea vitabu na kusisitiza umuhimu wa usomaji, kukuza utamaduni wa kusoma na kuboresha uelewa wa kijamii kwa ujumla.

    Siku hii ilitangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mnamo mwaka 1995, na tarehe ya maadhimisho 23 Aprili ikichaguliwa kuwa heshima ya waandishi wawili maarufu William Shakespeare na Miguel de Cervantes, ambao walifariki siku hiyo hiyo mwaka 1616.

    Siku ya Kimataifa ya Vitabu inaadhimishwa kwa njia mbalimbali duniani kote, ikiwa ni pamoja na matamasha ya vitabu, hafla za kusoma, mihadhara, na shughuli za kupata vitabu vya bure au vitabu kupunguzwa bei. Siku hii pia hutumika kutoa hamasa kwa watu wote, hususan vijana, kuanza kusoma vitabu na kuendeleza utamaduni wa kusoma kama sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku.

    Rafiki yangu nataka uitumie vizuri siku ya Leo.
    Na Kwa kuwa ni siku ya kusoma vitabu duniani. Leo utapata ebooks zangu zote kwa sh 7,000/- tu badala ya 10,000/-

    Audiobooks utazipata Kwa 5,000/- badala ya 10,000/-

    Changamka Sasa upate ofa hii. Hii ni ofa ya Leo. Na ni ofa ya Leo tu. Mwisho ni saa nne usiku.

    Cha kufanya, fanya malipo ya kitabu chochote unachopenda kwa Namba ya simu 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Kisha niambie ni kitabu kipi umelipia nikutumie.

    Enjoy siku ya kitabu duniani

    Cheers!

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Hiki ni kitu kitakachobadili maisha yako yote kuanzia leo……

    Mwaka Jana kwenye maonesho ya nanenane nikikutana na Dada Mmoja. Huyu dada alikuwa akipanga Kwa miaka mingi kuandika kitabu ila akawa haandiki.

    Sasa Leo hii alikuwa na swali Moja tu kwangu

    “Godius”, alisema. “Hivi Nina shida Gani? Kwa nini kila mwaka napanga kuandika ila sijawahi kuandika? “Nifanyeje ili niweze kuanza kuandika” Aliendelea

    Nilikaa naye na kuongea naye, leo hii tayari ameandika kitabu Cha kwanza kinekamilika. Sasa hivi anamalizia kuandika kitabu Cha pili.

    Kilichomkuta hugu dada kinawakuta watu wengi pia.

    Ebu Kwa mfano pata picha ni mara ngapi umekuwa unataka kuanza mazoezi.
    Ni mara ngapi umepanga kuweka akiba lakini hujafanya hivyo. Au ni mara ngapi umehamasika kujifunza na kusoma kitabu lakini hukufanya hivyo?.

    Hivi unajua hii tabia imekugharimu kiasi gani? Yaani, kutokuchukua kwako HATUA unajua kumekusababishia Nini?.
    Ni wazi kuwa laiti kama ungekuwa umeanzisha biashara yako ungekuwa tayari unafanya kile unachopenda. Au kama ungekuwa umeamua Kwa dhati kuandika basi ungekuwa umeshaandika kitabu chako.

    Ni wazi kuwa ungekuwa umeweza kuweka akiba pia, maana tangu mwaka ule ulipopatavkazi, mpaka Leo hii usingekuwa unahangaika, tayari ungekuwa na akiba yako ya kutosha tu.

    Lakini Leo hii unajionaje?

    Tukirudi kwa dada yetu tukiyeanza naye hapo mwanzo. Alikuja kugundua kuwa kuandika kitabu siyo kitu kigumu sana baada ya kuwa amechukua HATUA kama nilivyokuwa nimewelekeza.

    Unaweza kuangalia picha hii hapa chini kuona anachosema yeye mwenyewe Kwa maneno yake.

    Unajua nilifanyaje mpaka huyu dada akaweza kufanya haya yote.
    Nilimweleza vitu viwkubwa.

    1. Kwanza nilimweleza NGUVU YA KUCHUKUA HATUA KWANZA. Na nikamwonesha kwamba anapaswa kuweka kitabu chake kwenye uhalisia. Kuhakikisha kinakamilika.

    2. Lakini sikuishia hapo, nilimpa pia mwongozo wa kitabu kinachoitwa JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU.

    Hivi ni vitu viwili ambavyo nataka na wewe upate siku ya Leo.

    Chukua HATUA Leo hii upate
    Kitabu Cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KUCHUKUA chenye mwongozo kamili wa kukusaidia wewe kuanzia kufanyia KAZI kitu chochote ambacho umekuwa unatamani kufanya.

    Mtu yeyote ambaye amekuwa anakwama kuchukua HATUA ya kwanza. Anaweza kuchukua HATUA ya kwanza baada ya kusoma hiki kitabu.

    Mtu yeyote ambaye amekuwa akiwaza kuanzisha biashara, ataweza kuanzisha biashara yake bila shida yoyote mara tu baada ya kusoma hiki kitabu.

    Mtu yeyote ambaye amekuwa anakwama kuweka akiba, ataanza kuweka akiba mara baada ya kuwa ameanza kusoma kitabu hiki Cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.

    Kama umekuwa unapanga mipango yako ila unashindwa kuifanyia KAZI suluhisho hiki ni kitabu.

    Na sasa upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi yatakayobadili maisha yako. Nafasi ya wewe kuanza kufanyia KAZI vile vitu ambavyo umekuwa ukitamani kufanya au kuendelea na maisha yako ya kawaida.

    Kama utaamua kuendelea na maisha yako ya siku zote maana yake utaendelea kupata matokeo yaleyale ambayo umekuwa unapata mara zote na siku zote….

    *Lakini kama unataka kitu Cha tofauti kitokee kwenye maisha yako. Kama unataka kubadili mwelekeo wa maisha yako, utapaswa kufanya kitu Cha tofauti fanya Uamuzi wa tofauti na chukua HATUA ya kwanza Sasa
    Na HATUA hii ni kulipia ili kupata ebook ya kitabu Cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.
    Lipia Sasa hivi ili uweze kupata kitabu chako.

    Gharama ya kitabu ni 10,000/- ila Kwa ofa ya Eid unakipata Kwa 7,000/- tu.

    Aidha, ktabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU kinapatikana Kwa 10,000/-

    Ila kama utalipia vitabu vyote viwili Kwa Leo utavipata Kwa 15,000)- tu.

    Sikikiza, chukua HATUA Sasa hivi.
    Lipia kitabu hiki Kwa 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Kwa kusoma vitabu hivi nakuhakikishoa kitu kimoja. Zile ndoto zako ambazo umekuwa nazo Kwa siku Sasa. Yaani, Ile ndoto yako ya kuanzisha biashara itatimia.
    Ndoto yako ya kuandika itatimia.
    Ndoto yako ya ndoto ya kuweka akiba na kujenga utajiri itatimia.

    Nakuhakikishia kitu kimoja tu baada ya kusoma kitabu hiki. KUCHUKUA HATUA YA KWANZA NA KUANZA. Na siyo tu kwamba utachukua HATUA ya kwanza. Bali utakuwa na uwezo wa kukamikisha kile ukichoanza bila shida yoyote.

    Kwa kusema hivi basi fanya kitu kimoja. Lipia 7,000/- kitabu Cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA Leo hii.

    Au lipia 15,000/- upate vitabu viwili. Kitabu Cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA pamoja na JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU

    Badala ya 20,000/- jumla utalipia 15,000/- tu.

    Malipo yote yafanyike Kwa 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Fanya hivyo Sasa hivi.

    Ni Mimi Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Fanya kazi na kitu unachotaka kufanya kwa ubora

    Katika kazi au kitu chochote kile utakachoamua kufanya. Weka moyo, akili na kila kitu kwenye hicho kitu. Yaano, zama kabisa kwenye kile kitu kiasi kwamba hakuna kitu ambacho kinapaswa kukutoa wewe kwenye reli ya kukamilisha hicho kitu.

    Yaani, kwenye hili nataka upate mfano wa simba. Si unamjua Simba si mnyama mkubwa kuliko wote mbugani. Simba si mnyama mwenye akili sana kuliko wote. SIMBA si mnayama mwenye nguvu sana kuliko wote mbungani.

    Lakini cha kushangaza ni kwamba simba ara zote anaitwa Mfalme wa nyika. Unajua kwa nini anaitwa mfalme wa Nyika.

    Sababu ni moja tu

    Ni kwa sababu huwa anathubutu, na huwa akiamua kufanyia kazi jambo lake huwa harudi nyuma. Hiki ni kitu ambacho kinamtofautisha na wanyama wengine.

    Mpaka kuna usemi unaosema kwamba ni bora kuwa na kundi la kondoo ambalo linaongozwa na simba kuliko kuwa na kundi la simba linaoongozwa na kondoo.

    Kwa nini? Kwa sababu simba akiamua, ameamua. Harudi, na wala harembi mwandiko. Sasa katika mazingira kama hayo, simba akiwa na kondoo ni wazi kuwa kondoo nao watafuata mkondo wake.

    Lakini kondoo akiwa anaongoza kundi hilo, basi ni wazi kuwa akiongopa na akageuza mbio, basi ni wazi kuwa  hata wale simba watakimbia

    Kwenye maisha yako rafiki yangu. Kuwa simba.

  • Tumezindua kitabu kipya! Haya hapa ni mambo ya msingi sana unayopaswa kufahamu kuhusu hiki kitabu

    Rafiki yangu mpendwa, Salaam
    Moja ya kitu ambacho huwa kinanipa furaha kubwa ni pale ambapo huwa naandika kitabu, na kukikamilisha. Ni vigumu sana kueleza kwa UNDANI mchakato wote wa kuandika kitabu kwa ukamilifu. Ila furaha ile unayoipata baada ya kumaliza kuandika kitabu, ni furaha isiyo na kifani! Hivi unaijua furaha isiyo na kifani kweli……Hahaha

    Enewei, leo tarehe 21/4/2021 ni moja ya siku kama hizo.
    Ni siku ambapo nina furaha kubwa kutambulisha kwako kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. NA KWA NINI UNAHITAJI KUMALIZA KILE ULICHOANZA.
    Kitabu hiki kinapatikana katika mfumo wa nakala ngumu na nakala laini. Na utatumiwa popote pale utakapokuwa duniani.

    Labda kwanza tujiulize unaenda kujifunza nini kwenye hiki kitabu na kwanini unapaswa kununua hiki kitabu?
    Kama kichwa cha kitabu kinavyosema. Kwenye hiki kitabu unaenda kujifunza nguvu ya kuchukua hatua ya kwanza. Lakini siyo tu kwamba tutaishia kukuonesha wewe nguvu ya kuchukua hatua ya kwanza, bali tutaona kwa nini haswa unapaswa kumaliza kile unachopanga.

    Watu wengi sana huwa wanakuwa na ndoto kubwa za kuanzisha na kufanyia vitu. Ila kiuhalisia huwa hawafanyii kazi hivyo vitu. Hivyo, mwisho wa siku huwa wanaendelea kuwa na ndoto kubwa ambazo huwa hawazifanyii kazi.

    Unakuta mtu aliyekuwa na ndoto ya kuandika kitabu, ni mwaka wa saba ila hajaandika.
    Unakuta mtu alikuwa anasema kwamba ataanzisha biashara tangu mwaka 2010 mpaka leo hii bado anasema tu kwamba ataanzisha biashara.
    Unakuta mtu alikuwa anasema kwamba atawekeza au atamfungulia mwanae akaunti, tangu amezaliwa mpaka leo hii mtoto anaelekea kuanza shule, akaunti haijafunguliwa.
    Sasa kwenye hiki kitabu tunaenda kuona NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.

    Lakini haitoshi tu kuchukua hatua ya kwanza.

    Kumaliza kile ulichoanza ni jambo la msingi na sekondari kabisa. Hivyo hatuishia tu kuona kwamba unapaswa kuanza kufanyia kazi vitu. Bali unapaswa kumaliza kile ulichoanza. Yaani, ukifanyie kazi mwanzo mpaka mwisho.

    Siyo uanze kuweka akiba leo. Kesho uache
    Siyo uanze kufuga kuku leo, kesho ndiyo tukukute umeanza kulima tikiti, kesho kutwa tukukute umeagiza mzigo china, na siku nyingine tukukute umeanza kuwekeza kwenye cryptocurencies.

    Kumbe kwa mantiki hiyo ni kwamba, unapaswa kuanza. Lakini siyo tu kuanza, bali kabisa kuhakikisha umekamilisha kile ulichoanza.

    hiki kitabu ni mwongozo. Na ni mwongozo unaopaswa kuufuata.
    Kama nakuona vile kitakavyokusaidia kuondokana na lile tatizo lako ambalo limekuwa linakusumbua la kukosa mtaji. ANZA.
    Umekuwa unahofia kuongea mbelea ya watu. ANZA, KUJENGA UWEZO WAKO WA KUONGEA MBELE YA WATU.
    Umekuwa unatata kuweka akiba. ANZA tena leo hii.
    Umekuwa unatamani sana kusoma vitabu. Unasubiri nini. ANZA
    Umekuwa unataka kufanya kitu gani….ANZA.

    Kitabu sasa kipo tayari. Ni juu yako sasa kuchukua hatua ya kwanza ya kupata kitabu hiki.
    Kisha baada ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Utapaswa kusoma kitabu hiki na kukimaliza mpaka mwisho. Hapo utakuwa umeanza vizuri kwenye NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA.

    Njoo ujipatie nakala yako siku ya leo rafiki yangu
    Nakala ngumu yakitabu ni 20,000/- utaongeza 5,000 ya kutumiwa.
    Na nakala laini ni 10,000/-

    Ila siku ya leo nina ofa.
    Kama utachukua nakala laini softcopy na kulipia siku ya leo. BADALA YA KULIPIA 10,000/- unaenda kupata hiki kitabu kwa 7,000/-

    Hii ni ofa ya IDDI na itadumu kwenye hiki kipindi cha EID tu. Hivyo, itaduu mpaka tarehe 25. Baada ya hapo, hutaweza kupata hiki kitabu kwa hiyo bei.
    Cha kufanya sasa hivi ni kitu kimoja tu. Wasiliana na 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    ViTU VYA NYONGEZA UTAKAVYOPATA ENDAPO UTACHUKUA KITABU HIKI LEO HII
    Kwanza, utapata usimamizi wangu wa karibu wa siku 30. Utachagua kitu chochote ambacho umekuwa unatamani kufanya. Halafu utaniambia na nitakufuatilia kwa siku 30 mfululizo kuona mwnendo wako na namna unavyokifanyia kazi.
    Pia, utapewa zawadi ya kitabu cha NGUVU YA KUWEKA MALENGO.
    Njoo upate nguvu ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Ili uweze kujifunza NGUVU LIYOLALA kwenye kuchukua hatua ya kwanza.
    Lipia 7,000/ sasa kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
    Lipia sasa upate kitabu chako.

    NB: Hardcopy haina ofa kwa sasa hivi.
    Ila softcopy, unaipata kwa 7,000 badala ya 10,000

    Ni mimi rafiki yako
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    MOROGORO

  • Fanya kitu hata kama ni kidogo

    Fanya kitu kimoja kila siku ambacho kinakuogopesha. Fanya kitu hata kama ni kidogo. VItu vidogo mwisho wa siku ndyo huwa vinaleta matokeo na mafanikio makubwa sana. Kuna watu wanafikiria kuwa na mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara. Kuna watu wanafirikia juu ya kuja kuwa mabilionea.

    Hilo lengo ukiliangalia ni lengo kubwa sana. Lakini  sasa kulifanyia kazi kwenye uhalisia, ni kazi.

    Ndiyo maana unahitaji kulifanyia kazi hata kama ni kidogokidogo . Pata picha kila siku ukifanya jambo moja dogo, tena ukalifanya kwa mwendelezo na bilakuacha, ni wazi kuwa baada ya muda utakuwa umeweza kufanya makubwa.

    Mfano, kama kila siku ukiweka akiba, ni wazi kuwa akiba hii kidogokidogo, baada ya muda itakuwa imeweza kuwa akiba kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria.

X