Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Omba Utapewa

    MOJA YA ujuzi ambao una-paswa kuwa nao ni ujuzi wa kuomba. Yaani, kuomab kitu unachotaka kutoka kwa watu wenye nacho. Hiki ni kitu ambacho watu waliofanya makubwa huwa wanafanya.

    Wanaofanya makubwa siyo kwamba wanaweza kufanya kila kitu hapa duniani. Hapana, wanaweza kufanya vitu vichache, ila sasa kwa vile vitu ambavyo hawawezi, basi wanaomba wengine waweze kuwapa msaada. Hiki ni kitu ambacho nimeona nikwambie na wewe rafiki yangu. Mara ukiwa na jambo, omba

  • Usifanye Kosa Hili Unapotaka Kufanya Uwekezaji

    Hongera sana Kwa siku hii ya kipekee rafiki yangu.
    Nadhani unajua ni Kwa Namba Gani nimekuwa nakusisitiza kufanya uwekezaji.

    Wakati mwingine unaweza kusikia watu wakiongelea Kuhusu uwekezaji ukaona nguvu hii iliyolala kwenye uwekezaji, basi ukaamua kwamba na wewe utaenda kuwekeza. Lakini sehemu yako ya kukimbilia ikawa ni kupata mkopo.

    Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia siku ya Leo ni kuwa usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza. Iwe ni Kwa ajili ya Kununua hisa, hatifungani au vipande.

    Badala ya wewe kukopa Kwa ajili ya hivi vitu, fanya hivi:
    Anza kuwekeza kidogokidogo
    Hata kama ni kiasi kidogo sana.
    Anza kufanya uwekezaji Sasa.
    Huu uwekezaji utakufaa sana Kwa siku zijazo.

    Unajua Kwa Nini nakwambia usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza?
    Nakwambia usikope Kwa ajili ya kwenda kuwekeza Kwa sababu mrejesho unaoupata kutoka kwenye uwekezaji wako, unaweza kuwa ni mdogo kuliko hata riba unayopata. Hivyo kitu hiki kikasababisha wewe ushindwe kulipa mkopo wako Kwa kutumia uwekezaji uliofanya. Badala yake ukalazimika kutumia vyanzo vingine kulipa mkopo.

    Hivyo basi, badala ya wewe kukopa. Kuwa tayari kuanza kuwekeza kidogokidogo. Wekeza hata kama siyo kiasi kikubwa. Nakuhakikishoa hiki kiasi baada ya muda kitakuwa kikubwa kuliko unavyofikiri.

    Muda pekee unapaswa kukopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji
    Kama kweli ukalazimika kukopa Kwa ajili ya kuwekeza. Basi muda pekee unapaswa kukopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji ni pale unapokuwa unakopa Kwa ajili ya kuendesha maisha.
    Kama unakopa Hela ya kula. Kitu ambacho haupaswi kuwa unafanya
    Kama unakopa Kwa ajili ya kuendesha maisha yako ya kila siku, basi hakikisha kwamba kwenye kukopa Kwako. Unakopa Kwa ajili ya kufanya uwekezaji pia. Kwenye kile kiasi ulichokopa, toa kiasi kidogo, Kisha kiwekeze.

    Kila la kheri.

  • Kazi Yako Ya Kwanza


    Rafiki yangu mpendwa salaam. Najua kuwa unapambana sana kwenye shughuli zako za kila siku. Hongera sana Kwa hilo.

    Siku ya Leo ningependa kukwambia kitu kimoja kikubwa sana. Kitu hiki ni kuwa kama unataka kufanikiwa kwenye maisha basi fahamu kuwa KAZI yako ya kwanza kabisa ni kuhakikisha haufi.
    Hakikisha unaendelea kuishi.

    Hilo, ukishalifanikisha kinachofuata ni wewe kuendelea kupambania ndoto na malengo yako makubwa. Kama kweli utayapambania Kwa ustadi wa hali ya juu. Ni wazi tu kuwa Kuna siku, lazima tu utafanikiwa.

    Kwa sababu kanuni ya asili ilivyo ni kuwa hakuna juhudi ambazo Huwa zinapotea Bure. Kwa hiyo, hiki unachofanta Sasa hivi na vingine ambavyo umewahi kufanya, vitaunganisha nguvu na kukuletea wewe mfanikio makubwa.

    Hivyo, hakikisha unaendelea kuishi
    Jilinde
    Ilinde afya yako
    Kisha pambania malengo yako

  • Kama kila mtu angekuwa ni…

    Hivi kaa chini ufikirie kama kila mtu angekuwa ni mzembe kama wewe.

    Kama kila mtu angekuwa na visingizio kama wewe

    Kama kila mtu angekuwa ni mwoga kama wewe

    Kama kila mtu angekuwa ni mlalamikaji kama wewe.

    Kama kila mtu angeona aibu kuitumia akili yake?

    Kama kila mtu angesema ni acha nile maisha leo kesho itajijua yenyewe

    Hivi unadhani nani angethubutu kufanya vitu vya tofauti. Ni nani angethubutu kutengeneza nguo unazovaa? Ni nani angethubutu kuanzisha biashara ambazo zinakusaidia wewe kuweza kufanya kazi zako.

    Bila shaka asingekuwepo. Kila unapoona kitu kizuri basi ujue kwamba kuna watu waeamua kuachana na uoga, ulalamikaji, uzembe, kutupia watu lawama na wamekuwa tayari kubeba majukumu ya maisha yao.

    Hivyo basi, kitu ambacho unapaswa kufanya kuanzia leo basi ni kuchukua hatua, kuacha kulalamika, uzembe, kutupia watu  lawama na uwe tayari kubeba majukumu yanayokuhusu.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Kuwa Imara

    Tunaishi katika dunia ambayo haipendi vitu ambavyo siyo imara. Na hili jambo la KUWA imara halijaanza leo. Limekuwepo kwa siku nyingi sana.

    Vitu ambavyo vimekuwa imara kwa miaka mingi ya nyuma, ndivyo ambavyo viliendelea kuishi, huku vile ambavyo siyo imara vikidhoofu na kufa.

    Watu wanyonge, mimea minyonge, wanyama wanyonge havina nafasi kubwa ya kuishi Kama vile vitu ambavyo ni imara. Hivyo, na wewe unapaswa KUWA imara.

    Najua hiki kitu kinaweza kuonekana cha ajabu sana hasa kwa upande wako ukizingatia kwamba umezoea kuambiwa KUWA wewe Ni MNYONGE. Na hivyo kuna watu wanakutetea wewe na unyonge wako.

    Ninachotaka kukwambia ni kuwa, usikubali kuwa MNYONGE. Unyonge ni hali ya chini ambayo MTU yeyote hapaswi kuibeba.
    Unapaswa KUBEBA ujasiri, uthubutu, na sifa nyingine za aina hii.

    Unyonge haukai meza moja na ujasiri. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na uthubutu. Unyonge hauwezi kukaa meza moja na utawala.
    Ukiwa MNYONGE unanyongwa na haki yako hupewi. Huo ndio ukweli.

    Hivyo, nataka ujiondoe kwenye hali ya unyonge kuanzia Leo hii na uanze kuwa jasiri, uwe imara.

    Kama kuna rafiki unayemfahamu anayepaswa kuwa imara mtumie ujumbe huu hapa kupitia hapa chini

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

  • Fanya hiki kitu unapokuwa na watu mara zote

    Utagundua kwamba wiki hii nimekuletea makala za namna ya kuhusiana na watu, kuanzia juzi, jana na hata leo. Lengo ni moja tu. Uweze kujifunza saikolojia ya binadamu kwa undani na ikusaidie kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi kuliko mtu mwingine ambaye amekuzunguka.

    Nakumbuka wakati nipo chuoni, nilipata kusoma kitabu cha Dale Carnergie kinachoitwa How to Win Friends And Influence People.

    Hiki ni kitabu, kama jina lake linavyosema, kipo hivyo hivyo kwelikweli. Nilikisoma kwa umakini mkubwa sana, nikatumia mbinu zilizokuwe kwenye hiki kitab. Muda si mrefu, nikaanza kuwa mtu mwenye ushawihi miongoni mwa watu niliokutana nao.

    Kwenye hili la kuwajali wengine kuna mengi ambayo unaweza kufanya.

    1. Unaweza kuwajali kwa kukumbuka majina yao
    2. Unaweza kuwajali wengine kwa kukumbuka tarehe zao za kuzaliwa
    3. Unaweza kuwajali na kufuatilia vitu wanavyopendelea
    4. Kuwasifia n.k.

    Rafiki yangu, kuanzia leo hii, hatakama ulikuwa hujali sana kuhusu maisha ya watu. anza kuonesha kwamba unawajali hao watu. Onesha hilo kwa vitendo, hata kama unaongea na hao watu kwa simu,

    Na ubora vitu unavyohitaji kuonesha kwa watu kuwa unawajali siyo vitu vya gharama. Ni vitu vya ambavyo unaweza kufanya tena bure kabisa.

    Kwa hiyo basi, kuanzia leo hii, jenga utaratibu wa kuonesha kuwa unajali wengine. Hiki kitu kitakuweka mbele kuliko watu wengine wote ambao umewahi kukutana nao kwenye maisha yako.

    Na kujali kunaanzia hapahapa. Kama umeipenda hii makala au ambazo umesoma siku za nyuma, washirikishe wengine unaowajali ili waisome. Watumie link hapa chini

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

  • Kosa kubwa unalofanya unapokuwa unaongea na watu

    Sasa tukiwa bado hapo kwenye kuongea na kuzungumza na watu, siku ya leo ningependa tu kukwambia makosa ambayo watu huwa wanafanya wakiwa na watu, na jinsi ya kuyaepuka haya makosa ili uweze kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi.

    Kosa la kwanza kabisa ambalo watu huwa wanafanya ni kutumia simu wanapokutana na watu. Rafiki yangu katika ulimwengu wa leo, simu ni dhana muhimu sana ambayo tunaitumia. Nadhani na wewe utakuwa unaitumia sana, sana simu. Pamoja na raha nyingi za kuwa na simu, pamoja na mambo mengi ambayo simu inaweza kutusaidia kufanya, kuna kitu kimoja ambacho naona bado watu hawajaweza kukitambua. Na kitu hiki ni kwamba unapokutana na mtu kwa ajili ya mazungumzo, tafadhali usitumie simu.

    Simu unayo muda wote. Yaani, wewe unashinda na simu na ulala nayo na pengine kitu uachoangalia kikiwa cha kwanza asubuhi ni simu.

    Sasa pamoja na kuwa unakuwa na muda mwingi wa kutumia simu kiasi hicho ni kuwa unapokutana na mtu bado unataka kutumia simu tu. hivi hili ni kweli? Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, watu wanapenda sana kuonekana wanathaminiwa, na njia ya watu kuonekana kwamba wanathaminiwa ni wewe kuwapa umakini wote pale unapokuwa unaongea hao watu. Hivyo basi, unapokutana na mtu yeyote, hakikisha kwamba hautumii simu.

    Weka umakini na nguvu zako zote kwenye mazungumzo yako na huyo mtu. Achana na vitu vyote au kitu kingine ambacho hakiendani na mazungumzo.

    Utakuwa na muda wa kutosha wa kutumia simu yako hapo baadaye, hivyo, kwa sasa achana kabisa na simu yako. Weka nguvu zako zote kwenye mazungumzo. Hiki kitu kitakusaidia kutogawa umakini wako. Hiki kitakusaidia kumsikiliza mtu kwa umakini. Hiki kitu kitakusaidia wewe kupata ushawishi zaidi wa watu.

    Inashangaza sana kuona kwamba watu wanaalikana ili wapige stori halafu badala ya kupiga stori, wanaanza kuongea na simu, wanaanza kuchati na kutuma jumbe.

    Ukiamua kwamba unaenda kukutana na mtu, usitumie simu.Na kama kutakuwa na ulazima wa wewe kutumia simu. Basi mwombe huyo mtu ambaye umekutana naye kwamba ungependa kuongea na mtu fulani mara moja au ungependa kumtumia mtu fulani ujumbe mara moja kisha unaendela na mazungumzo.

    Siyo unaongea na mtu halafu unatumia simu yako, hiyo ni dharau. Yaani, mtu ameacha majukumu yake yote, amekuja kukutana na wewe. Halafu, wewe unatumia simu muda wote. Huo ni ukosefu wa nidhamu aisee.

    Achana nao.

    Kosa la pili amablo watu wanafanya ni kutoangalia watu kwenye uso. Naam, unapooongea na watu unapaswa kuwaangalia watu kwenye uso. Hiki kitu kitaonesha kwamba uko makini kwenye mazungumzo ambayo yanaendela, lakini pia kitakusaidia wewe kuweza kumfuatilia mhusika kwa ukaribu na kuona namna anavyowasilisha mada kwako. Sambamba na hilo kumwangalia mtu usoni kunaonesha kwamba uko makini sana na unajali.

    Sasa kuanzia leo hii usiongee tu na watu. ukiongea na mtu yeyote yule hakikisha kwamba unaongea na ukiwa umemwangalia usoni. Mara zote, mwangalie huyo mtu usoni. Hiki kitu kitakupa maksi kubwa sana.

    Juzi juzi wakati napita mtandaoni nilikutana na nukuu ya

    Anasema kwamba kama unaangalia simu kuliko unavyoangalia watu usoni, jua kwamba kuna kitu kikubwa unakosea.

    Kumbuka hii ni nukuu ya mkurugenzi wa kampuni kubwa ya APPLE inayozalisha simu. Lakini bado anasisitiza wewe kuwaangaliwa watu usoni kuliko unavyoangalia simu yako. Na leo hii kwenye hii makala, bado naendelea kukusisitiza wewe kuendelea kuwaangalia watu usoni hasa pale unapokuwa unaongea nao.

    FANYA HIVYO MARA ZOTE,

    Kwa upande mwingine inawezekana hiki kitu hujakizoea. Kama hujazoea hiki kitu, kuna kitu kimoja tu unaweza kufanya kuanzia sasa hivi. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kuhakikisha kwamba unaanza kujenga utaratibu wa kuangaia watu usoni pale unapokuwa aunaongea nao. Fanya hivyo kuanzia siku ya leo.

    Nakutakia kila la kheri

  • Jinsi Ya Kupata Ushawishi Mkubwa Miongoni Mwa Watu

    Rafiki yangu mpendwa salaam,

    Umeshawahi kuona hili, unakutana na mtu, anakwambia au unamwambia kwamba nakukumbuka sura yako, ila sikumbuki jina lako. Sijawahi kukutana na mtu ambaye anakumbuka jina la mtu ila amesahau sura yake. Kwenye makala ya leo tunaenda kuangazia sula zima la MAJINA YA WATU. Tutaona njia rahisi utakayoitumia kupata majina ya watu, kukumbuka majina ya watu.

    Hivi umeshawahi kujiuliza ni kitu gani ukikifanya, kwa watu watu watapenda sana kuendelea kuwa karibu na wewe na watavutiwa kuonana na wewe mara kwa mara. Naam, kitu cha aina hiyo kipo.

    Kitu hiki ni kukumbuka majina ya watu. Hakuna mtu hata mmoja ambaye huwa anachukia kuitwa jina lake. Kila mmoja huwa anapenda sana kusikia akiitwa kwa jina lake.

    Hivyo kama kuna kitu cha maana sana ambacho unaweza kufanya, basi kitu hicho ni kuhakikisha kwamba mara zote unakumbuka majina ya watu. Majina ya watu ni silaha kubwa sana ambayo unapaswa kuitumia kwenye maisha yako.

    Nadhani imewahi kukutokea ukawa kwenye kusanyiko la watu na kukawa na mzungumzo ambayo yanaendelea. Mara ghafla ukasikia kwamba kuna kikundi cha watu wanataja jina lako. Linaweza kuwa ni eneo lenye kelele nyingi sana, ila kile kitendo cha wewe kusikia jina lako likitajwa na wale watu, kinakufanya  wewe uanze kufuatilia yale mazungumzo yao hata kama wale watu mwanzoni ulikuwa hufuatilii mazungumzo yao.

    Hiki ni kiashiria tosha kuonesha ni kwa namna gani huwa tunaweka nguvu kubwa kwenye kufuatilia majina yetu na kutaka kujau ni kwa na mna gani watu wanaongea juu yetu.

    Hivyo, basi kuanzia leo hii nakupa jukumu moja tu. Jukumu la kuhakikisha kwambna kila mtu ambaye wewe unakutana naye unakumbuka jina lake. na hili litawezekana kama utafuata mambo yafuatayo.

    Kwanza, kama utahakikisha kwamba kila mtu ambaye unakutana naye unamsikiliza vizuri pale anapokutajia jina lake. MARA NYINGI WATU huwa wanasahau majina ya watu, ila kitu kikubwa sana ambacho uwa kinawafanya hao watu wasahau majina ya watu ni kwa sababu huwa hawako makini kwenye kusikiliza hayo majina mara ya kwanza kabisa. unakuta kwamba mtu anataja jina lake lakini anayetajiwa jina hilo, hayuko makini kusikiliza.

    Sasa kama wewe unataka kuhakikish kwamba unakumbuka jina la kila metu  ambaye unakutana naye, kitu cha kwanza kabisa, ni kuhakikisha kwamba unamsikiliza kwa umakini mtu huyo anapokuwa anakutajia jina lake.

    Lakini siyo tu kumskiliza kwa umakini, baada ya huyo mtu kukutajia jina lake hakikisha kwamba unatumia jina la huyo mtu kwenye mazungumzo. Litumie mara kwa mara kwenye mazungumzo na kwenye maeneo ambapo unaona kwamba linafaa kutumiwa. Mtu asiishie tu kujitambulisha kwako, halafu wewe ukawa hujatumia jina lake kwenye maongezi naye.

    Pili, kama mtu amekutajia jina lake na wewe hujalisikia. Basi hakikisha kwamba unamwuliza vizuri ili arudie kukutajia jina lake kwa usahihi. Usiishie tu kusema kwamba ahaa, ok sawasawa.

    Tatu, mara zote hakikisha kwamba unajua namna jina la mtu linavyotamkwa na linavyoandikwa. Kuna mtu anaweza kukutajia jina lake ukawa unajiuliza hivi hili jina linaandikwaje, au linatamkwaje, kuwa makini kwenye hilo. Mara zote hakikisha kwamba unajua jina la mtu linavyoandikwa na linavyotamkwa pia.

    Lakini pia katika ulimwngu wa leo, unaweza kupata jina la mtu kupitia intaneti, bado ukiongea na huyo mtu utapaswa kumwuliza namna sahihi ya kutamka hilo jina ili huyo mtu aweze kujitambulisha kwako kwa usahihi na wewe uweze kutambua jina lake.

    Nne, kama mtu huyo anatambulishwa kwako na mtu mwingine, hakikisha aliyemtambulisha kwako amelitamka vizuri jina la mhusika na wewe umelisikia. Kama hilo jina hujalisikia vizuri, usikubali yapite. Maana mara nyingi watu huwa wanaona kama hawatakuja kuonana na mhusika ambaye wameongea naye, ila ukweli ni kuwa unapaswa kulikumbuka vizuri jina la mtu, hata kama unahisi huyo mtu hutaonana naye tena maishani mwako.

    Njia nzuri ya kupata majina ya watu

    Njia nzuri ya kupata majina ya watu ni wewe kujitambilisha kwa hao watu na kuwaambia kwamba wewe unaitwa…. Na kuwauliza wao wanaitwa akina nani? Hakikisha kwamba unajitambulisha kwa watu unaokutana nao punde baada ya kuwa umekutana nao.

    Ukiacha kujitambulisha kwa hao watu na ukaacha muda ukapita, nakuhakikishaia kwamba, baada ya muda  wa kukaa na huyo mtu, utajikuta kwamba umezoea kukaa naye ila humjuui jina lake, na itakuwa ni vigumu kwako kuweza kumuuliza tena, maana utaogopa kuonekana kama mtu ambaye hajali muda wote huo hujauliza jina lake na sasa hivi ndio unataka kuuliza jina lake.

    Kwa hiyo, unapouktana na mtu, jitambulishe, na muulize yeye jina lake.

    Kisha litumie hilo jina kwenye mazungumzo yako na yeye bila kurudi nyuma.

    Kwa mfano, mimi naitwa Godius Rweyongeza, na wewe ni……(EBU JAZA JINA LAKO KAMILI, BARUA PEPE NA NAMBA YAKO YA SIMU HAPO CHINI). Nitakupigia simu kukupongeza kwa kusoma makala hii.

    Sasa ukijua majina itakusaidia nini

    Kwanza itakusaidia kuteka umakini wa mtu. Ngoja nikupe mbinu ambayo utaitumia siku ya leo. Unapotaka hapa fanya kitu kimoja tu, nenda uulize jina la mtu ambaye hujawahi kukutana naye na wala hajui jina lako. Ukishajua jina lake, nenda uonane naye. Kisha ukionana na huyo mtu, mchangamkie. Mtaje jina lake kisha msalimie. Kwa kufanya kitu hicho kidogo tu, utaona ni kwa namna gani huyo mtu ataanza kukuuliza hivi jina langu umelifahamuje. Na utaona namna ambavyo huyu mtu atakuwa tayari kukusikiliza kwa umakini zaidi kwenye kile unachoongea.

    Ukijilijua jina la mtu na ukalitumia jina hilo kwenye mazungumzo, basi nakuhakikishia kuwa  huyo mtu utamvuta umakini wake. na hata kama huyo mtu alikuwa na mambo mengi ambayo anayafanyia kazi, nakuhakikishia kuwa huyo mtu ataacha kila kitu na kukusikiliza wewe kwanguvu zako zote.

    Pili, majina utayatumia kwenye mahusiano ya kawaida ya kila siku. Pata picha leo hii mtu amejitambulisha kwako, halafu kesho, ukakutana tena na huyo mtu. Ukamwita jina lake na ukaendelea kuongea naye kwa ustadi wa hali ya juu kuhusuaiana na kitu fulani. Ni wazi kuwa huyo mtu atapenda sana, kuwa karibu na wewe na hivyo, itakusaidia wewe kujenga mahusiano makubwa zaidi pamoja na yeye.

    Tatu, Kwenye biashara. Kama mfanyabiashara, unakutana na watu wengi, na kama mfanyabiashara unafanya kazi na watu wengi, ambao wanaweza kuwa ni wafanyakazi, wahisani, wapambe, wawekezaji, washirika n.k.. Rafiki yangu, unahitaji kuhakikisha kwamba unakumbuka majina yao.

    Tatu kwenye mauzo, utatumia majina ya watu kwenye mazungumzo na watu ili kuweza kuwauzia. Mara zote. unapokuwa unafanya mazungumzo ya mauzo hakikisha kwamba unatumia majina ya watu kwenye mazungumzo nao.

    Nne, kwenye kampeni. Kama wewe ni mwanasiasa na unataka kupata ushawishi mkubwa wa watu, basi kumbuka majina ya hao watu.

    Kwenye matangazo, ulimwengu wa sasa hivi umerahisha sana. Unaweza kufanya matangazo kwa njia mbalimbali, na kwa kutumia hizi njia unaweza kutumia majina ya watu na kuyataja. Mfano, utangazaji wa kutumia baruapepe…au kwa kutumia njia ya simu. Bado unaweza kutaja jina la mhusika na hivyo kuendelea kuvuta umakini wake kwenye kukusikiliza.

    Endapo utatumia vizuri hizi mbinu ambazo nimezianinisha hapa, ni wazi kuwa baada ya muda utakuwa superstar kwenye kukumbuka majina ya watu. Utaachana na dhana ya kwamba nakukumbuka  sura ila sikumbuki jina lako.

    Jina la mtu ni muhimu sana, ndio maana leo nimezama ndani zaidi kueleza hiki kitu.

    Unaweza kuwashirikisha wengine makala hii pia kwenye mitandao ya kijamii

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Sehemu Wanapokosea Wajasiriamali

    Watu wengi wamekuwa wakifahamu kuwa ujasiriamali ndiyo njia ya uhakika ya kutoboa na kufanya makubwa. Hata hivyo, wengi wamekuwa wanakosea kwa namna wanavyofanya ujasirimali na biashara zao kiasi kwamba, kutoboa kwao imekuwa ni ngumu sana.

    Kinachowakwamisha watu wengi ni kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Unakuta mtu ameanzisha biashara, wakati huohuo ana kitu kingine anachofanya sehemu nyingine. wakati huoho anapoteza muda mwingi sana kwenye mitandao. Biashara yake ikiwa bado haijatengamaa anasikia kwamba kuna fursa ya kuwekeza pesa zake sehemu akapata mara mbili ndani ya muda mfupi, anakimblia kuwekeza huko.
    Maabo yake yakiwa bado hayajakaa sawa anakimbilia kucheza vikoba ili siku moja aje apate mkopo.

    Na hapa ndipo wanapokosea wajasirimali wengi. Yaani, wanafanya vitu vingi sana, kwa wakati mmoja. ukifanya vitu vingi kwa wakati mmoja rafiki yangu, ni wazi kuwa huwezi kuona matokeo unayotegemea. Maana utakuwa unatawanya nguvu zako badala ya kuziweka sehemu moja. Nguvu zako ukiziweka sehemu moja, utapata matokeo makubwa kuliko ukitawanya nguvu zako kwenye maeneo mengi.

    Ni kama mwanga wa jua. Huu mwanga huwa una nguvu kubwa sana, ila huwa umetawanyika. ila ukikusanywa sehemu moja, huwa unawasha moto. sasa na wewe kama unataka kuwasha moto, kama unataka biashara yako iende kwenye ngazi za kimataifa, basi washa moto na weka nguvu zako sehemu moja. Sehemu ambapo utaweza kupata matokeo makubwa.

    Nakuhakikishia kuwa hiki ni kitu ambacho watu wengi hawapo tayari kukifanya, ukiweza kukifanya, kitakupa matokeo makubwa sana.
    Kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Njia Ya Uhakika Ya Kutoboa Kwenye Biashara

    Rafiki yangu, siku ya leo ningependa kukwambia njia ya uhakika ya wewe kutoboa kwenye biashara yako, unajua njia hii ni ipi?

    Ngoja kwanza nikwambie kitu. Tafiti nyingi kwenye biashara zimeonesha kwamba asilimia 90 ya biashara ambazo huwa zinaanzishwa kila mwaka, huwa zinakufa. hii ndio kusema kwamba kati ya biashara 100 ambazo huwa zinaanzishwa kila mwaka ni biashara kumi tu ambazo huwa zinauvuka mwaka wa kwanza.
    Na kati ya hizo biashara kumi ambazo huwa zinauvuka mwaka wa kwanza, bado ni biashara chache sana ambazo huwa zinaweza kuvuka mpaka kufikia miaka mitano.

    Hili wewe mwenyewe unaweza kulishuhudia kwenye maneneo yako unayoishi. Ni wazi kuwa kuna watu wengi ambao huwa wanajitahidi kila mwaka kuhakikisha kwabna wanaanzisha biashara mpya, ila ni wachache sana ambao huwa wanaweza kuendeleza biashara hizo kabla hawajafunga.

    Unadhani shida hapa ni nini?
    Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo watu wanaoanzisha bishara kila mwaka wanakosa. Ukiwa na hivi vitu, ni wazi kuwa utaweza kufanya makubwa, naam, utaweza kufanya makubwa sana.

    Kwanza unapaswa kufanya biashara ambayo unapenda. Haupaswi kufanya biashara au kitu ambacho hupendi. Kwa sababu unaenda kuwa unaamka kila siku kwenye hii biashara maisha yako au kwa miaka mingi ijayo. Sasa haifai hata kidogo kwako kufanya biashara ambayo wewe mwenyewe hupendi, au hujisikii kufanya.

    sasa kosa kubwa ambalo watu huwa wanafanya ni kufanya biashara kwa mkumbo. Kisa eti kasikia watu wanasema kwamba biashara fulani inalipa, basi na yeye anakimbilia kwenye kufanya biashara hiyo. Rafiki yangu, naomba unielewe kitu kimoja na cha uhakika. Fanya biashara unayopenda, tena biashara unayopenda kutoka moyoni, ila siyo biashara ambayo umesikia watu wanasema kwamba inalipa.
    Hii siyo ngoma ya kuingia ili ubahatishe tu. Unapaswa kuchagua kitu ambacho kuwa tayari kukifanya kwa muda mrefu

    Pili, unapaswa kufanya kwa muda mrefu. Siyo unaingia leo hii kwenye biashara halafu kesho unategemea kuwa umetoboa na kupata mafanikio makubwa. Kitu kama hiki hakipo rafiki yangu. inahitaji muda. ndio maana hata serikali huwa zinapewa muda. Unakuta kwamba muda wa uongozi wa serikali tangu wanapoingia madarakani mpaka uchaguzi mwingine unapofanyika ni miaka mitano. Hiki ni kipindi ambacho inatarajiwa kama jambo au mambo fulani yatafanyiwa kazi kwa mwendelezo kila siku na bila kuacha yatakuwa yameweza kuonesha matokeo.
    Lakini siyo suala la kulala leo na kuamka kesho.

    Sasa nikuulize wewe kitu chako umeshakifanya mfululizo, tena kila siku kwa miaka mitano mfululizo. Kama bado hujakifanya kwa miaka mitano ujue wazi kuwa bado unahitaji kuweka nguvu na juhudi kubwa kwenye kukifanya hiki kitu.

    Tatu, unapaswa kujituma kwenye kazi na kuwa tayari kufanya kazi kwa viwango vya juu kuliko watu wengine. Hiki ni kitu muhimu sana rafiki yangu, na hakikisha kwamba unakifuatilia kwa umakini mkubwa sana na bila ya kuchoka.

    Nne, jali afya yako. kwa kuwa hii ngoma siyo ya muda mfupi, basi hakikisha kwamba unajali afya yako. Yaani, hakikisha kwamba afya yako imekuwa ni kipaumbele chako nambari moja. Mara zote na siku zote, ipambanie afya yako. Hakikisha kwamba afya yako ndiyo kipaumbele chako nambari moja kila siku. Kula vizuri, pata muda wa kulala pia na fuata taratibu zote za kitalaamu kwenye afya. Hili jambo litakufanya uwe na afya njema, mara zote uwe kwenye mapambano.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

X