Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Asilimia 99 ya Maisha ya Watu Hujihusisha Na Vitu Hivi

    Leo nimekuandalia vitu ambavyo huwa vinachukua muda wa watu japo huwa havina manufaa yoyote kwao. Ni jukumu lako kuvifahamu na Kisha kuamua kuachana navyo.

    1. Watu wengi hupoteza muda mwingi wakihofu jinsi watu wengine wanavyowafikiria, wakati na wao wanahofu wanasemwaje.

    2. Watu wengi huishi maisha kwa kutaka kuwaridhisha wengine; wakati mtu pekee wanayepaswa kumridhisha ni wao wenyewe.

    3. Watu hutumia muda mwingi kwenye mahusiano yanayowaumiza wakitarajia  yatakuwa mazuri muda wowote.

    4. Watu wengi hutumia mida mwingi kuongea umbea na kuwasema watu. Ukweli ni kwamba mtu anayemsema mwingine mbele yako. Atakusema na wewe mbele ya wengine.

    5. Watu wengi hutumia muda mwingi wakijaribu kuishi aina fulani ya Maisha ili waendane na jamii husika. Kitu ambacho huwa kinawafanya wasiishi uwezo wao halisia.

    6. Watu wanatumia muda mwingi kufanya kazi ambayo hawaipendi. Wakishindwa kutoa hata dakika kidogo tu za kufanya kitu wanachopenda.

    7. Watu wengi wanatumia muda mwingi kutafuta fursa nzuri ya kufanyia kazi. Kitu ambacho huwa kinawafanya wakimbizane kutoka fursa moja kwenda nyingine.

    Pata nakala ya kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE Leo kwa elfu sita (6,000/-)

    Tuma sasa elfu 6 kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    KARIBU
    NI MIMI
    GODIUS RWEYONGEZA
    +255755848391
    MOROGORO-TZ

  • Hiki Ndicho Kitakachotokea Miaka Mitano Ijayo…

     Miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo ,isipokuwa kwa vitu viwili. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao. Watu unaokutana nao wana uwezo wa kukubadili na kukufanya mpya. Watakupa mtazamo wao, fikra zao, ujuzi n.k.

    Ukitaka kwenda MBALI ambatana na watu sahihi.

    Vitabu pia ni muhimu sana. Vitabu muda mwingine vinaweza kukukutanisha na watu sahihi. 

    Muda mwingine kama hupati watu sahihi, basi unapaswa kuvifanya vitabu kuwa rafiki yako wa kweli.

    Kwa kulifahamu hili, nimekuandalia kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZIBEBE ZIKUBEBE. Ili kiweze kuwa mwongozo kwako kwenye suala zima la fursa.

    Hakikisha unapata kitabu hiki cha kipekee, ambacho kinapatikana kwa bei nafuu tu  ya elfu sita (6,000)/-)

    Kupata nakala ya kitabu hiki lipia elfu sita kwa

    MPESA 0755848391

    Airtel money: 0684 408 755

     Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Ni mimi

    GODIUS RWEYONGEZA

    +255755848391

    MOROGORO-TZ

  • USIPOZIBEBA FURSA, HAZITAKUBEBA

     

    Moja ya shida ya watu ambao huwa wanashindwa kutumia fursa ni kujuta mbeleni.

    Ndio baadaye unakuja kusikia mtu anasema kuwa;
    👉 Mtu fulani tulisoma wote.
    👉Mtu fulani tulianza kazi kwa pamoja.
    👉Maeneo fulani viwanja vilikuwa   vinauzwa kwa bei ndogo ila sasa havishikiki.
    Ne  mengine mengi

    Hiki ni kiashiria kimojawapo kuwa mhusika hakutumia fursa zilizojitokeza maishani mwake vizuri. Usipozitumia fursa vizuri, ni ukweli kuwa haziwezi kukubeba.

    Pata kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE leo kwa elfu sita (6,000/-) tu leo.
    Nakala hii imesheheni mambo mengi mazuri kuhusu fursa.
    👉kimeeleza maana ya fursa: kwenye kitabu utakutana na zaidi ya maana kumi za fursa.
    👉 utajua jinsi ya kuziona fursa.
    👉 Utajua kwa nini watu hawazioni fursa hata japo mimi ninasema fursa zipo za kutosha
    👉 Tutajibu swali la kwa nini maisha ni magumu japo fursa zipo nyingi.
    👉 Tutaona maeneo zilipojificha fursa
    👉Tutaona fursa zilizohama kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Hizi ni fursa ambazo zilikuwepo miaka mingi sana iliyopita na bado zipo sasa hivi; yaani alizitumia babu yako mpaka wewe kitukuu
    👉  Tutaona jinsi ya kuhamisha fursa kutoka eneo moja kwenda jingine
    👉 Jinsi ya kugundua fursa mpya
    👉 Vigezo vya kuitambua fursa ya kweli na mengineyo mengi.

    Hakikisha unapata nakala yako leo kwa elfu sita (6,000/-) tu.  

    Lipia kwa:

    MPESA 0755848391

    Airtel money: 0684 408 755

     Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Ni mimi

    GODIUS RWEYONGEZA

    +255755848391

    MOROGORO-TZ

  • Kwa Nini Asilimia 1 Tu Ya Watu Duniani Ndio Hufanikiwa Sana

    Tafiti nyingi zimeonesha kuwa asilimia 1 ya watu duniani ndiyo wenye mafanikio makubwa kukiko wengine. Na hiki kitu kinaelekea kuwa kinafanya kazi kila sehemu.

    Asilimia 1 ya watu ndio wanaoohodhi mitandao tunayoitumia mara kwa mara. Ndiyo maana juzi anguko la mitandao ya facebook limeleta taharuki kubwa sana.

    Asilimia 1 ya watu ndio wanaomiliki mashamba makubwa na ndio wanaozalisha kwa wingi kuliko asilimia 99 iliyobaki.

    Na mwendelezo huu unaweza kuuona karibia kwenye kila sekta.

    Sasa kwa nini watu wachache tu ndio wanabarikiwa hivi?
    Kwa sababu maisha ni fursa. Wale wachache ambao wanakuwa tayari kubeba fursa hizi na kuzitumia ndio ambao wanabarikiwa zaidi, huku wale ambao hata hawana jicho la fursa wakiendelea kubaki vilevile. Na fursa ukizitumia lazima tu zitakubeba. Kitu hiki kinawafanya watu wachache sana kufanikiwa ukilinganisha na wengine.

    Hivyo, basi unapaswa kubadili mtazamo wako na kuanza kuangalia maisha kwa mtazamo wa kuziona fursa. Maisha Ni Fursa Zibebe.

    Kwa kuona hili, nimekuandalia kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA. ZITUMIE ZIKUBEBE , kwenye kitabu hiki nimekueleza kwa kina kila kitu Unachohitaji kujua kuhusu fursa. Ni kitabu ambacho nisingependa kuona unakikosa.
    Hakikisha unapata nakala yako leo.
    Kupata nakala yako, tuma elfu sita tu (6,000/-) kwa
    Airtel money: 0684 408 755 au

    Mpesa 0755848391

    kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Baada ya malipo utaniambia nikutumie kitabu.

    NB. Kitabu hiki ni soft copy.

    Changamka sasa upate nakala yako.

  • TUKUZE AKAUNTI AISEE

    !

    Siyo za insta wala facebuku!

    Ila za benki kuu,

    Na siyo kwa kuongeza wafuasi,

    Bali kwa kipato hata cha buku,

    Kitokanacho na kazi ya mikono yetu,

    Tuifanyayo mchana hata usiku,

    Tukuze kipato chetu.

    Kipato ni chanzo uhuru,

    Uhuru wa maisha mazuri,

    Na siyo  wa kujionesha bila senti,

    Kipato kitakusaidia mpaka wajukuu 

    Wao watafurahi hata kama siyo sikukuu

    Watafurahi kuwa ulikuwa mpambanaji mkuu

    Aliyewaachia urithi mkuu

    Tupambane!

    Weka moja ya kumi

    Ya kila upatayo makumi

    Iwe januari au  wa kumi

    Weka bila ya kukosa!

    Haiozi!

    Nikukumbushe tu kuwa kitabu cha MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE sasa kinapatikana tena kwa elfu sita (6,000/-)

    Tuma fedha sasa kukipata

    Tuma kwa mpesa 0755848391 au 

    Airtel money: 0684 408 755

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Godius Rweyongeza

    +255755848391

    Morogoro-Tz

  • MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie


    Hakuna fursa ambayo huwa inapotea. Usipotumia vizuri fursa inayokuja kwako, kuna mtu ambaye ataitumia. Asiyejulikana.

    Huwezi kuongelea ulimwengu wa kompyuta na mapinduzi ya kompyuta kiujumla bila kumwongelea Gary Kildall. Huyu jamaa ndiye alipaswa kuwa Bill Gates wa nyakati zetu ila akachezea fursa..endelea kusoma ili ujue kilichotokea.

    Mwaka 1977 kampuni ya apple ilitengeneza kompyuta yao ya kwanza iliyojulikan kama APPLE 1. Hapo ndipo vuguvugu la PERSONAL COMPUTERS lilipoanzia. Zilikuwa bado hazijawa za mpakato kama ilivyo sasa hivi, ila kampuni ya APPLE ilikuwa imeleta mapinduzi makubwa.

    Kampuni ya IBM kwa kuona kuwa wanaachwa nyuma, walitengeneza timu ya dharula ya kushughulika na hili na suala. Lengo la hii timu ilikuwa ni kutengeneza PERSONAL COMPUTER haraka iwekezakavyo kabla hawakapoteza fursa ya kuwa sehemu ya mabadiliko.

    Hiyo timu ilianza kazi na mwaka 1980 kazi upande wa HARDWARE ukawa umekamilika. Kilichobaki ulikuwa ni mfumo wa kuiendesha kompyuta (OPERATING SYSTEM) ambayo wataalamu wa IBM hawakuwa na uwezo nayo. 

    Kutokana na uharaka ilibidi wamtafute Bill Gates awasaidie. Walipoenda kwa Bill Gates aliwapokea na kuwaelekeza kuwa kampuni yake haikuwa na mwelekeo wa kutengeneza mfumo huo (operating system) kwa siku za karibuni. Hivyo, aliwaelekeza kwa rafiki yake ambaye alikuwa tayari ametengeneza mfumo huo ambaye sasa ndiye Gary Kildall.

    Gary Kindall alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kabisa kuona uwezekano wa kutengeneza kompyuta  binafsi (PERSONAL COMPUTERS), kiasi alishaanzisha kampuni inayotengeneza operating system iliyokuwa inaitwa Digital Research Inc. 

    Hivyo kumbe, Bill Gates alipowaelekeza watu wa IBM kwa huyu jamaa siyo kwamba alikuwa anatania, bali ulikuwa ukweli.

     Gary Kindall alipokea simu kutoka kwa Bill Gates ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanakuja, hivyo atapaswa kuongea nao vizuri. Ila hakuambiwa ni watu gani? Garry Kindall akawa amechukulia poa hilo suala na hivyo akapanda ndege yake binafsi kwenda kwenye mishemishe nyingine.

    Watu wa IBM walipofika hawakumkuta Gary Kindall, hivyo walilazimika kuongea na mke wake. Hata hivyo mazungumzo yao hayakwenda vizuri. Kitu kitu kikubwa kinachosemekana kilifanya mazungumzo yao yasiende sawa, maana mke wa Gary alishindwa kuchukua badhi ya maamuzi kutokana na mme wake kutokuwepo.

    Hivyo watu wa IBM waliondoka kwa hasira bila mafanikio yoyote. Ilibidi wamrudie Bill Gates kumwomba msaada. Bill Gates kuona hiyo nafasi imerudi kwake mara ya 2, ikabidi aitumie.

    Alichofanya alinunua kampuni ambayo kiuhalisia siyo kwamba ilikuwa imetengeneza operating system ya kwake, bali ilikuwa imeiga kutoka kwa akina Gary Kindall. Hivyo, alichofanya Bill Gates alichukua SOFTWARE hiyo, na kuwapa IBM. Huo ukawa mwanzo wa Bill Gates kuwa Bill Gates na Gary Kindall kupotea kwenye ramani….

    Umejifunza nini hapa?

    Hakikisha unapata kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    Lipia elfu 6 tu Leo uweze kupata kitabu. Ndiyo elfu sita (6,000). Changamka sasa

    Tuma fedha kwa 

    M-PESA 0755848391 au

    Airtel money: 0684 408 755

     jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Siku njema

    Godius Rweyongeza

    +255755848391

    Morogoro-Tz

    www.songambeleblog.blogspot.com

  • UCHAMBUZI WA KITABU CHA SUGU MAISHA NA MUZIKI. Mambo 14 niliyojifunza kwenye kitabu hiki kinachoeleza Maisha ya Sugu Kutoka Mtaani Mpaka Bungeni

    Mwishoni wa uchambuzi huu, nimeeleza jinsi unavyoweza kupata nakala ya kitabu hiki. Nipo tayari kukuchangia kiasi kidogo ili upate nakala ya kitabu hiki kizuri cha Kitanzania.

    Kwanza, karibu kwenye uchambuzi wa  cha SUGU. kitabu hiki kimeeleza maisha ya msanii Joseph Osmund Mbilinyi, maarufu kama Sugu. Ambaye ni mmoja kati ya wanahiphop wa kwanza hapa Tanzania, aliyeshiriki kikamilifu katika kuanzisha aina hii ya muziki na baadaye kuikuza. Sugu anasema yeye ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kwanza kabisa walioanza kuchana kwa lugha ya Kiswahili na pia kuichana serikali bila kificho.

    Anasema kabla yake waliokuwa wanaimba aina hii ya muziki walikuwepo; ila hawakuwa wakichana kwa lugha ya Kiswahili, badala yake  walitumia kiingereza na tena waliiga wasanii wa kizungu waliokuwa maarufu kwa wakati huo. Kuchana kwa Kiswahili   kulimfanya kuwa mtu wa tofauti na hata kupendwa zaidi.

    Leo tunaenda kuona sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kitabu hiki cha SUGU: THE AUTOBIOGRAPHY: MUZIKI NA MAISHA. From The Streets To Parliament.
    Pale ambapo nitatumia lugha ya kishikaji ambayo sijazoea kutumia kwenye blogu hii, nitaomba uivumilie maana mwandishi kaitumia hapa na pale kwenye kitabu. Sasa bila kupoteza muda haya hapa ndiyo mambo 14 niliyojifunza kwenye kitabu

    1. Sugu anasema siyo kwamba amefika hapo kwa bahati au upendeleo kama wengi wanavyofikiri badala yake anasema amesota sana mpaka kufikia hatua ya kuwa SUGU! Ukurasa wa 42 wa kitabu.

    2. Sugu anasema amepitia mengi ikiwa ni pamoja na kufanya uhuni akiwa Mbeya Day, sekondari ambayo alisoma. Kitu kilisababisha mpaka afukuzwe shule na baadaye kuhama shule hiyo. Baadaye akiwa kijana alijaribu kwenda Afrika Kusini kutafuta maisha kitu ambacho hakikufanikiwa na baadaye akiwa tayari amekuwa mwanamziki alienda Ulaya pia kujaribu maisha, ila bado hakuweza kutoboa.

    Kila mara alipoenda nje ya nchi alikuwa akikutana na changamoyo kama kufungwa kwa mipaka au kuumwa (home sick) kitu ambacho kilikuwa kinasababisha arudi nyumbani.

    Kwenye hili nimejifunza kuwa; zile hadithi za kuwa ukienda sehemu fulani utatoboa haraka, zinaweza kuwa zinavutia, ila ukienda eneo husika wanaposema kuna maisha mazuri, ndipo unauona ukweli wenyewe   Kumbe usidanganyike kwa kutaka kukimbilia sehemu fulani, kisa eti unasikia kuna maisha mazuri, kuna uwezekano ukaenda huko na usiyapate hayo maisha mazuri.

    3. Sugu anatuonesha nguvu ya watu waliokuzunguka wanavyoweza kukufanya uinuke au uanguke. Na hili utaliona wazi kwenye maisha yake kuanzia utotoni mpaka ukubwani. Ni marafiki zake wa sekondari waliomfanya awe mhuni.
    Ni rafiki yake ndiye alimfundisha kuandika mistari kwa  Kiswahili badala ya kiingereza.
    Ni rafiki zake pia waliokuwa wakimpa konekisheni na watu muhimu kwa wakati huo
    Na ni rafiki zake au watu waliokuwa wamemzunguka kwa wakati huo waliojenga njama za kumwangusha na hata kupelekea yeye kustaafu muziki bila kutaka.

    4. Kwenye kitabu hiki anaonesha pia jinsi wazazi walivyo na nafasi kubwa kwenye maisha ya watoto wao. Anamkubali sana baba yake kwa mengi aliyoyafanya na hasa kikubwa kutafuta maisha na kuitunza familia yao vizuri.

    Pia kwenye kitabu amemweleza mama yake kama mtu ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwenye uimbaji wake. Mama yake ndiye aliyemruhusu aingie kwenye gemu ya mziki. Hii ni kutokana na ukweli kuwa miaka hiyo, muziki ulikuwa unaonekana ni kitu cha hovyo. Wazazi hawakuruhusu watoto wao wawe wanamziki. Ila hali kwa mama yake Sugu ilukuwa tofauti. Alimruhusu.
    Pia mama yake ndiye aliyekuja kuwa mhimili mkubwa sana pale alipotaka kuacha mziki; mwishoni mwa miaka ya 90. Alimpa moyo kwa kusema aendelee.

    5. Sugu anasema alijenga historia ya kuwatoa wasanii wawili kwenye albamu yake ya milenia aliyoitoa mwaka 2000. Wasanii hao ni Afande Sele na Lady Jay Dee

    6. Sugu anaamini kuwa kusafiri kunakufanya ujifunze mambo mengi ambayo huwezi kujifunza kwa kukaa eneo moja. Na yeye anasema kwamba ameweza kujifunza mengi kwa kusaifiri nje ya nchi kukiko hata wasomi wanavyoweza kujifunza darasani.

    7. Sugu anasema kila mti wenye matunda huwa haukosi kupigwa mawe. Kwenye kitabu hiki anaeleza jinsi alivyopitia changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kutopewa mauzo sahihi ya albamu zake. Kuendeshwa kwa kampeni za wazi za kumwangusha na baadhi ya watu wakiwemo wamiliki wa redio ya Clouds, kitu ambacho anasema yeye alikipinga vikali.

    8. Muda mwingine ni muhimu kuonesha msimamo wako ili kujenga heshima yako na mazingira mazuri ya kikazi.

    9. Usilewe sifa. Ukipata sifa weka kazi zaidi kwenye kile unachofanya. Achana kujisikia kupita kiasi kitu ambacho kinaweza kupelekea upotee kimziki. Yeye anasema ni kitu hikihiki ambacho kimewapoteza wengi kwenye gemu.

    10. Ukipata kazi, basi ifanye kwa bidii. Hiki ni kitu ambacho Sugu anakieleza kwa kina kwenye kitabu hiki na anaonesha wazi kuwa kila kazi ambayo aliwahi kupata alikuwa akiifanya kwa moyo wake wote.
    Aliwahi kuajiriwa kama mlinzi, lakini kwenye kitabu anaonesha kuwa alikuwa akiifanya kazi hii kwa kujituma na kwa moyo wake wote. Aliwahi kuajiriwa Uingereza kama mtu wa kubeba mizigo kwenye kampuni, kazi anayosema ilikuwa ngumu ila aliifanya kwa kujituma japo alikuwa haipendi kivile.

    11. Sugu anaamini kuwa mtu mzuri wa kushirikisha naye ‘kimziki’ ni yule ambaye mna historia kubwa kutoka utotoni na siyo yule ambaye harakati za kikazi zimewafanya mkutane anasema hivyo baada ya vikundi vyote alivyokuwa akijiunga navyo kuishia njiani kwa baadhi ya watu kuacha muziki.  Mfano ni mshikaji wake BBG.

    12. Sugu pia kaonesha kuwa kitu unachopenda sana ndicho huwa kinakuumiza sana. Yeye anasema wazi kuwa  kuna vitu vitatu ambavyo alikuwa anavipenda Sana.
    Familia yake ya nyumbani
    Muziki na
    Mrembo mmoja aliyekuwa anaitwa Prude.
    Ila hivi viwili vya mwisho vilimuumiza mara kwa mara na hasa mwaka 2002 alipostaafu mziki kwa kulazimika kufanya hivyo na wakati huohuo akawa ameachana na mchumba wake.

    13. Sugu anatufundisha pia kutokuwa ving’anganizi wa maamuzi hata kama ni mabovu. Anaonesha hili kwa jinsi alvyoacha muziki na kwenda nje nchi. Ila akiwa huko alishauriwa kurudi kwenye gemu, kitu ambacho alikifanya kwa mara nyingine na aliporudi akawa ameweza kuendeleza harakati zake.

    Kumbe ukifanya maamuzi, na baadaye ikatokea unataka kubadili hayo maamuzi (baada ya kuwa umejua kuwa  kuna maamuzi mengine bora ya hayo). Unaruhusiwa kubadili mtazamo. Siyo dhambi. Ila kwa maoni yangu mchambuzi; Ni dhambi kunga’ngania kitu kile kile hata baada ya kugundua kuwa uamuzi huo haukuwa sahihi.

    14. Sugu anasisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kukuingizia fedha. Anaeleza jinsi ambavyo muda mwingine alikuwa akihangaika na hasa ilipokuwa inatokea anafuria.

    15. Ni muhimu sana kutafuta fedha na kuwa nazo. Bila ya kuwa na fedha utalazimika muda mwingine kufanya vitu hata kama vinakuumiza au vinaenda kinyume kabisa na misingi uliyojiwekea kimaisha. Mfano mzuri wa hili ni Sugu kukubali kurekodi albamu mojawapo na jamaa ambaye alikuwa akiuza kazi zake bila kumlipa vizuri.

    Alifanya  hivyo baada ya kuwa anahitaji sana fedha za kwenda nje ya nchi ila hakuwa nazo. Hivyo, alilazimishwa kurekodi albamu na jamaa ambaye alikuwa anajua wazi kuwa anamwibia maana hilo ni sharti alilowewekewa. Aliambia kama unataka fedha, niachie albamu ili nikupe fedha.

    Pia sugu kaeleza kisa kingine ambacho kilimfanya akiuke misingi yake, ila alilazimika kufanya hivyo, maana hakuwa na fedha. Ulikuwa uzinduzi wa albamu yake ya nne. Alilazimika kufanya kazi na watu wa Clouds, ambao yeye anasema kuwa hakuwa akiwapenda ila hakuwa na jinsi ambavyo angeweza kuzindua kazi yake bila wao. Hivyo, alilazimika kufanya hivyo, kitu kikichopelekea kulipwa kidogo sana na matarajio yake, na bado akasumbuliwabkwa kutolipwa fedha yake yote mpaka leo (leo hapo inamaanisha wakati anaandika kitabu; pengine sasa hivi watakuwa wameshamlipa)!

    Ok kitabu hiki ni kizuri na kina mengi ya kujifunza ndani yake. Kitabu hiki kina kurasa 147, ambazo ni hakika huwezi kuzizungumzia kiundani kwenye uchambuzi mfupi kama huu. Kama utapenda kukisoma kitabu hiki, Niko tayari kukuchangia kiasi kidogo ili upate nakala yako. Kitabu hiki kinauzwa elfu 20. Binafsi nitakuchangia 5,000/- na wewe utalipia 15,000/- ila gharama za usafiri zitakuwa juu yako. Nitafanya hivyo kwa watu watatu tu.

    Kwa hiyo basi kama utapenda kupata nakala yako kwa bei hiyo, tuwasiliane Sasa 0755848391.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Mitandao Mitano Ambayo Vijana wa Kitanzania Wanapenda Kutembelea Sana

     

    Siku ya leo nimeona nikuibie hili. Mtandao wa Alexa huwa una utaatibu wa kupangilia mitandao yote kutokana na wingi wa watembeleaji kutoka kwenye kila nchi.
    Kwa kutumia mtandao huu unaweza kujua nchi ipi, watu wake wanapendelea kutembelea mtando  upi.

    Na leo tunaenda kuona mitandao ambayo Watanzania wanapenda kutembelea sana. Hii ni muhimu kwako kuifahamu kwa sababu inaweza kukusaidia kufanya mengi.
    Moja; inaweza kukusaidia kujua wapi watu wanatumia muda wao kwa wingi, na hivyo kuweza kutumia jukwaa hilo vizuri. Pia, inasaidia kama unataka kufanya Ia matangazo, kujua wapi watu walipo ili utangazie huko.

    Kitu kimoja cha uhakika ni kuwa mitandao ambayo Watanzania wanapenda kutembelea itakushangaza. Ni tofauti na vile ambavyo wewe mwenyewe ulikuwa unategemea. Najua  wengi wanaweza kudhani labda WhatsApp ndio mtandao nambari moja unaopendwa kutembelewa. Ukweli ni kuwa  WhatsApp siyo mtandao nambari moja au mbili. Ifuatavyo sasa ni mitandao mitano ambayo vijana wa kitanzania wanapenda kutembelea:

    1. Google
    2. YouTube
    3. Facebook
    4. Yahoo
    5. Wikipedia

    Mitandao miwili ya ziada ambayo Watanzania wanapenda kutembelea ni
    6. Jamii Forums na
    7. Instagram

    Hiyo ndiyo mitandao inayotembelewa sana hapa Tanzania. Ni muhimu sana kwako kuifahamu kwa sababu Kuna fursa ndani yake. Unaweza kujua muda mwingine ukitaka kufanya kampeni fulani, utumie mtandao gani kufanikisha hiyo kampeni.

    Kwa sababu watu wake wako huku.

    Nimeandika kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA;  ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki ninaenda kukizindua rasmi tarehe 1.10.2021.

    Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na kwa atayaweka oda; 

    Kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo. 

    Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.

    Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa  vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.

    Vitabu utatavyopewa kwa sasa ni 

    1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

    2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA

    3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

    Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.

    Namba ya malipo ni 

    MPESA 0755848391

    Airtel money: 0684 408 755

     Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.

    .

    Vitabu vyote ni soft copy.

    Ni mimi

    GODIUS RWEYONGEZA

    0755848391

    MOROGORO-TZ

  • ZEGE HALILALI

    Wajenzi wanalifahamu hili. Zege ikichanganywa, kwa vyovyote vile hata iweje, inapaswa kuisha, la sivyo ikilala, asubuhi, hutaikuta kama zege, badala yake itakuwa imekauka.

    Itakuwa siyo zege tena…
    Itakuwa haifai tena kwa ajili ya ujenzi.
    Ndio maana huwa wanaenda kwa kanuni ya zege HALILALI.

    Na wewe unaweza kujiwekea utaratibu kama huu. Kuna vitu katika maisha yako unapaswa kuvifanya kuwa kama zege. Na havipaswi kulala hata kidogo. Vifanye siku hiyohiyo na uvikamilishe.
    Kama kuna majukumu ya kuandika, hata kama ni maneno kidogo, hakikisha unayaandika kila siku bila kulaza kiporo. Maana zege halilali.
    Kama unapaswa kufanya mazoezi yafanye maana zege HALILALI.
    Kama unapaswa kuweka akiba leo, usiseme kwa kuwa kesho nitapokea fedha nyingine ngoja ya leo niitumie nitakuja kuweka akiba ya kesho au kesho kutwa. Kumbuka fedha ya leo inapaswa kuwekewa akiba yake na kesho inapaswa kuwekewa akiba yake pia.

    Kwako fanya vitu kama hivyo kuwa mwiko. Vifanye kuwa kama zege, maana ZEGE HALIPASWI KULALA.

    Ni kitu gani unaenda kukifanya kuwa kama zege leo?
    *******************************************************

    Nimeandika kitabu kinachoitwa MAISHA NI FURSA;  ZITUMIE ZIKUBEBE. Kitabu hiki ninaenda kukizindua rasmi tarehe 1.10.2021.

    Ila habari njema ni kuwa leo hii unaweza kuweka oda ya kupata kitabu hiki. Na kwa atayaweka oda;
    Kwanza atapata kitabu kwa bei ya punguzo.
    Pili, nitampa vitabu vingine vya ziada kama zawadi; tena hivyo vitabu vingine vya zawadi nitavituma leo hii baada ya mtu huyo kuweka oda.

    Kuweka oda utalipia, elfu kumi tu (10,000/-) tu. Ila kwa kuwa utalipia elfu kumi leo hii, utpewa  vitabu vingine vitatu wakati ukiendelea kukisubiri kitabu cha maisha ni fursa, ZITUMIE ZIKUBEBE.
    Vitabu utatavyopewa kwa sasa ni
    1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
    2. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA
    3. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

    Rusha elfu kumi leo kwa namba 0755848391. Upate vitabu hivyo vitatu, na kitabu cha MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE kitatumwa kwako tarehe 1.10.2021 bila wewe kuhitajika kuongeza senti ya ziada.

    Namba ya malipo ni

    MPESA 0755848391
    Airtel money: 0684 408 755
    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    NAKUKUMBUSHA TU: Ukituma elfu kumi leo. Taarifa zako zitatunzwa vizuri, na tarehe 1.10.2021 utatumiwa kitabu cha MAISHA NI FURSA; ZITUMIE ZIKUBEBE bila kuongeza senti ya ziada, wala bila kutukumbusha tukutumie.

    Karibu.
    Godius Rweyongeza
    +255755848391
    Morogoro-Tz

  • Karibu kwenye darasa la mwisho la kuandika kitabu kwa mwaka 2021

    Njoo ujifunze kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu

    Kwa mara nyingine tena, napenda kukutangazia kuwa dirisha la kujiunga na darasa la uandishi limefunguliwa. Ila zamu hii litakuwa darasa la mwisho kwa mwaka 2021.

    Kama una mpango wa kuandika kitabu kabla mwaka haujaisha, Basi jiunge na darasa hili.

    Nani anahitajika kwenye darasa?

    Mtu yeyote mwenye nia ya kuandika kitabu na kujifunza mambo yote yanayoendana na uandishi.

    Darasa litaanza lini na litafanyikia wapi?
    Darasa letu huwa linafanyikia WhatsApp na sasa hivi tumeongeza kipengele cha kujifunza kupitia telegram pia.

    Kwa darasa hili ambalo ni la mwisho kwa mwaka huu, tunategemea litaanza kati ya tarehe 15-20 mwezi 10. Wanadarasa tukishatimia tutapanga tarehe rasmi ya kuanza kati ya hizo, ila itakuwa kati ya 15-20 oktoba.

    Wanahitajika watu wangapi darasani?
    Wanahitajika watu watano tu. Darasa likijaa limejaa, kutakuwa hakuna nafasi ya ziada.

    Kuna gharama yoyote ya kuhudhuria darasa hili?
    Ndiyo. Kwa kawaida darasa hili huwa linalipiwa elfu sabini (70,000). Ila zamu hii wahudhuriaji wote wanapewa ofa ya kuhudhuria darasa hili kwa elfu hamsini tu (50,000/-)

    Mfumo tunaoutumia ni wa first come, first served

    Karibu ujihakikishie nafasi kwa kulipia kupitia 0755848391.

X