Category: Uncategorized

  • Kuna fedha naisubiri…

      Imekuwa inatokea mara kwa mara watu wanaahidiwa fedha na kuanza kuweka mipango kamambe juu ya hiyo fedha.  Hata hivyo huwa kuna mawili kwenye fedha ya kuahidiwa. Inaweza kutumwa kweli. Au isitumwe kabisa kitu ambacho kitakukwamisha au la utaendelea kusema, Kuna fedha naisubiri. Unaweza kupanga kufanya mipango mingi kiasi kwamba fedha hiyo inapokuja, unashindwa kufanya…

  • Inawezekana kuondokana na madeni

    Madeni ni moja ya kitu ambacho kinawasumbua watu wengi na hivyo kuwafanya washindwe kuwa na uhuru lakini hapohapo kuwanyima mwanya wa kuufikia uhuru wa kifedha. Sasa ukweli ni kwamba, inawezekana wewe hapo kuufikia uhuru wa kifedha na kuondokana na madeni. Vifuatavyo ni vitu muhimu vya kufanya ili uweze kuondokana na madeni. Kwanza orodhesha madeni yako…

  • INAWEZEKANA

     Inawezekana wewe kufikia kiwango cha mafanikio unachotaka. Inawezekana wewe kuishi bila madeni.  Inawezekana wewe kuifikia ndoto yako kubwa. Inawezekana wewe kuufikia uhuru wa kifedha. Kiufupi hakuna kitu ambacho Kama utaamua kufanya kitashindikana. Ila itapaswa kuweka malengo ya kufikia kitu hicho. Kisha kuanza kuyafanyia kazi hatua kwa hatua. Ebu Sasa niambie ni kitu gani ambacho wewe …

  • UKISIMAMA MBELE YA MUNGU

    Umepewa kipaji hivyo unapaswa kukitumia vizuri kiasi kwamba siku ukifa ukaenda mbele ya Mungu usiwe umeacha hata tone la kipaji chako ambacho hakijatumika. Kiasi kwamba uwe na ujasiri wa kumwambia Mungu kuwa ulichonipa chote nimekitumia.

  • Jinsi Ya Kudandia Teknolojia Mpya

    Tunaishi katika dunia ambapo teknolojia mpya inazidi kubadilika kila siku. Sasa mabadiliko haya ya kiteknolojia hayapaswi kukuacha nyuma muda wote. Kuna namna ambayo unapaswa kuitumia ili uweze kuendana na mabadiliko haya. Ebu fikiria kwa mfano Sasa hivi, uwepo wa maroboti umeanza kuwafanya watu wakose kazi hata wale ambao ziku zote walikuwa na kazi ambazo ziliaminika…

  • JITUME KWA FAIDA YAKO

      Katika kazi yoyote ile unayofanya jenga utaratibu wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Hata kama kazi hiyo siyo yako. Unapojituma humnufaishi mtu yeyote, unakuwa unajinufaisha mwenyewe. Hata kama kazi umelipwa fanya zaidi ya vile unavyolipwa. Usiangalie manufaa ya muda mfupi badala yake angalia manufaa ya muda mrefu. Hivyo jitume zaidi kwa manufaa yako.…

  • Jifunze Kitu Kwa Kila Mtu

    Usiwachukulie poa watu ambao unakutana nao leo. Kila mtu ana funzo kubwa ambalo unaweza kulipata haijalishi mtu huyo amefanikiwa au hajafanikiwa. Bado kuna kitu kikubwa cha kujifunza kwake.  Kama amefanikiwa hapo ndio unahitaji kujifunza mbinu alizotumia yeye mpaka kufanikiwa. Zitumie mbinu hizo kwa manufaa yako pia.  Kama hajafanikiwa ila anapambana kuelekea ndoto yake, bado unaweza…

  • Hii Hapa Ndiyo Sababu Kuu Inayopaswa Kukusukuma Wewe Kutimiza Ndoto Yako

        pata nakala ngumu kwa kuwasiliana na 0755848391 Umewahi kujiuliza ni kwa nini unapaswa kutimiza ndoto za maisha yako? Kwa nini?Kwenye kitabu changu cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako (ukurasa wa 36-38) nimeeleza sababu kumi za kwa nini unapaswa kufanyia kazi ndoto zako. Siku ya leo ninaenda kukupa sababu moja ya ziada na hivyo…

  • Ifuatayo ni orodha kamili ya vitabu vyangu vyote

     Ifuatayo ni orodha kamili ya vitabu vyangu vyote. Ni kitabu gani ambacho hujasoma? Chagua kimoja ukipate kwa punguzo la asilimia 20 leo ikiwa ni siku valentine.  Hivi vya kwanza ni hardcopy๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ 1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO (20,000). (Hardcopy) 2. Kutoka sifuri MPAKA KILELENI (10,000) (hardcopy)  Hivi vingine Ni soft copy๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ 3. Nyuma ya ushindi…

  • Wiki hii kwa ufupi: Masomo Sita Yaliyotikisa Wiki Hii

      Juma la saba la mwaka 2021 limeshafika ukingoni. Ule mwaka uliokuwa unaonekana mpya sasa umeshaanza kuota mvi za uzee. Sio mpya tena. Wengi walioweka malengo  wameshayasahau na wengine hawajachukua hata hatua moja kufanya kitu KUELEKEA hayo malengo yao. Hili siyo mimi tu ninayelisema, bali tafiti za kitaalamu pia zinaonesha hivyo. Tafiti zinaonesha asilimia kubwa…

  • vitu vitano vinavyowatofautisha watu wanaofikia malengo yao na wale ambao wanashindwa

     Kitu kimoja kikubwa kuhusu wanaotimiza malengo siyo kwamba wana akili sana, au kwamba wamebarikiwa na Mungu kuliko wewe. Hapana. ila kitu ambacho kinawatofautisha na kitaendelea kuwatofautisha kwa siku nyingi ni kwamba. 1. wanaweka lengo wanalifanyia kazi mpaka linatimia. wanafanya hivi bila kujali wanapitia katika hali gani. bila kujali wamekutana na vikwazo gani. wao wanachojua ni…

  • Mwalimu Mazumila Asema Kitabu Cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako Kimegeuka Kuwa Baraka Kwake

    JINSI Ya Kufikia Ndoto Zako ni kitabu kimoja ambacho kimeendelea kuwa msaada mkubwa kwa watu. Mpaka sasa asilimia kubwa ya watu waliokosoma kitabu hiki mwaka 2020 wanasema kimekuwa ni kitabu bora Sana. Mmoja watu hao ni Edius Katamugora ambaye unaweza kusoma maoni yake kuhusu kitabu hiki HAPA. Mwalimu Mazumila naye amekisoma na haya hapa ndiyo…

  • Hivi ndivyo unaweza kuonesha kuwa una upendo kwa watu

        Ni njia gani unaweza kutumia kuonesha kwamba una upendo? Hivi umewahi kufikiria kuhusu hili? Siku ya leo nimeona nikuoneshe njia ya kawaida ambayo unaweza kutumia kuonesha upendo kwa watu. na njia hii ni kuwasaidia watu  kufanya kitu fulani au kutimiza kitu fulani. Inaweza pia kuwa ni kuwasaidia watu kutatua tatizo fulani au hata…

  • KAMA UNATAKA KUFANIKIWA, KUBALI KULIPA GHARAMA

     Wahenga wanasema kuwa mtaka cha uvunguni sharti ainame. Hii ndiyo kusema kuwa kama wewe unataka kupata kitu chochote kizuri, Ni sharti uwe tayari kulipa gharama ili kupata kitu hicho. Vitu vizuri vinahitaji uvigharamikie kuvipata. Ukiwekwepa kutoa gharama inayopelekea kupata vitu vizuri, utaishia kupata vitu feki. Sasa kwa kwa nini usilipe gharama?  Je, gharama zenyewe unazopaswa…

  • UKITAKA KUFANIKIWA UZA KWANZA VYOTE ULIVYONAVYO…

      NB: Usiishie tu kusoma kichwa cha makala bila kusoma makala yenyewe Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze vyote ULIVYONAVYO, kisha njoo unifuate -Biblia. Kwenye Biblia kuna usemi huo wa kishujaa, ukieleza sifa moja muhimu ya kumfuata Yesu. Siku ya leo siyo kwamba ninataka nikuhubirie, hapana. Na wala siyo kwamba nitapenda ukauze ulivyonavyo ili Ufanikiwe, maana…

  • Kitu Muhimu Kuhusu Fursa

     Watu wengi wamekuwa wanapenda kuongelea fursa. ila wanasahau kuwa kitu kikubwa kuhusu #fursa siyo kuziongelea tu. badala yake kitu muhimu kuhusu fursa ni kuhakikisha kwamba unazichangamkia. hapa ndipo watu wengi wanafeli na hivyo kuendelea kupitwa na fursa zile zile ambazo wao wanaongelea kila siku kwenye vijiwe mitaani au kwenye mitandao ya kijamii. sasa ninachopenda wewe…

  • Mambo Saba Ya Kufanya Ili Mwaka Wako Uende Sawasawa

      Mwaka 2021 unapaswa kuwa mwaka wako ambao utafanya vitu vya kipekee. Yafuatayo ni mambo kumi ya kufanya ili mwaka wako uweze kuwa wa kipekee. 1. Usiongee sana tenda Sana. 2. Usiingie Sana kwenye mitandao ya kijamii 3. Hakikisha unapata muda wa kutafakari kila siku 3. Panga siku yako unapoamka 4. Kila siku jioni jiulize…

  • KAMA HAWAHESHIMU MUDA WAKO, HAWAKUHESHIMU

        Najua. Ndiyo najua. Kuna siku umewahi kupanga kukutana na mtu fulani sehemu ambayo unaifahamu wewe na ukawa umejiandaa siku nzima kwa ajili ya hilo tukio halafu mtu huyo akawa amekwambia dakika za mwisho kuwa hatakuja au la hakuonekana kabisa na hakukuwa na taarifa yoyote ile aliyokupa. Pengine wewe mwenyewe umekuwa ukiwafanyia watu wengine…

  • Jinsi Ya Kuanza Uwekezaji Mkubwa Kwa Fedha Kidogo

     Kuna siku hapo nyuma nilikuwa nafahamu kuwa ili uitwe mwekezaji basi unapaswa kuwa mtu kigeni au mtu kutoka nchi za ulaya, bara la asia na maeneo mengineyo ila siyo hapa nchini Tanzania. Hata hivyo kadiri siku zilizvyoendelea nilikuja kugundua kuwa huhitaji kuwa umetoka nchi za nje ili uweze kuwa mwekezaji, uwekezaji unaweza kuufanya popote pale…

  • FANYA KAZI KWA BIDII

     Inawezekana Kuna watu wenye kipaji kizuri kuliko wewe, hilo lipo nje ya uwezo wako. Hata hivyo hakuna mtu ambaye anapaswa kufanya kazi kwa bidii na kukuzidi (kufanya kazi kwa bidii kupo ndani ya uwezo wako) Kufanya kazi kwa bidii kutakutoa hata kama  huna kipaji kikubwa. Fanya kazi kwa bidii. SOMA ZAIDI: ACHA UTAPELI WEWE? Hivi Ndivyo…

X