-
Sifa Moja Kuu Ya Watu Wanaofanya Vitu Visivyo Vya Kawaida

Wanaofanya vitu visivyo vya kawaida siyo kwamba wao wameshuka kutoka mbinguni au wana upekee ambao wewe huna.
Ni watu tu kama wewe ambao wamejitoa kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanafika mbali. Na huo ndio mwanzo wao wa kufanya vitu visivyo vya kawaida
Godius Rweyongeza
-
Unawezaje Kupata Wazo La Biashara La Kipekee?
Kwenye makala iliyopita nilikwambia kwamba huwezi kupata wazo la kipakee la biashara. Ni vigumu kupata wazo ambalo halijawahi kufanyika kabisa.
Unachohitaji sana wewe, siyo wazo la kipekee ambalo halijawahi kufanyika. Unachihitaji ni kUchagua kitu kimoja na kuhakikisha kwamba unashughulika na hicho.
Angalia jamii yako ina tatizo gani kisha tatua hilo tatizo. Ebu fikiria kuhusu sehemu unapopata huduma mtaani kwako. ebu fikiria juu ya supermarket yoyote mjini kwako. au fikiria kuhusu basi ambalo huwa unatumia kusafiri, hawa jamaa hawa hawakuwa wa kwanza kuingia kwenye soko.
Kitu kikubwa ni kwamba walifanya uamuzi wa kwamba tunaenda kuzalisha bidhaa na kutatua tatizo ambalo linawakumba watu. Basi. Hawakuwa wagunduzi wa hicho kitu, hawakuwa waanzilishi wala wa kwanza kufanya hicho kitu.
Ebu kwa mfano fikiria kampuni inayotengeneza redio. Haikugundua hiyo redio. Na walikuwa wanajua kwamba kuna redio nyingine huko mitaani zinauzwa. Hawakukaa na kuanza kufikiri juu ya wazo gani jipya na la kipekee waje nalo.
Kitu pekee walichokuwa na uhakika nacho ni kwamba, kila mtu anahitaji redio na watu wananunua redio mara zore. Hivyo, ngoja na sisi tutengeneze moja na kuiuza.
Hivyo, huhitaji kuwa wa kwanza kwenye soko. Wanunuaji wanapoenda kununua hawanunui kwa sababu mtu au kampuni ili kuwa ya kwanza kutengeneza bidhaa husika.
Bali wenyewe wananunua kwa sababu,
- Wana tatizo na
- Wameona bidhaa ambayo inatatua tatizo lao
Hivyo. Badala ya wewe kuanzakufuta wazo ambalo halijawahi kufanyika hapa duniani, fanya hivi:
- Angalia tatizo walilonalo watu
- Tengeneza bidhaa inayoweza kutatua hilo tatizo lao
- Ilete mbele ya wahusika.
Acha kulisubiria wazo la kipekee. Ukisubiria wazo la aina hii, utakufa ukiwa bado unasubiri.
Kila la kheri
Godius Rweyongeza
0755848391
SOMA ZAIDI
-
E-BOOK MPYA: KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

Najua umekuwa unajiuliza, hivi mimi nimezaliwa na kipaji? Kipaji changu Ni kipi?
Nawezaje Kukigundua?Nakiendelezaje na kinawezaje kuninufaisha?
Kwa majibu ya maswali yote hayo na zaidi, karibu usome ebook ya kipaji ni dhahabu. Ebook hii ya kipekee sana imejaa mambo mengi muhimu kuhusu kipaji, unavyoweza kukinoa, kukiendeleza mpaka kikakufikisha mbali.
E-book hii ya kipekee itakusaidia wewe kugundua kipaji chako na kukitumia kwa manufaa.
Kuona yaliyomo na kusoma utangulizi BONYEZA HAPA
E-book hii unaweza kuipata sasa kwa elfu 5 tu. Tuma fedha kwa 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Baada ya hapo utaniambia nikutumie e-book hii.
SOMA ZAIDI:Kipaji Ni Dhahabu: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa
/
KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa
-
Ungekuwa wewe umewekeza kwenye hii kampuni ungefanyaje?
Brown Unaendeleaje? Bila shaka umeamka salama kabisa.
Leo ninataka niongee na wewe kuhusu uwekezaji.
Kwanza ebu niambie mimi, Ni kampuni gani unaikubali hapa Tanzania? Ni kampuni gani ambayo kwa vyovyote vile unapenda huduma zake na kamwe huchoki kwenda kwao. Ebu niambie ni ipi hiyo?
Inaweza hata isiwe kampuni kubwa, ikawa biashara yoyote ya kawaida tu, pengine hata mtaani kwako, ila wewe binafsi unaikubali. Kila mara lazima uende kwao kupata huduma zao.
Sasa ebu fikiria kwa jinsi ambavyo wewe unaikubali hiyo kampuni, biashara au taasisi hiyo, ungekuwa wewe ndiye mmiliki au mmoja wa watu wenye maamuzi makubwa kwenye hiyo kampuni ni kitu gani cha ziada ungefanya kuhakikisha kwamba kampuni yako inazidi kusongambele?
Ebu andika jibu lako chini. Ujue jibu lolote utakalopata litakusaidia wewe pia.
Nataka jibu lolote utakalopata uende na wewe ullitumie kwenye biashara au kipaji chako.
Kama umeona hicho kitu ndicho kinaweza kuifanya biashara unayoikubali bora zaidi, na wewe ukikitumia ni wazi kuwa kitaboresha biashara yako pia. Kwa hiyo kakitumie wewe KWENYE kampuni au biashara yako.
Pia tumia mbinu nyingine ambazo unaziona kwa hiyohiyo kampuni unayoikubali. Angalia mbinu ambazo wanatumia kuhudumia wateja, kuwasiliana nao n.k.
ZITUMIE kuboresha biashara yako na kuifanya kuwa Bora zaidi.
Kama unaikubali biashara hiyo kwa sababu ya huduma nzuri. Na wewe Anza kutoa huduma nzuri Kama wao wanavyofanya. Iga kwao. Inashangaza kuona kwamba watu huoenda kuiga vibaya na kuacha sifa nzuri kama hizi. Sasa ebu wewe ziige hizi sifa.
Muda siyo mrefu utaweza kuifikisha mbali sana hiyo biashara yako.
Kama unaikubali biashara au kampuni hiyo kwa sababu ya bidhaa Bora, ebu na wewe anza kuzalisha bidhaa Bora.
Kwa vyovyote vile. Endelea kusonga mbele. Utaweza kufanya makubwa zaidi pale utakapokuwa na mtu unayemwangalia na kujifunza masomo kwake. Ukajifunza na kufanyia kazi unachojifunza.
Kila la kheri.
Godius Rweyongeza
Morogoro-Tz
0755848391
https://songambele.co.tz -
KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa
Nakumbuka mwaka 2013 nilikutana na vijana wenzangu ambao walikuwa kwenye mjadala mkali kuhusiana na Messi, Ronaldo na Neymar. Kwenye mjadala huu walikuwa wakijadili kuhusiana na uwezo wa wachezaji hawa, huku wengine wakisema kwamba Messi na Neymar wana kipaji ila Ronaldo akiwa anatumia nguvu.
Nadhani kama wewe ni mpenzi wa soka, mijadala kama hii utakuwa unaifahamu ambavyo huwa inatokea sana. Na jinsi ambavyo huwa inateka umakini wa watu.
Kwenye mijadala kama hii watu huwa wanatoa hoja zao kwa nguvu kuonesha kwamba mchezaji fulani ni mzuri na ana kipaji kuliko mwingine.
Mijadala mingine ya aina hii huwa ni mijadala ya wasanii, ambapo huwa wanalinganishwa wasanii wawili. Umewahi kushiriki mjadala kama huo?
Hivi kwanza wewe mwenyewe unakijua kipaji chako?
Mjadala kama huu ndio ulinifanya nitafakari na kujiuliza hivi mimi mwenyewe nina kipaji gani? Je, hawa wanaozungumzia kipaji cha Messi, Neymar na Ronaldo wanajua vipaji vyao? Ukiwauliza wewe una kipaji gani wanaweza kukujibu? Na tokea hapo nikaianza safari ya kujitafuta ili niweze kujua kipaji changu. Maswali kama kipaji ni nini? Hivi ni kweli kila mtu amezaliwa na kipaji au kuna baadhi ya watu wachache tu ambao wamebarikiwa ndio walizaliwa na kipaji? Kipaji ni kitu cha kuzaliwa nacho au unaweza kukipata ukubwani?
Safari hiyo tu imenifunza mengi ambayo unaenda kukutana nayo kwenye ebook hii hapa ya kipekee.
Kila Mtu Kazaliwa Na Kipaji Ila Hapaswi Kulinganishwa Na Mwingine
Nakummbuka Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba kila mtu ni gwiji, ila tatizo ni pale ambapo unamhukumu samaki kwa uwezo wake wa kupaa.
Hapo ndipo nilipogundua kumbe mimi na wewe tuna vipaji, ila sasa kipaji changu hakiwezi kufananishwa wala kulinganishwa na wewe.
Ni wazi kuwa kwa vyovyote vile samaki hawezi kuwa gwiji kwenye somo la kupanda mti, kupaa wala kukimbia. Yeye uwezo wake mkubwa upo kwenye kuogelea na huko lazima atafanya vizuri tu.
Sasa hivyo hivyo kwa kipaji chako. Hakiwezi kulinganishwa na mtu mwingine, unacho wewe na ni kwa ajili yako tu. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na kipaji kama cha kwako.
Mgawanyo Wa Kitabu
Kwenye ebook hii hapa nimeeleza kipaji kwa kina hasa ili hata kama ebook hii anaisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa kuhusiana na kipaji.
Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.
Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako. Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.
Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.
Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.
Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na inatenti.
Kwenye sura ya saba tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?
Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.
Kupata YALIYOMO YA EBOOK HII BONYEZA HAPA
Mafunzo haya yapo kwenye ebook ambayo unaweza kuipata kwa elfu 5 tu. kuipata ebook hakikisha kwamba lipie elfu 5 kwa 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. ukishalipia utanitaarifu kwa namba hiyohiyo ili niweze kukutumia hiyo ebook.
-
Kipaji Ni Dhahabu: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kutumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

Kitu Kimoja Muhimu Usichokijua Kuhusu Darasa Rasmi La Uandishi Mwaka 2022
Kuanzia tarehe 16 machi, 2022 tutakuwa na darasa rasmi la uandishi. Darasa hili maalumu litahusisha watu wachache tu. Watu 10.
Ukihudhuria darasa hili:
👉Utaandika kitabu chako na kitakamilika ndani ya siku 30.
👉 Nitakusimamia na kusoma kazi zako unazoandika kila siku na kukusaidia kuziboresha.
👉 Nitakufungulia blogu ya bure.
👉 Utajifunza mengi kutokana na yale wanayoandika wenzako na maoni nitakayokuwa natoa kuhusu kazi za wenzako.
👉 Utapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.
👉 Utapata jarida lenye hatua 15 za kufuata ili kuandika magazetini.
👉 Utapata mafunzo ya audio zaidi ya 10. Yakiwemo mahojiano na waandishi wakubwa hapa nchini.
👉 Utaungana na waandishi wengine wanaoandika na kujifunza mengi kutoka kwao.
Pamoja na hayo leo nataka nikwambie kitu kimoja tu usichokijua kuhusu darasa hili.
Kitu hiki ni kwamba ukihudhuria darasa hili huna chochote cha kupoteza.
Gharama ya kuhudhuria darasa hili la kipekee ni laki mbili (200,000/-)
Ila huna chochote cha kupotezaHuna cha kupoteza.
Wakati wa darasa au baada ya darasa kuisha, ukiona kwamba kile ulichopata hakiendani na thamani ya fedha uliyotoa. Utaniambia na mimi nitakurudishia fedha yako bila kukuuliza swali lolote.
Yaani, sentensi hiyo ulivyoisoma ndivyo ilivyo leo na ndivyo itakuwa tarehe 17.Aprili siku moja baada ya kumaliza darasa letu.
Huna chochote cha kupoteza.
Unaweza kuuliza kama ni hivyo, sasa si bora watu wahudhurie bure tu kwenye hili darasa? Itakuwaje kama watu wote watadai fedha zao baada ya darasa.
Ninachotaka ufahamu ni kwamba darasa hili ni la kipekee sana. Nina uhakika na kile unachoenda kujifunza. Nimealiandaa likaandalika, nimelipika likapikika. Kwa hiyo mtu yeyote ambaye atahudhuria darasa hili atapata thamani mara 10 zaidi ya atakavyolipia.
Thamani ya darasa hili ni kubwa Sana. Ndio maana kwa uhakika kabisa nasema kwamba endapo mtu atakuwa hajaridhika na hii thamani ambayo ni mara kumi zaidi basi nitamrejeshea fedha yake. Darasa limepikwa, likapikika!
Kama kweli upo siriazi kujifunza kuhusu uandishi. Basi fanya hivi.
JIUNGE na darasa hili leo hii.Nakuhakikishia kuwa huu unaenda kuwa uamuzi wako bora kuwahi kutokea.
Fanya malipo sasa hivi kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili ujihakikishie nafasi yako.
Wako,
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Maswali Unayopaswa kuwauliza watu waliofanikiwa
Ukikutana na mtu ambaye amefanikiwa, usitoke bure kwake. Kuwa mdadisi ili uweze kujua ni kitu gani ambacho kimeweza kumpa mafanikio makubwa.
Yafutayo ni maswali ambayo unapaswa kuwauliza watu waliofanikiwa?
1. Imekuwaje umefanikiwa wakati wengine huona siyo rahisi kufanikiwa maishani?
2. Unawezaje kuendesha miradi mikubwa wakati mimi nahangaika na miradi midogo?
3. Nini siri ya mafanikio yako?
4. Ni kitu gani kinakupa hamasa ya kuendelea zaidi?
5. Ulianza anzaje? Je, tangu unaanza maisha ulikuwa hivi?
6. Una mipango gani miaka 10 ijayo?
Usichoke kuuliza maswali. Kila unapokutana na mtu aliyefanikiwa jua kuwa kuna vitu vingi vya kujifunza kutoka kwake. Hivyo basi, kuwa tayari kumuuliza, kitu ambacho kimeweza kumfanya afanikiwe.
Hiki Kitu kitakupa nguvu zaidi wewe na kukufanya usonge mbele zaidi.
Kwanza, utaona kwamba mafanikio siyo kitu cha watu wachache. Na wewe pia unaweza kufanikiwa.
Lakini pia utaona kwamba na wewe ndoto zako zinawezekana. Kama huyu kaweza na mimi nitaweza.
Tatu, utaona kuwa unaweza kuanzia popote ulipo na bado ukatoboa kwenye maisha.
Nne, utapata ule mtazamo halisi wa kimafanikio kutoka kwa mtu aliyefanikiwa.
Mimi nakutakia kila la kheri.
1.KUMBUKA kwamba mafanikio ni haki yako ila tofauti na haki nyingine. Mafanikio hayadaiwi mahakamani. Unapaswa kupambana kuhakikisha kwamba unayapata.
2. Ukitaka kupata matokeo yasiyo ya kawaida, sharti ukubali kufanya vitu ambavyo siyo vya kawaida.
3. Ukitaka kupata matokeo ambayo hujawahi kupata, sharti ukubali kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya.
Kila la kheri.
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Je, kizazi kijacho cha Mabilionea wa Afrika kitatokea wapi?

Takwimu zilizotolewa na gazeti la Forbes ni kwamba karibia bilionea mmoja anatengenezwa kila baada ya dakika moja. Hii Ndio kusema kwamba fursa za kutengeneza mabilionea zaidi zinazidi kuongezeka.
Nafasi ya wewe kutengeneza ubilionea pia ipo, lakini endapo tu utaifahamu na kuiishi misingi na kanuni za kibilionea.
Kwa leo ninataka nikuelekeze eneo ambapo mabilionea wajao wa Afrika watatokea. Yapo maeneo 11 kama ambavyo nimeyaeleza kwenye kitabu Cha SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA ila kwa Leo na kwa ufupi sana nataka nizungumzie eneo moja tu.
Kilimo. Afrika imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri yenye kilimo.
Idadi ya watu Afrika inazidi kuongezeka kila siku. Na watu hawa wanahitaji kula.
Mambo mengine yanaweza kubadilika ila kula kutabaki palepale. Pengine MATUMIZI ya mtandao wa intaneti yanaweza kubadilika ila hatutaacha kula.
Idadi ya watu duniani kwa ujumla pia inazidi kuongezeka na ongezeko hili linahitaji chakula pia.
Kwa misingi hiyo basi, sisiti kusema kwamba kilimo ni mojawapo ya eneo ambalo linaenda kutengeneza mabilionea wapya Afrika. Kwenye ebook ya SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA nimeeleza kwa kina hili.
Ila kwa hapa itoshe tu kusema kuwa kilimo Ni SEKTA muhimu sana ya kuangalia kwa jicho la pili.
Ndio maana mimi nimeshaanza harakati zangu za kuhakikisha kwamba natengeneza mabilioni yangu huku.
Mfano mzuri tu hapa Tanzania. Kuna mazingira yanayoruhusu kuzalisha karibia kila zao. Lakini cha ajabu ni kuwa unaweza kwenda supermarket na kukuta kuna mazao ya nje ya nchi yanauzwa.
Wewe kama kijana unaweza kuchagua baadhi ya mazao na kukomaa nayo, ukayazalisha kwa viwango vizuri kiasi cha kuweza hata kusafirisha nje ya nchi.
Hivyo, ukaliteka soko la ndani na nje ya nchi. Upo tayari kwa ajili ya hii safari.MAFUNZO ZAIDI
-
Kama Bado Hujapata Nafasi Ya Kushiriki Darasa La Uandishi Kwa Mwaka 2022 Chukua Hatua Sasa Hivi
Tunategemea kuwa na darasa rasmi la uandishi kwa mwaka 2022. Darasa hili la kipekee litaanza rasmi tarehe 16 machi.
Kama ulikuwa huna habari basi taarifa rasmi ilitolewa HAPA HAPA na BAADAYE ikatolewa hapa.
Idadi ya watu ambao watashiriki kwenye darasa hili hapa la kipekee Ni kumi tu, na nafasi zinazidi kupungua kila kukicha. Hivyo, kama hujachukua hatua ya kujiunga, fanya hivyo leo.
Kuna kitu gani cha kipekee kwenye hii semina?
Kozi hii ni ya waandishi, siyo wale wanaojiita waandishi, ila waandishi wanaoandika, hicho ndiyo kitu Kikubwa tunachopambana nacho kwenye hii kozi. Hata kama hujawahi kuandika,
Mpaka kozi inafikia mwishoni utakuwa tayari umeshaandika, siyo mara moja, siyo mara mbili, ila utakuwa umeandika kiasi cha kuweza kumaliza kitabu chako.
Hiki ni kitu siyo tu ambacho nakwambia kwa nadharia, ila ni kitu ambacho watu wengine wamekifanyia kazi kwa mafanikio makubwa, Nina uhakika kama upo siriazi pia utaweza kukifanyia kazi.
Sasa kama kuna watu wametumia mbinu hizi ninazofundisha kuandika na kukamilisha vitabu vyao, unadhani wewe utashindwa?
Kozi imeandaliwa katika mfumo wa kukufanya uandike na ukamilishe lengo lako ndani ya muda wa kozi. Ukijiunga na kozi tutawasiliana na kuweka mpango. Utaweza kuandika hata kama hujawahi kuandika.
Hivyo kwa mara ya kwanza baada ya kuhudhuria kozi hii utakuwa mwandishi. Yale masuala ya kujiita mwandishi mtandaoni wakati hata hujawahi kuandika kwishney.
Kozi hii ina mwongozo uliokamilika na ina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi.
Mbali na hilo kwenye kozi hii:
👉Utaandika kitabu chako na kitakamilika ndani ya siku 30.
👉 Nitakusimamia na kusoma kazi zako unazoandika kila siku na kukusaidia kuziboresha.
👉 Nitakufungulia blogu ya bure.
👉 Utajifunza mengi kutokana na yale wanayoandika wenzako na maoni nitakayokuwa natoa kuhusu kazi za wenzako.
👉 Utapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.
👉 Utapata jarida lenye hatua 15 za kufuata ili kuandika magazetini.
👉 Utapata mafunzo ya audio zaidi ya 10. Yakiwemo mahojiano na waandishi wakubwa hapa nchini.
👉 Utaungana na waandishi wengine wanaoandika na kujifunza mengi kutoka kwao.
Nafasi kwenye kozi hii ni 10 tu. Hivyo, kama unataka kuhudhuria kozi hii, sharti uwahi kujihakikishia nafasi yako kabla hazijaisha.
Na gharama za kuhudhuria darasa hili la kipekee itakuwa ni laki mbili (200,000/) tu. Jihakikishie nafasi yako Sasa hivi kwa kuwasiliana na 0755848391 kabla nafasi hazijaisha.
NAKUKUMBUSHA TU: kozi hii ni ya siku 30 tu, na huna kitu chochote cha kupoteza. Endapo utajiunga na kozi hii ila katikati mwa kozi au mwishoni ukaona kuwa haifai, utanipigia simu nami nitakurejeshea fedha yako bila kukuuliza maswali yoyote.
Hivyo, jisajili sasa hivi kwa kuwasiliana na 0755848391.
Nafasi zimebaki chache.