Category: Uncategorized

  • Badili Fikra zako Ili Ubadili Maisha Yako

    Mwandishi nguli wa vitabu anayejulikana kama Napoleon Hill, alikiita kitabu chake THINK AND GROW RICH. Ikiwa na maana kwamba fikiri na uwe tajiri. Najiuliza “hivi kwa nini mwandishi huyu hakuiita kitabu hiki, FANYA KAZI KWA BIDII ILI UWE TAJIRI.au kwa nini hakukiita, jitume sana ili uwe tajiri.Au pengine kukiita pambana uwe tajiri. Alitumia tu neno…

  • Hivi Ndivyo Huwa Napata Mawazo Kuandika Ya Makala Kila Siku

    Moja kati ya swali ambalo ninakutana nalo kila siku, ni swali la  “Je, ninapata wapi vitu vya kuandika kila siku”? Huwa napenda kujibu swali kirahisi sana kama swali lenyewe lilivyo rahisi? Huwa nauliza watu unapata wapi cha kuongea kila siku? Wengine huwa wanasema, unajua kuongea sio sawa na kuandika. Sasa hapa nataka kukuonesha wapi huwa…

  • Hii Ndio Hali Ambayo Huwa Naipata Nikiwa Naandika Makala Za Blogu Au Magazetini

    Moja kati ya muda ambapo huwa ninakaa na kufikiria sana ni pale ninapoanza kuandika. Kinachonifanya nifikiria sana ni pale ambapo huwa nafikiria makala hii itasomwa naRaisi wa nchi lakini pia itasomwa na mtu wa kawaida kijijni.Makala itasomwa na wasomi wa vyuo vikuu (wenye Phd) pamoja na watu walioishia darasa la kwanza au ambao hawajasoma darasa…

  • MAKALA YA 599: KUTOKA MAKTABA YA SONGAMBELE; ITAMBUE KAZI YAKO.

    makala hii iliandikwa  kwa mara ya kwanza machi 23 2017 Kazi kubwa sana ya vyombo  vya habari ni kuyoa habariKazi ya jembe ni kulimaKazi ya kalamu ni kuandikaKazi ya gari ni kusafirisha watuKazi ya maji kukata kiuKazi ya chakula ni kusjibisha wenye njaa na kutoa virutubishoKazi ya Je wewe kazi yako ni ipi? Itafute kazi…

  • HII NI NJIA BORA YA KUPOTEA

    Katika maisha kama unataka kupotea, basi anza kuwaiga wengine. Anza kuishi kama wengine na fanya kama ambavyo watu wengine wanafanya. Hii ni njia bora sana ya kupotea. Kuna wewe mmoja tu. Na unapaswa kujisikiliza kwa umakini sana. Usifanye kitu kutaka kuwaridhisha wengine, tafuta kujiridhisha mwenyewe Usitafute kuonekana na wewe umo, jiridhishe wewe kwanza. Mtu mmoja…

  • NI MARUFUKU KUKATA TAMAA

    Mtu mmoja amewahi kusema kwamba hapa duniani kila mtu ana kazi yake. Kuna watu kazi yao ni kukatisha tamaa. Kwa hiyo ukiona mtu anakukatisha tamaa, jua yupo kazini. Na wewe endelea na kazi yako.Ila cha msingi ni kwamba, kazi za watu wengine zisikukwamishe wala kukuzuia kusonga mbele. Nakumbuka siku ya kwanza nilipoandika makala na kuiweka…

  • NI MARUFUKU KUKATA TAMAA

    Mtu mmoja amewahi kusema kwamba hapa duniani kila mtu ana kazi yake. Kuna watu kazi yao ni kukatisha tamaa. Kwa hiyo ukiona mtu anakukatisha tamaa, jua yupo kazini. Na wewe endelea na kazi yako.Ila cha msingi ni kwamba, kazi za watu wengine zisikukwamishe wala kukuzuia kusonga mbele. Nakumbuka siku ya kwanza nilipoandika makala na kuiweka…

  • Usiogope Kushindwa, Ni Sehemu Ya Kujifunza

    Thomas Edison anafahamika kwa ubunifu wake wa vitu vingi sana. Moja kati ya kauli yake ambayo amewahi kuisema ni hii hapa, “siku zote naogopa vitu ambavyo huwa nagusa mara ya kwanza na vinafanya kazi pale pale”. Maana yake, nini? Maana yake vitu hivyo havijakupa nafasi ya kujifunza. Na havijakupa nafasi ya kukua zaidi. Sio kwamba…

  • NI KOSA KUJUA KITU, UKAJIFICHA NA KITU HICHO

    Kwenye kitabu chake cha think big, Ben Carson anaelezea kisa kilichomkuta siku moja.  Ipo hivi kuna jamaa alimfuata Ben Carson na kumwambia, “yaani wewe Ben, ukijua kitu hutulii. Unataka kila mtu ajue kwamba unajua”. Sikumbuki vizuri Carson alimjibu nini huyu jamaa, ila leo napenda kusema kwamba kama kuna kitu unajua na unajificha hutaki kukionesha ni…

  • THINK DIFFERENT AND JUST DO IT

    Baada ya kurudi kwenye kampuni ya apple mwaka 1997, Steve Jobs alirudi na falsafa ya THINK DIFFERENT. Wakati huo huo kampuni ya NIKE ya Phil Knights ilikuwa na falsafa yake ya JUST DO IT ambayo walianza kuitumia miaka ya themanini. Binafsi nazipenda falsafa hizi mbili.Kwanza falsafa ya Jobs ibakuhitaji kufikiri tofauti. Nimekuwa nikisema sana kwamba…

  • Huu Ni Muda Wa Matokeo Makubwa

    Ni nani asiyependa matokeo makubwa? Ni nani? Kila mtu hupenda matokeo makubwa katika kila eneo la maisha. Watu wanapenda mahusiano yenye mafanikio makubwa. Watu  wanapenda elimu ya kiwango cha juu. Watu wanapenda kuwa hela kiasi ambacho hawataweza kupata hofu.  Wanafunzi mashuleni wanapenda kupata ufaulu mkubwa na unaopendeza. Haya yote ni matokeo makubwa. Ila matokeo makubwa…

  • Hivi Nidvyo Kazi Za Sanaa Zinavyoweza Kukufanya Ufanye Makubwa Sana

    Binafsi ni mpenzi mzuri sana wa kazi za sanaa. Kazi hizi huwa zinanifanya nifikiri kwa kina sana na pengine huwa zinaniletea mawazo mengine ambayo ni bora zaidi kuliko yale niliyokuwa nayo awali. Kuzitafakari kazi hizi hunifanya niweze kutuliza akili yangu sehemu moja na kujiona bora zaidi.Wapo watu ambao hawaipendi sanaa kwa kusema wao ni wanasayansi,…

  • Hivi Ndivyo Mazoezi Yanaweza Kukufanya Ule Meza Moja Na Mfalme

    Katika mazingira yetu ya sasa hivi wafalme sio watu  waliozoeleka sana kulinganisha na kipindi cha nyuma. Zamani kidogo ulikuwa unakuta kabila fulani lina mfalme wake ambaye watu wote wanamsikikiza na sauti yake iko juu kwenye masuala ya utawala. Lakini pia mfalme kama kiongozi alikuwa anapata vitu vyote vizuri. Yaani kwake nguo zilikuwa ni nguo bora…

  • Hatua Muhimu Za Kuchukua Unapojikuta Una Mambo Mengi Ya Kufanya Na Muda Ni Mchache

    Mambo ni mengi, muda ni mchache. Huu ni usemi ambao unapata umaarufu sasa hivi. Labda swali ambalo tunapaswa kujiuliza sasa hivi, Je, mambo ndio yameanza kuwa mengi sasa hivi? Mambo ni mengi siku zote. Hakuna siku ambapo mambo yamegeuka kuwa machache. Watu pekee wenye mambo machache ni wale ambao wameaga dunia. Kutokana na wingi huu…

  • Kitu Hiki Ndicho Kimefanya Maisha Kuzidi Kuboreshwa Kila Siku

    Leo hii akirudi mtu mmoja ambaye aliishi miaka 2,000 iloyopita na kuona kinachoendelea hapa duniani atashangaa sana.Kila kitu kwake utakuwa mshangao. Sio tu namna tunavyovaa nguo nzuri bali pia tunavyolala mahali pazuri.Sio tu namna tunavyowasiliana tukionana kwa simu bali pia usafiri wa mabasi, ndege na majini ulivyobadilika. Yaani kila kitu kimebadilika kabisa.  Hadi vyakula tunavyokula,…

  • Huku Ndipo Unapaswa Kuwekeza Asilimia Kubwa Ya Muda Wako

    Siku moja ina masaa 24. Ndani ya muda huu (yaaniasaa 24) kuna muda wa kulala, kufanya kazi, kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine. Muda wote huu ukiuunganisha unapata karibia masaa 20 ambayo yanatumika. Ila cha kufurahisha ni kwamba unabakiza masaa 4 ambayo yapo yapo tu. Watu wengi huyatumia masaa haya kuangalia tamthiliya, kupiga soga na…

  • Masomo Saba (07) Ya Kujifunza Kutoka Kwa Wajasiliamali Wakubwa

    “Kila mtu atapaswa kufanya walau kitu kimoja kikubwa katika maisha yake” huu ulikuwa ni wosia wa  Sakichi Toyoda kwa wanae  Kiichiro Toyoda. Sakichi alikuwa ameanzisha kampuni ndogo ya kutengeneza vifaa vya magari na sasa wakati miaka inaenda na anakaribia kifo chake basi ikabidi atoe wosia huu kwa mwanae. Wosia huu uliambatana na kumkabidhi mwanae biashara…

  • Ukiweza Kumpa Mtu Kitu Hiki , Basi Utapata Chochote Unachotaka Kutoka Kwake

    Kila mtu huwa kuna kitu ambacho anapendelea zaidi ya mwingine. Unaweza kukuta huyu anapenda mziki, lakini mwingine akawa anapenda kusafiri.Moja ya kitu ambacho utapaswa kujifunza katika maisha basi ni kuwapa watu  kitu ambacho wanataka. Hili sio tu kwa watu. Hata mvuvi anajua ili kumpata samaki basi atapaswa kumpa chambo. Sio kwa sababu eti anapenda maziwa…

  • MAAJABU; Ona Kinachoendelea Kwenye Ulimwengu Wa Sasa. Watu Wameacha Kujifunza, Mashine Ndizo Zinajifunza

    Kati ya vifaa vizuri ambavyo tunavyo kwenye zama hizi hapa basi ni Simu za mkononi na kampyuta. Vifaa hivi ni muhimu sana maana vinarahisisha maisha lakini pia vinasogeza taarifa karibu. Tatizo linakuja linawakuta watumiaji wa vyombo hivi kiasi kwamba wanakuwa mateja.Kwa sasa sio jambo la kushangaza kukuta watu waliopanga na wametumia nauli zao kutoka mbali…

  • Hii Ni Kwa Wale Tu Wanaohitaji Mafanikio Kama Vile Wanavyohitaji Kupumua

    Siku moja kijana mdogo alimwendea Socrates ili amuulize siri ya mafanikio. Alichofanya  Socrates alimwambia njoo kesho muda fulani, tutakutana  kwenye mto. Kesho yake kijana alijiandaa na kufika eneo husika. Socrates alianza kuingia kwe maji huku akimwambia kijana nifuate. Kijana alishangaa huyu ananipeleka wapi? Waliingia kwenye maji na kina cha maji kilianza kuongezeka. Ghafla Socrates alimshika…

X