Author: Godius Rweyongeza

  • Hii Ndio Maana Kuu Ya Cheti, Na Cheti Kikuu Ulichopewa Bure Kabisaaa

    Duniani kuna zawadi na vyeti vingi sana ambavyo vimewahi kutolewa. Kama umesoma shule kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo basi utakuwa una rundo kubwa sana la vyeti.  Lakini Swali ni je, vyeti hivi unavihitaji vyote? Utavitumia wapi? Maana sasa hivi imefikia hatua hadi kuhudhuria semina watu wanatoa vyeti. Ukisoma vitabu watu wanakupa vyeti.  Sasa hivi…

  • Huyu Ni Mtu Ambaye Lazima Utamwambia Hapana

    Kila siku huwa ni fursa mpya. Fursa kuanzia watu tunaokutana nao. Watu tunaoongea nao, vitu tunavyofanya n.k Sasa fursa hizi huwa zinategemea ni kwa jinsi gani ambavyo mtu anaenda kuzitumia. Moja ya fursa ambayo inajitokeza ndani ya siku katika maongezi ni kukubali au kukataa. Kusema ndio au Hapana. Kuna watu wanafikiri kwamba haya ni maneno…

  • Kitu Kikubwa Unachoweza Kufanya Juu Ya Ndoto Yako Kuu

    Safari ya maisha inahusisha mambo mengi sana. Katika safari hii kuna watu wana kusudi kubwa ambalo wanapaswa kulitimiza na kuna watu wenye ndoto kubwa mno. Ndoto ni picha kubwa ya kesho yako ambayo unaijenga leo.Ndoto ni jambo kubwa sana ambalo linakufanya usilale (halikupi usingizi) mpaka utakapokuwa umelitimiza. Kutokana na ukubwa wa ndoto ambazo watu huwa…

  • Hili Ndilo Wazo Kubwa Sana Kuwahi Kutokea

    Duniani kumekuwa na mawazo makubwa ambayo yameweza kubadili mwonekano wa dunia hii. Wazo la kuweka ndege angani lilikuwa ni wazo kubwa sana ambalo kiukweli mpaka sasa Kila mtu ni shuhuda kwamba limebadili mwonekano wa uso wa dunia. Wazo la kujenga ghorofa lilikuwa ni wazo kubwa sana ambalo kila anayeona jengo aina ghorofa leo hii lazima…

  • Mambo Matano (05) Unayoweza Kufanya Ukiwa Katika Mazingira Yanayokufanya Usijiamini

    Moja kati ya vitu muhimu sana ambavyo unahitaji  katika maisha yako basi ni kujiamini. Kujiamini katika kazi unayofanya.Kujiamini katika kile unachoongeaKujiamini unapokuwa na watu n.k Ubora Wa kujiamini ni kwamba unaonekana kwa macho. Yaani mtu anaweza kukuona kabisa na kukwambia kwamba hujiamini. Hii ni kutokana na tembea yako, ongea yako na mwonekano wako. Sasa leo…

  • Hapa Ndipo Mabadiliko Makubwa Huanzia

    Maisha yanahusisha mabadiliko mengi sana. Kuna mabadiliko ya vipindi vya mwaka. Kuna mabadiliko ya hali ya hewa. Kuna mabadiliko kati ya siku moja na nyjngine. Kuna mabadiliko kutoka sehemu moja kwenda nyngine.Kuna mabadiliko kati ya mwaka mmoja na unaofiata. Mabadiliko haya hutufanya tukae tukijua kwamba hatupaswi kutulia na kitu kimoja au kuridhika na hali ile…

  • Mwandikie Mtu Huyu Barua Ya Kurasa Mbili Leo

    Naam rafiki yangu. Siku zinazidi kusogea Mbele na maisha yanazidi kuwa bora zaidi. Tangu mwaka huu umeanza kuna hatua ambazo umekuwa unapiga kila siku. Inawezekana hatua hizi ni ndogo sana ila ni muhimu sana maana mafanikio makubwa sana huwa ni muunganiko Wa vitu vidogo vidogo ambavyo tunaviunganisha kila siku. Mwisho wa siku muunganiko wa vitu…

  • Huu Ndio Upenyo Ambao Unapaswa Kuutumia Kusoma Vitabu

    Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya kipekee sana. Hii ndio siku ambayo unapaswa kuitumia kuhakikisha kwamba unafanya makubwa sana. Kati ya visingizio vya watu wengi sana kuhusu kusoma vitabu ni kwamba hawana muda.Leo hii napenda nikupe upenyo mdogo ambao utautumia kusoma vitabu kila siku. Na upenyo huu upo kwenye muda wa ziada…

  • Hii Ndio Njia Bora Ya Kujiinua Mwenyewe

    HII NDIO NJIA BORA YA KUJIINUA MWENYEWE Hongera sana  rafiki kwa zawadi ya kipekee sana. Hii ndio siku iliyoandaliwa kwa ajili yako. Ifurahie na kuhakikisha unaitumia vyema kabisa. Kila siku ni siku yako wewe kuhakikisha unakuwa bora sana kuliko jana. Yaani kujiinua.  Unapaswa kujiinua kwa vitendo, maneno, na wajibu, shughuli zako unazotimiza kila siku. Ila kama…

  • Hivi Ni Vitu Ambavyo Ni Rahisi Sana Kutovifanya

    Ninajua kwamba kila siku unakuwa na majukumu mengi sana ya kutimiza. Kuanzia majukumu ya kazi, biashara, familia na mengine mengi. Kati ya hayo majukumu huwa unajikuta huyatimizi kila siku.Sio kwamba huyatimizi kwa sababu ya ukubwa wake. Bali huyatimizi kwa sababu ya hujajua kitu hiki kimoja. Na kitu chenyewe ni kwamba  MAJUKUMU MADOGO NDIO HUWA YANAWASHINDA…

  • Hii Ndio Aina Ya Maarifa Unayopaswa Kuyapata

    Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana.Kama umesahau ni kwamba zimepita siku 19 tangu mwaka huu uanze. Sasa karibu sana kwenye somo la leo. Watu huwa wanaanzisha vitu ila huwa havidumu. Kuna watu huwa wanaanza kusoma  ila mwisho wa siku hawamalizi kozi wanazozianza.Kuna watu huwa wnajiunga na mafunzo fulani mtandaoni ila mwisho…

  • Hizi Ni Baraka Zako Unazopaswa Kuhesabu

    Bila shaka umewahi kusikia usemi unaosema kwamba hesabu baraka zako! Usemi huu unapenda tuwe watu wa kushukuru nakuona mazuri pale ambapo wengine wanaona mabaya. Kiukweli kuna mambo mengi sana ambayo unaweza kushukuru Kila iitwayo leo. Ni mengi sana ndio maana unapaswa kuhesabu baraka zako.Ebu ona hapa;1. Leo hii bado unavuta pumzi na kuishi wakati kuna…

  • Haya Ni Mambo Ya Kipekee Sana Usiyoyajua Kuhusu Biashara

    Hivi ushawahi kuanza kitu baadae ukaja kugundua kwamba picha uliyokuwa nayo juu ya kitu ni tofauti? Au umewahi kupata safari ya kwenda mahali ambapo hukuwahi kwenda kabla, ukawa unajenga picha katika akili yako, ila ikatokea kwamba picha ya eneo uliyojenga ni tofauti na uhalisia? Je, umewahi kuwa unawasiliana na mtu katika simu ambaye hujawahi kukutana…

  • Vitu Vitano Vinavyoharibu Ubunifu Wa Watanzania

    Moja kati ya vitu muhimu sana katika biashara, mahusiano na kazi ni ubunifu. Ni kupitia ubunifu mtu unaweza kuja na mbinu mpya za kuongeza wateja, ni kupitia ubunifu unaweza kujua ni bidhaa gani ukiiboresha zaidi itakuongezea wateja zaidi. Ni kupitia ubunifu utajua ni bidhaa gani ukiipunguza  au ukiiondoa kwenye mfumo wako wa biashara utakuwa hujapungukiwa…

  • Zawadi nne(04) Kubwa Inazoweza kujipatia 2019

    Tumezoe kwamba huwa tunanunua zawadi kwa ajili ya rafiki zetu, ndugu jamaa na marafiki.Na pengine huwa kuna misimu ambapo watu hujikita zaidi katika kununua zawadi. Watu huiita misimu hii kwamba ni misimu ya zawadi.Misimu hii inaweza kuwa ni ya sikukuu au siku ya wapendanao, siku ya mama au baba n.k Katika kipindi hiki huwa tunawanunulia…

  • Kitu Hiki Huwezi Kukiepuka Mwaka Huu

    Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana. kwa hakika leo ni siku ya kipekee sana ambayo wewe unapawa kuhakikisha kwamba unaitumia vyema sana ili uweze kusonga mbele na kujikuta kwamba unafanya mambo makubwa. Kwa kawaida kuna vitu ambavyo huwa unaambiwa kwamba uviepuke ilil uweze kuwa na maisha ya namna fulani. Au kabisa unaambiwa…

  • Kama Tatizo Ni Nyota Ya Kwako Imeenda Wapi?

    Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi hii ya kipekee sana. Zawadi ya maisha. Moja kati ya vitu vinavyoongelewa sana na watu ni nyota. Mtu akifanikiwa wanasema ni nyota. Asipofanikiwa pia wanasema ni nyota. Mtu akijenga mahusiano mazuri wanasema ni nyota. Lakini pia mahusiano yake yakiwa mabaya wanasema ni nyota.  Imefikia hatua sasa watu wamesahau misingi…

  • UCHAMBUZI WA KITABU; THE 5 AM CLUB, Miliki asubuhi yako, miliki maisha yako

    Kitabu Cha THE 5 AM CLUB kilitoka katikati ya mwezi Wa 12, 2018. Binafsi, nilianza kukisoma wiki moja baada ya kutoka na nimekuwa nikikifanyia uchambuzi katika kundi LA HAZINA YETU TANZANIA. Mpaka ninaanza uchambuzi Wa Kitabu hiki nimesoma vitabu vingi sana, ila usomaji Wa Kitabu hiki umekuwa Wa kipekee sana.Kwa Mara ya kwanza nimeandika mambo…

  • Sheria Muhimu Unazopaswa Kuziishi

     1. Ongea kidogo zaidi ya wengine wanavyoongea. 2.shinda kwa matendo wala sio maneno. 3. Omba msaada pale unapouhitaji.  Usitake kushinda peke yako, tafuta kuwafanya with watu wengine ndipo na wewe utshinda zaidi (win-win) 4. Tumia kutokiwepo kwako, kufanye kuwa kwa manufaa.Ni bora watu wakasema, kwa nini sijakuona muda mrefu, kuliko watu kuuliza, hivi na leo…

  • Hili Ni Jambo Litakalokupa Uhuru Maishani Mwako

    Uhuru! Uhuru! Uhuru! Miaka mingi sana Tanzania ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni. Mara tu baada ya uhuru mwalimu Nyerere alikuwa na haya kusema. Watanzania tunapaswa kupambana na maadui wakuu watatu ambao ni ujinga umasikini na maradhi.Vitu hivi vitatu mwalimu aliviita maadui wa taifa. Ila dawa ya vitu hivyo vyote vitatu ilikuwa ni elimu.Ujinga ni matokeo…

X