Category: Uncategorized

  • TATIZO LAKO WEWE

      Kama naona jinsi utakavyoruka andiko hili . Maana umeona pameandikwa TATIZO LAKO, basi unaona ulipite ukaendelee na mambo mengine. Hutaki kujua tatizo lako ni nini. Ndivyo ilivyo kwa wanadamu, mtu akisikia yanaongelewa matatizo ya wengine Basi ndio kwanza anatega sikio ili ayasikie vizuri wakati utakuta na mwenyewe  ana matatizo Kama hayohayo. Tena unaweza kukuta…

  • Vitu Vitano Vya Kuepuka Unapoamka Asubuhi

    Moja, epuka kusikiliza taarifa ya habari. Asubuhi ni muda ambao akili inakuwa inafanya kazi kwa viwango vya juu, utumie muda huu kusoma na kujifunza mambo ya maana badala ya kusikiliza taarifa ya habari ambayo ni hasi. Soma Zaidi: Sababu Tano Kwa Nini Unashindwa Kuamka Asubuhi Na Mapema Na Kitu Gani Unaweza Kufanya Sasa Hivi Pili, epuka…

  • Kuanzia Chini Ni Tiketi Ya Kufika Juu

      Kuanzia chini kusikuzuie wewe kuendelea kuiona picha kubwa. Endelea kuiona picha kubwa hata kama umeanzia chini.Kuanzia chini kuwe Ni tiketi ya wewe kuzidi kupanuka kila Mara. Usikubali kubaki nyuma Nakushukuru sana kwa kuweza kufuatilia somo hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA…

  • RIPOTI MAALUMU: HATUA 15 ZA KUFUATA ILI KUANDIKA MAGAZETINI

    Watu wengi wamekuwa wakiniuliza Hivi na mimi naweza kuandika kwenye magazeti? Napataje namba za wahariri? Hili swali au mengine ya aina hii yamekuwa yakija kwangu mara mara. Sasa kutokana na uzoefu wa takribani miaka mitatu wa kuandika magazetini nimeandika ripoti maalumu kueleza kiundani kuhusu uandishi wa magazetini. 1. Hatua muhimu za kufuata ili kupata nafasi…

  • Ninawezaje kununua hisa na ninatakiwa kuwa na shilingi ngapi?

      Inategemea unanunua hisa za kampuni gani.  Kuna hisa ziko juu kwa bei na nyingine ziko chini. Hivyo kiwango kitatofautiana ila ukiwa na fedha ya hisa kumi, unaweza kununua. Iko hivi. Tuseme wewe unapenda kununua hisa za kampuni SMB (SONGA MBELE BLOG). Hahah! Halafu, hisa za kampuni hii zinazuzwa kwa shilingi 500 kila hisa. Hii…

  • Kitu muhimu unachopaswa kukifurahia

    Wafuatiliaji wa mpira huwa wanapenda sana kufuatilia ligi kuu na kuona jinsi ambavyo timu yao inazidi kupanda juu kwenye viwango. Kitu hiki hufanya wajue kwa hakika nini kinaendelea na nini kinaweza kufanyika ili timu yao iendelee kuwa kileleni. Sasa na wewe kuna mchezo ambao unaweza kuufurahia. na mchezo huu ni mchezo wa kukuza utajiri wako.…

  • Kama huoni pa kuanzia kabisa ili kupata fedha Basi Anza

    1. Kwa kutumia nguvu zako (fanya kazi kutumia nguvu zako ulipwe) 2. Kwa kutumia muda wako (Kuna watu wako bize na wewe una muda wa kutosha tu. Utumie kuwasaidia hao watu ili wakulipe) 3. Tumia ujuzi wako (Sasa sijui wewe una ujuzi gani, kama hauna ujuzi wowote futa app ya facebook kwa mwezi mzima Kisha…

  • MAKOSA Matano Yanayokurudisha Nyuma Kiuchumi

    Kuna makosa matano ambayo watu wanafanya, kitu kinachosababisha watu hao warudi nyuma. Yaepuke makosa haya kama ukoma Moja ni kosa la kununua bando la kuchati, kufuatilia maisha ya watu wengine. USHAURI: KAMA hauna kitu cha maana cha kuongea na watu wala kufanya mtandaoni bora usinunue  bando. Itumie hiyo fedha kuweka akiba au kuwekeza. Pili, kuwekeza…

  • JINSI ya kunufaika na blogu kwa kazi yako unayoifanya.

    Jana juna mtu alinifuata inbox na kuniuliza swali hili hapa. Kaka , salama ? Mimi nawezaje kunufaika na blog kazi yangu ni mhubiri neno la Mungu Ujimbe niliomjibu naamini utakuwa wa msaada kwako pia nilimjibu hivi. 1. Mahubiri yako yatakuwa hewani na kutuzwa. Kitu ambacho kitawasaidia wasomaji wako hata ambao hawakujui kuweza kuyasoma kwa wakati…

  • Chagua kitu kimoja hapa

     Mwezi wa sita ndio huu umefika, nikusaidie nini? 1. Kuanzisha tabia ya kusoma vitabu itakayodumu 2. Nikusaidie uanze kuandika kitabu chako 3. Kujijengea tabia ya kuweka akiba hata kwa kuanza kidogo. 4. Kuachana na uraibu wa mitandao ya kijamii 5. Kuachana na uraibu mwingine. 6. Nikusaidie ujenge tabia ya kufanya mazoezi 7. Kuanza kutengeneza fedha…

  • Vitu Vitano Vinavyokuzuia Kufanikiwa

      Hufanikiwi kwa sababu unavunja Sana sheria za mafanikio. Na kama utaendelea kuvunja hizi sheria ujue utaendelea kukwama. Sasa zifuatazo ni sheria tano unazovunja. Zifuate kwa manufaa yako. Moja, Ni kile unachoingiza kichwani mwako. Ujue unachoingiza kichwani ndicho utatoa nje. Hivyo kuwa makini kuingiza kitu kizuri kichwani. Soma vitabu na kaa na watu chanya. Kumbuka,…

  • Mo Dewji Atoa Siri Tano Zilizomfanya kufanikiwa Sana

    Siku ya leo nimeona nikusogezee siri tano za mafanikio kama ambavyo Mo Dewji amezitaja kwenye mojawapo ya Twitter yake. Kwenye hiyo Twitter, Mo Dewji anasema; Toka nikiwa kijana nilikuwa na ndoto ya kuwa mjasiriamali.Safari ya ujasiriamali imejaa vikwazo matuta na kona nyingi. Unahitaji kuwa na nidhamu, ustahimilivu na zaidi adabu, kadri unavyosonga mbeleKutumia njia za…

  • Ujumbe Muhimu Kwa Wasomaji Wote Wa Vitabu

        Rafiki yangu habari ya siku ya leo. Hongera sana kwa nafasi ya siku hii ya kipekee sana. siku ya leo nina ujumbe muhimu kwako wewe msomaji mzuri wa vitabu. na ujumbe huu ni kwamba kama unafikiri kwamba unaweza kujifunza zaidi kupitia usomaji wa vitabu, basi unapaswa kuandika kitabu chako pia. Kama wewe umekuwa…

  • Kutana na Zhang Yiming, Billionea wa Kichina Na Mwanzilishi Wa TikTok Pamoja Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwake

      Zhang Yiming ni mwanzilishi wa mtandao wa kampuni mama ya ByteDance ambayo ipo nyuma ya mtandao Tiktok. Billionea huyu aliyezaliwa mwaka 1983 ana utajiri wa Zaidi ya bilioni 44. Siku siyo nyingi bilionea huyu alistaafu uongozi wake kwenye kampuni yake huku akisema kuwa kwa sasa anaenda kujisomea vitabu ili aweze kupata mawazo mengine mazuri…

  • Huduma Sita Muhimu Unazoweza Kupata Kutoka Kwangu

    Habari yako rafiki yangu. Siku ya leo nimeona nikushrikishe huduma  ambazo unaweza kupata kutoka kwangu. 1. HUDUMA YA VITABUMpaka sasa nimeandika vitabu 16. Unaweza kuona baadhi ya vitabu hivyo hapa. Chagua kitabu chochote unachoona kinakufaa, Kisha jipatie nakala ya kitabu husika. BONYEZA HAPA KUONA ORODHA YA VITABU VYANGU VYOTE. 2. HUDUMA YA KUJIFUNZA UANDISHIMoja ya…

  • Njia Tano Za Kuingiza Fedha Mtaani Kwako Kuanzia Leo

    Habari ya leo rafiki yangu. Siku ya leo nimeona nikuletee njia tano za haraka zitakazokufanya wewe kuanza kuingiza fedha kuanzia leo hapo mtaani Kwako. 1. Angalia kitu ambacho watu wanalalamikia sana kisha kifanye vizuri kwa kuondoa tatizo wanalolalamikia watu. 2. Tafuta sehemu yenye tatizo kisha litatue hilo tatizo. 3. Anza leo kufanya biashara ya mtaji…

  • Maeneo Matano Unapopaswa Kukaa Kimya

    Tumepewa mdomo na masikio mawili. Mara nyingi hiki kimekuwa kinatumiwa Kama kiashiria cha kuwa tunapaswa kuwa wasikivu.  Kuna mazingira ambayo wewe unapaswa kuwa kimya na usiongee sana. Sasa siku ya leo ninakuletea maeneo matano ambapo wewe unapaswa kuwa mkimya. Moja, kama unaona mtu unayeongea naye hakupi nafasi ya kuongea. Pili, pale unapoona mtu anaweza kukuelewa…

  • Ushauri Wa Mhe Jakaya Mrisho Kikwete Kwa Kijana anayetaka Kufanikiwa

      Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ni rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku ya leo nimeona nikuletee ushauri murua kabisa kutoka kwake ambao Nina hakika utakusaidia sana wewe. Mheshimiwa anasema kwamba, kama unataka kula lazima ukubali kuliwa. Hii ndiyo kusema kwamba huwezi kupata vinono kama hujakubali kuhenyeka kwanza. Ukitaka…

  • Nukuu Tano Zilizokonga Nyoyo Za Watu Kutoka Kwenye Kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

    Kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, ni kitabu ambacho kimeeleza kwa kina jinsi wewe unavyoweza kufanikisha NDOTO ZAKO na kufanya mambo makubwa. Kitabu hiki kina madini kuanzia mwanzo wa kitabu mpaka mwisho wa kitabu. Sasa kwenye hiki kitabu kuna nukuu nyingi ambazo zimekonga nyoyo za watu, ila leo nitakushirikisha nukuu tano tu. 1. …Ukweli…

  • Njia Tano Za Kusoma Vitabu Vikubwa Bila Kutumia Nguvu Kubwa

    Vitabu ni mojawapo ya njia ya kuongea na watu waliofanikiwa, viongozi maarufu, wanafalsafa, na hata watu wengine ambao tayari walishaaga dunia. Ni kupitia usomaji wa vitabu ndipo tunapata kuongea nao, kusikiliza maoni yao na hata kujadiliana nao mada fulani fulani. Sasa, watu wengi huwa hawapendi kusoma vitabu kutokana na ukweli kuwa vitabu vingine ni vikubwa…

X