-
Kuwa Mwanafunzi wa KUDUMU

Dr. Myles Munroe ni mmoja watu ambao walikuwa wamefanikiwa sana kwenye sekta ya maendeleo binafsi. Kazi zake nyingi zimegusa maisha ya watu wengi enzi za uhai wake mpaka leo hii. Siku moja alikuwa anaeleza namna alivyoenda kwenye duka la vitabu na kununua kitabu cha zaidiya dola 125. Dola 125 ni zaidi ya laki mblii na nusu za Tanzania.
Msaidizi wake alishangaa kuona kwamba Dr. Myles Munroe amenunua kitabu cha gharama kubwa hivyo. Kwa nini unatumia gharama kubwa hivyo kununua kitabu kimoja tu? Kw anini usitumie hii hela kufanya vitu vingine kama kununua nguo? Hapo ndipo Dr. Myles Munroe alipomwambia msaidizi wake kwamba, hiii ndiyo tofauti inayotutofautisha mimi na wewe. Ndiyo maana mimi ni kiongozi na wewe ni mfuasi. Unajua kwa nini alimwambia hivyo? Alimwambia hivyo kwa sababu alijua wazi mazuri yaliyo kwenye vitabu ambavyo msaidiz wake alikuwa bado hayajui.
Ukweli ni kuwa kwenye maisha ya kila siku ni kwamba unapaswa kuwa mtu ambaye anajifunza bila ukomo. Wekeza nguvu na muda wako kwenye kujifunza mara kwa mara bila ya kuchoka. Kamwe usifikie hatua ambapo utajiona kwamba umejifunza na umeju akila kitu kwenye maisha yako. kila mara unapaswa kuwa unaendelea kujifunza bila ya kukoma. Kujifunza ni tiketi ya wewe kufanya makubwa. Kujifunza kunakufanya unaona mbali kuliko pale ambapo unakuwa hujifunzi.
Kwenye haya maisha, kubali watu wakuite mzembe, ila siyo kwenye vitu viwili. Kwanza usikubali kuitwa mzembe kwenye kufanya kazi kwa bidii, na usikubali kuitwa mzembe kwenye kujifunza. Hivi ni vitu viwlii ambavyo unapasw akuwa unavipambania kila siku, bila ya kuacha na bila ya kujali kitu gani ambacho kinatokea kwenye maisha yako. hakikisha mara zote unapambana kushinda kila siku kwenye haya maeneo mawili.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kwa Kujiunga naye hapa
-
HITIMISHO LA KILA MAKALA
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.
Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
ISBN kwenye Kitabu Ni Nini Na Inafanya Kazi Gani?

ISBN kwenye kitabu ni Nini na inafanya kazi Gani?
Umeandika kitabu lakini Bado unajiuliza unawezaje kupata ISBN kwa ajili ya kitabu chako?
Umekuwa unaona ISBN kwenye vitabu mbalimbali lakini hujui maana yake ni nini, au unawezaje kuzipata?
ISBN (International Standard Book Number) ni namba ya kipekee inayotolewa kwa kila kitabu kilichochapishwa ili kukitambulisha kimataifa. Ina tarakimu 13 (zamani ilikuwa 10) na hutumiwa na wachapishaji, maktaba, na maduka ya vitabu kwa madhumuni ya kutambua na kufuatilia vitabu.
Namba hii inakuwa na maelezo kuhusu mwandishi, kuhusu kitabu na hutumika kutofautisha kitabu kimoja na kingine.
Ni muhimu kitabu chako Kiwe na namba hii kwa ajili ya kukifanya kitabu chako kitambuliwe kimataifa.
Kujifunza zaidi kuhusu uandishi wa vitabu na uchapishaji.
Karibu
SONGAMBELE CONSULTANTS✅ Tunakuandikia kitabu chako (ghostwriting)
✅ Tunatoa mwongozo wa kuandika kitabu chako
✅ Tunahariri vitabu
✅ Tunatoa usimamizi wa karibu kwenye uandishi wa kitabu chako
✅ Tuna vitabu bora vyenye hatua muhimu za kufuata katika uandishi
✅Uandishi wa makalaMawasiliano:
Simu/WhatsApp: +255 755 848 391
Email: jifunzeuandishi@gmail.comEneo: Morogoro mjini, Mafiga Tenki Bovu
Wasap:
-
Njia Bora Ya Kuanza Uwekezaji Kwenye Hisa

☝🏿Ndiyo, tunapoelekea kuanza mwaka mpya 2025, hakikisha unauanza mwaka mpya kwa KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE
Kabla ya mwaka mpya kufika jifanyie favor kwa kupata nakala ya kitabu hiki Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE.
Ndani ya kurasa za kitabu hiki utajifunza bidhaa tatu ambazo kinapatikana kwenye SOKO letu la HISA.
Yaani, HISA zenyewe. Zinavyofanya kazi na namna ya kuanza KUWEKEZA kwa usahihi.
VIPANDE. Hapa utapata kujifunza kuhusu VIPANDE na mifuko yote ya UTT AMIS, na namna inavyofanya kazi.
HATIFUNGANI za serikali na za makampuni zote zimeelezwa pia.
Pata nakala ya kitabu chako Sasa.
Na ni rahisi sana kukipata.
Kitabu ni 25,000/- tu
Ebu bonyeza hapa chini
https://wa.me/message/5ICRGY7P6S4NE1
Kujipatia nakala Yako.
Kumbuka kitabu ni 25,000/- tu.
Nicheki Sasa hapa
https://wa.me/message/5ICRGY7P6S4NE1
-
Jinsi Kufanya Majukumu Mengi Kwa Wakati Mmoja Kunavyokupotezea muda badala ya kusevu muda
Rafiki yangu unaendeleaje,
Kuna wakati unajikuta una majukum mengi na hivyo kuona ufanye majukumu hata mawili kwa wakati Mmoja ukidhani kuwa utarahisisha kufanikisha majukumu Yako kwa wakati.
Hata hivyo nataka nikwambie kuwa kufanya Majukumu Mengi Kwa Wakati Mmoja kunakupotezea muda mwingi. Kazi ambayo ungeifanya kwa muda mfupi unajikuta unaifanya kwa muda mrefu.
Ngoja nikupe mfano mzuri.
Ebu Sasa hivi andika sentensi
Kufanya Majukumu mawili kwa wakati mmoja ni kupoteza muda
Umetumia sekunde ngapi Kuandika hiyo sentensi?
Chini yake andika sentensi nyingine pia. Andika hivi;
Sasa nimeelewa
Umetumia sekunde ngapi Kuiandika na hiyo?
Sasa nataka hizi sentensi mbili uziandike kwa wakati mmoja.
Yaani uandike,
Kufanya Majukumu mawili kwa wakati mmoja ni kupoteza muda
Na
Sasa nimeelewa kwa wakati mmoja
Andika herufi Moja Moja ya kila sentensi kwa kubadilishana.
Anza sentensi ya kwanza kwa Kuandika
K
Na kwenye sentensi ya pili andika
S
Endelea kuandika herufi Moja Moja kwa kila sentensi kwa kubadilishana mpaka kila sentensi ikamilike. Utagundua kwamba umetumia muda mwingi kwenye kuandika pale unapokuwa unaandika sentensi mbili kwa wakati mmoja. Unaweza kutumia muda mpaka mara kumi zaidi ya muda wa kawaida
Kumbe ujumbe tunaoondoka nao Leo ni kwamba tusifanye majukum mengi kwa Wakati Mmoja, badala yake tujikite kwenye jukumu Moja kwa wakati, tulikamilishe kabla ya kwenda kwenye jukumu jingine.
Imeandikwa na
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro Tanzania
-
-
Umuhimu wa Uakifishaji
Uakifishaji ni uwekaji wa alama za uandishi kama vile nukta, mkato, mshangao, kiulizo, funga semi na fungua semi pamoja alama nyingine nyingi ambazo kimsingi, ndiyo nguzo ya uandishi wa aina yoyote ile.
Leo ninazungumza na ndugu zangu waandishi wa vitabu. Ni ukweli usiyopingika kwamba, hakuna namna unaweza kujiita mwandishi kama hujui matumizi sahihi ya alama hizi.
Unaweza ukasoma kitabu cha mtu mpaka ukahisi kuchanganyikiwa kwa sababu, aya nzima yenye mistari zaidi ya mitano, hajaweka alama yoyote ya uandishi, yaani hata zile alama za kawaida kabisa ambazo huwezi kuzikwepa (nukta na mkato), hazipo. Ameandika tu kiasi kwamba ukisoma, unasikia kama unapigiwa kelele masikioni. Hili ni kosa katika uandishi, badilikeni.
Ndugu zangu waandishi, ninajua mnajua umuhimu wa alama hizi, ninachokifanya hapa ni kuwakumbusha tu ili tuzibe panapovuja na jumbe zetu ziifikie jamii kama ilivyokusudiwa.
Ni vyema ieleweke kwamba, ukiukaji wa matumizi ya alama za uandishi, unaweza kupotosha ujumbe mzima na hadhira unayoiandikia ikapokea kitu kingine kabisa ambacho ni tofauti na matakwa yako.
Kwa mfano, unataka utoe taarifa kuhusu ujio wa Juma halafu wewe unaandika hivi…
Baba Juma amekuja
Unadhani kwa uandishi huo, hiyo taarifa itafika kama ilivyokusudiwa! Kimsingi sentensi hiyo ilitakiwa iandikwe hivi…
Baba, Juma amekuja.
Sentensi tajwa hapo juu, zina maana tofauti kabisa ingawa maneno yaliyotumika yanafanana. Sentensi ya kwanza inatoa taarifa kuhusu ujio wa baba yake Juma na sentensi ya pili, ndiyo inayotoa inayotoa taarifa kuhusu ujio wa Juma. Kitendo cha kuacha kuiweka alama ya mkato kwenye neno baba katika sentensi ya kwanza, kimepotosha taarifa mzima ambayo mwandishi alikusudia kuitoa.
Sasa unaweza kuona namna ambavyo maudhui ya kitabu chako, yanavyoweza kupotoshwa kama usipozitumia kwa usahihi alama za uandishi.
Ukitaka upate matokeo bora katika kazi yako, lazima ufanye kilicho bora.
Hivyo, tujitahidi kuzingatia matumizi ya alama hizi ili kazi zetu ziwe bora na si bora kazi.
Asante kwa kufuatilia makala zetu za uandishi, tukutane wakati mwingine.
Jina langu ni
Magdalena Donacian Kamambi
Mhariri
-
Zingatia kitu hiki kimoja kama unataka kufanya makubwa
Habari ya asubuhi kila mmoja, Leo ni siku nyingine muhimu ya Mimi na wewe kwenda kupambania MALENGO ND ndoto kubwa tulizonazo.
Leo nataka nikwambie kitu kimoja muhimu sana ambacho unapaswa kujifahamu
Unapaswa kujua ni muda Gani kwenye simu huwa unakuwa na uzalishaji mkubwa, na unapaswa kuulinda huo muda kwa NGUVU zako zote.
Siyo kila muda unakuwa na uzalishaji mkubwa.
Ila Kuna muda ambao huwa unakuwa na uzalishaji mkubwa kuliko mwingine.
Ulinde sana huo muda ili uweze kufanya makubwa zaidi.
-
KITABU: Watu 60 Walioshindwa Karibia Katika Kila Kitu Lakini Bado Wakashinda Kwa Kishindo
Rafiki yangu, nimezindua kitabu kipya. Kitabu hiki kinaitwa watu 60 walioshindwa karibia katika kila kitu walichofanya. Lakini hawa watu watu hawakukata tamaa, wala hawakurudi nyuma. Kila walipokutana na kikwazo, kwao huo haukuwa mwanzo wa kukata tamaa wala kurudi nyuma, bali ulikuwa ni mwanzo wa wao kuongeza juhudi zaidi, kupambana zaidi ili waweze kufikia malengo na ndoto zao kubwa.
Kitabu hiki kinakupa njia walizotumia hawa, ambazo na wewe unaweza kuzitumia pia kufanya makubwa.
Kitabu hiki pia kinakutia moyo. kwamba japo unakutana na vikwazo na changamoto nyingi kwenye maisha yako. Lakini usikate tamaa. Endelea kupambana, bila kukwamishwa na mtu au kitu chochote MPAKA KIELEWEKE.
Hakikisha unapata nakala yako mapema rafiki yangu. Kupata nakala yako ni rahisi sana. WASILIANA NAMI KWA 0684408755. utapokea nakala yako popote ulipo duniani.
-
Unataka Kwenda Mbinguni Kuishi Milele Ili Ufanye Nini? Una Uhakika Utautumia umilele wako Vizuri?
Unakuta mtu hajui ni kitu Gani anapaswa kufanya hapa duniani.
Lakini Bado anang’ang’ania kuwa anataka kwenda mbinguni. Huko mbinguni unataka kwenda kufanya Nini kama ya duniani yamekushinda.
Imeandikwa kuwa usipokuwa mwaminifu kwenye mambo madogo hutakuwa mwaminifu kwenye MAKUBWA. Kama usipokuwa mwaminifu kwa muda mchache wa hapa duniani. Unamwaminishaje Mungu kuwa mbinguni utautumia vyema ?
Kama tu maisha ya miaka michache ya hapa duniani yamekushinda, Sasa hayo maisha ya Kuishi MILELE utayaweza wewe? Huendi kuwa chokoraa huko mbinguni🤔
Ama kweli ukistaabu ya Musa, utayaona ya Filauni.