-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-97 tatizo unaogopa vitu vitakavyokufanya ukue
Kuna vitu vingi sana ambavyo vimekuzunguka na vipo kwa ajili yakukufanya wewe ukue.Watu waliokuzunguka wapo kwa ajili ya kukufanya wewe ukue, japokuwa wanaweza kuwa wanafanya kitu ambacho wewe hupendezwi nacho.Acha waendelee kufanya kile wanachopaswa kufanya. Wakati wewe ukiendelea na shughuli zako. Inawezekana wana kitu ndani yao wanafanya ambacho wanafanya japo hakikupendezi, ila ni kitu bora…
-
Hizi Ni Kurasa Za Vitabu Unazoweza Kuandika Mwaka 2018
Mwishoni mwa mwaka 2018 Rafiki zangu wengi sana walikuwa wakinitumia jumbe mbali mbali za kuuaga mwaka, na kuukaribisha mwaka. Wengine walinitumia jumbe za shukrani, wengine jumbe za kuukaribisha mwaka, wengine jumbe za kuuaga mwaka kutaja ila machache. Jumbe zote hizi kwangu zilikuwa zina maana kubwa sana. Moja kati ya ujumbe ambao ulinifanya nione kwamba maisha…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-96 hujaondoa vitu ambavyo sio wewe
Kuna vitu vingi sana ambavyo unafanya ila sio sehemu ya maisha yako na vinapokupeleka sio kule unapopaswa kwenda. Kama utaendelea kuvibeba 2018 basi jua kwamba utakwama, utakwama, utakwama sana. Yaani kuna hatari ya kupita tu 2018. Je, unavijua vitu ambavyo si wewe? Je, unajua vitu gani ambavyo haupaswi kutembe navyo 2018? Hii hapa ni orodha…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-95 tatizo unasubiri mwaka mpya
! Habari ya siku ya leo rafiki yangu! Leo ni tarehe mosi januari 2018! Hongera sana kwa siku hii njema sana ya leo! Lakini swali langu kwako kitu gani kimebadilika leo!Nikiangalia nje ya nyumba sasa hivi naona mwanga wa jua kama ilivyokuwa jana. Ninaona ndege wakiruka, lakini hata jana walifanya hivyo. Miti naiona ikimeremeta, ingawa…
-
NAAM! KIPENGA KIMEPULIZWA 2023!
Duniani hapa kumeshuhudiwa mitanange mingi sana ya mpira tangu dunia imekuwepo mpaka leo hii unaposoma makala haya. Mitanange hii si ya mipira ya ligi kuu ya vodacom au ligi kuu ya ulaya tu bali pia kuna mitanange ya michezo mingine ya maisha. Kuna mechi ambazo huwa zikichezwa, kwa hakika huwa zinavutia sana. Sio tu kwamba…
-
Mafunzo Matatu Kutoka Kwa Viwavi
Mwanasayansi wa kifaransa John Henry Fabre alifanya jaribio kwa kutumia viwavi. Alichukua viwavi akaweka kwenye sahani, huku kiwavi mmoja akiwa amemgusa kiwavi mwingine. Viwavi hawa wakawa wametengeneza mzunguko kamili. Akachukua chakula pendwa cha viwavi na kukiweka katikati yao, ikiwa ni sentimeta chache sana kutoka pale walipokuwa. Wale viwavi walianza kuzunguka kwa kufuatana, kiwavi mmoja akimfuata…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-85 Tatizo hujua umuhimu wa vitu vinavyoonekana vibaya
Kuna vitu ambavyo kwa kuviangalia katika maisha huwa vinaonekana vibaya ila kiukweli ndani yake hazina kubwa sana. Kwa kuuangalia udongo hakuna ambaye anaweza kusema kwamba udogo unaweza kutoa mti wenye matunda matamu sana. Maana unakuta udongo ni mchafu sana kiasi kwamba kama wewe ni mtanashati huwezi hata kupenda mtu yeyote Yule akugusishe udongo huo. Lakini…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA -81 tatizo haujawa mwekezaji
. Hivi ushawahi kujiuliza ni kitu gani kampuni inahitaji ili kukua?Kama hujawahi kujiuliza swali kama hili hapa, ebu kaa chini na ujaribu kujiuliza swali hili hapa muhimu sana. Utagundua kwamba ili ukue unahitaji kuwa na watu. Ni watu ndio ambao wanakubeba. Ni watu wenye uwezo wa kukusimamisha. Ni watu wenye uwezo wa kukuangusha. Je, unajua…
-
Hivi Ndivyo Vitu Vitatu (03) Ambavyo Watu Hudharau Sana.
Kuna vitu ambavyo huwa vinapendwa sana na watu wengi sana. Huku kukiwa na vingine havipendwi na kudharauliwa. Mfano unakuta vijana wengi sana wanapenda kuangalia mpira na kuhukumu wachezaji ambao wao (vijana) wanasema hawachezi vizuri japokuwa wao hawataki kuingia uwanjani kucheza. Na pengine mwingine ukimwambia aingie uwanjani acheze atakwambia mimi muda Wangu wa kucheza tayari umepita…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA -80 Tatizo unafukuza swala wawili
Kuna msemo wa Kiswahili ambao unasema kwamba “mshika mbili moja humponyoka”. Bila shaka wahenga waliosema maneno haya walikuwa wanawalenga watu ambao katika maisha yao wanalenga sehemu kubwa sana za kimafanikio lakini bado hata yale mambo ammbayo yanawatoa kwenye mafanikio bado wanayataka. Watu ambao wanapenda kuwa na maisha makubwa sana kiuchumi, kijamii na kimahusiano lakini bado…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZLIZOPOTEA-79 tatizo hujataka kuwa Thomaso
Moja kati ya watu ambao huwa wanazungumziwa sana kwa kutokana na kupenda kuhakikisha na kuuliza kwao ni Thomaso. Thomaso ninayemzungumzia hapa ni yule aliyeelezwa kwenye Kitabu cha Yohana 20:19-29 Imeandikwa hivi katika biblia “ikawa jioni siku ile ya kwanza ya juma pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya wahahudi, akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia,…
-
Kifanye Kwa Ubora Zaidi
Kila siku inapoanza tunaenda kujishughulisha na kazi au shughuli fulani. Hii ndio kusema kwamba kila mtu walau kwa siku kuna shughuli fulani ambayo yeye lazima aifanye. Hata kama ni ndogo kiasi gami lakini lazima ifanyike. Kinachotokea watu wengi wanajaribu kufanya kazi badala ya kufanya kazi haswa. Matokeo yake ni kwamba kazi nyingi sana ambazo watu…
-
Maajabu ya kitabu cha barabara ya mafanikio.
Kitabu cha barabara ya mafanikio kinazidi kupamba moto na kuwafikia watu wengi zaidi. Huku kila mtu ambayo anakisoma anakuja na ushuhuda wake. Kila mtu anasema ni kwa jinsi gani Kitabu kile hakimwacha jinsi alivyo. Kama hawa wamesoma na kunufaika wewe umesubiri nini? Jipatie na wewe hapo nakala ya Kitabu hiki cha karne hii ya 21.…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA- 78 tatizo unahairisha kuishi
Watu wengi sana wanahairisha kuishi kila kunapokucha. Anasema kwamba atafanya kazi fulani kesho. Ataishi maisha fulani kesho,Ataanza kula vizuri kesho akipata kazi nzuri.Ataanza kuongea na watu vizuri kesho….orodha ya namna hii ni kubwa kiasi kwamba siwezi kuimaliza hapa. Je, na wewe mmoja wapo?Kwanza kabisa naomba tufahamu kwamba kesho sio siku.(Rweyongeza, 2017)Pili tunapaswa kufahamu kwamba muda…
-
Hatua Sita Za Kujenga Maisha Ya Kuigwa.
Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa Makala kutoka katika blogu hii ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kuweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba umeweza kufikia mafanikio makubwa sana. Ndani ya siku hii ya leo tujifunze hatua sita ambazo zitatufanya sisi tuishi maisha…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-70 Tatizo ni hujaandika kile unachotegemea kutoka kwa watu
Je, ni mara ngapi umeaachia watu kazi na unakuta kwamba ile kazi uliyokuwa umewaachia hawajaifanya? Je, ni mara ngapi kazi ambayo ulikuwa unategemea kuwa imefanyika umekuta hijafanyika? Je, unajua kwa nini? Bila shaka hapa utaniambia kwamba watu ambao nawaaambia huwa hawanisikilizi. Badala yake wao huwa wanawafanya kazi zao ambazo wanapenda kufanya. Ngoja nikwambie kitu cha…
-
TATIZO SI RASILIMALLI ZILIZOPOTEA-68 Tatizo hujajua kwamba hujuii kila kitu
Katika zama hizi kuna taarifa nyingi sana. Taarifa hizi zinatujia kwa njia tofauti tofauti sana katika maisha yetu. Taarifa hizi zinzaweza kukujia kupitia kwa watu ambao wamekuzunguka. Vitu unavvyokutana navyo, vikwazo vinavyokuzuia na vingine vingi. Hata hivyo kama hujajipanga kuzitafuta taarifa hizi hapa huwezi kuzipata. Hii ndio kusema kwamba kama bado hujakubali kwamba hujui ili…
-
USIOGOPE KUSHINDWA
Kushindwa ni moja ya jambo ambalo lipo katika njia ya kuelekea katika mfanikio. Bila shaka utakuwa umesikia mara nyingi sana maneno kama wewe ni mshindi, umezaliwa mshindi, na maneno mengine mengi sana. Haya maneno yapo sahihi kwa asilimia kubwa sana. Ila mbali na kwamba kweli wewe umezaliwa mshindi na umezaliwa kushinda bado katika njia…
-
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-68 Tatizo hujawatumia watu wengine
Watu walio pembeni mwako kuna kitu kizuri sana ambacho wanakiona kwako ambacho wewe hapo huwezi kukiona. Kama utaweza kukijua vizuri kitu hiki kutoka kwa watu wengine basi utaweza kufaidika kwa hali ya juu sana. Hivi ushawahi kugundua kwamba mtoto mdogo sana akiwa ana kitu ambacho anataka kufanya anakuja kwa mzazi kuomba msaaada. Mfano mtoto atakuja…
-
Watafute Watu
Miongoni mwa vitu ambavyo unavihitaji sana maishani mwako ili kufanikiwa na kuhakikisha kwamba unapiga hatua kubwa sana ni watu. Unahitaji watu ili uweze kufanya biashara zako. Unawahitaji watu ili uweze kuwa kiongozi. Maana kipimo bora cha kwamba wewe ni kiongozi bora kitaonesha majibu pale patakapokuwa na watu. Unahitaji watu ili ukae darasani na kusoma. Hawa…