-
Aina za mazoezi Unayopaswa kuwa unafanya
Mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kuna aina tatu ya mazoezi ambayo unapaswa kufanya kila siku, unajua ni aina zipi?
Mazoezi ya mwili. Kama kukimbia, Kwa siku tenga walau musu saa Kwa ajili ya hili
Mazoezi ya akili. Haya niazoezi unayafanyia Kwa kujifunza, KUSOMA VITABU na kupata mafunzo ya semina n.k
Mazoezi ya kiroho. Haya unayafanyia Kwa kupata muda wa jahajudi salaam n.k
Inashautiwa walau kuwa na dakika 20 Kwa ajili ya Kila kimoja Kila siku
Hizi ni aina za mazoezi ambazo unapaswa kuwa unafanya mara zote.
Wewe unafanya zipi Kwa Sasa, na Nini mpango wako?Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
Jinsi Ya Kujilipa Mshahara Kutoka Kwenye Biashara Yako. Njia Mbili Zilizothibitishwa
Changamoto kubwa ambayo imekuwa inawakumba wafanyabiashara wengi ni kuchanganya pesa zao na pesa za biashara. Makala ya leo, inaenda kuwa mwarobaini wa hili.
Sikiliza uhusiano mkubwa uliopo kati yako wewe na biashara yako ni kwamba wewe ni mmiliki wa biashara, lakini fedha za biashara haupaswi kujimilikisha na kuzifanya kuwa za kwako. Fedha za biashara ni za biashara. wewe unapaswa kupata pesa kutoka kwenye biashara yako kwa njia mbili tu.
Njia ya kwanza ni kama mshahara, wewe kama mfanyakazi kwenye biashara yako basi unastahili kupata mshahara. na njia ya pili ya wewe kupata pesa kutoka kwenye biashara yako ni gawio au faida.
Nje na hapo fedha ya biashara ni ya biashara na fedha ya kwako ni ya kwako.
lakini si tunaanzisha biashara ili tupate fedha?
Najua unajiambia hivyo, ndio. ni kweli. ila sikiliza. Biashara yako ni kama kiumbe hai, inahitaji kula, inahitaji kupumua na inahitaji kukua. Endapo haitapata vitu muhimu kwa ajili ya biashara yako kukua, ukweli ni kwamba biashara hii haitakua.
Hivyo, usiibemende biashara yako kwa kuchukua hela za biashara ya kujimilikisha. Ziache fedha za biashara ziendelee kuwa za biashara
Tena biashara inapaswa kuwa na akaunti yake benki. Na wewe unapaswa kuwa na akaunti yako pia.
Hela yako ikae kwenye akaunti, na helaya biashara iwe kwenye akaunti yake. Usizichanganye.
Hapa najua unajiuliza mbona lakini muda mwingine huwa naongeza hela kwenye biashara, hili nalo limekaaje?
Ndiyo, kama unaongeza hela kwenye biashara maana yake kuna kitu umeona kwamba kikipata nguvu utakuja kupata faida zaidi hapo baadaye. Kama kwa sasa faida ulikuwa unapata milioni kwa wiki, maana yake unatazamia utapata milioni na nusu. Kitendo cha wewe kuongeza fedha kwenye biashara hakikupi wewe uhuru wowote wa kuifanya hela ya biashara kuwa ya kwako.
Najua unajiuliza swali jingine, kuwa je, kwa mfano, nikipata shida wakati hela ya biashara ipo nifanyeje?
Jibu langu ni kwamba, ukipata shida, tumia mshahara wako. Kama mshahara unaupata kutoka kwenye biashara yako haukutoshi, ongeza bidii ili mshahara huo uweze kupanda.
Ninaposema ongeza bidii maana yake, weka mkazo kwenye mauzo,ili uweze kuuza zaidi na hatimaye uweze kupata mshahara mkubwa zaidi kutoka kwenye biashara yako.
Sasa swali jingine unalojiuliza, ni je, nijilipe shilingi ngapi kutoka kwenye biashara yangu?
Jibu lake ni kwamba, kuna aina mbili za malipo ambayo unaweza kupata kutoka kwenye biashara yako.
Aina ya kwanza ni malipo ya mshahara ambao uko fixed. Yaani, unajiwekea kiwango maalumu cha mshahara ambacho utakuwa unapokea kila wiki au kila mwezi.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba unakuwa na kiwango ambacho kitakuwezesha kukidhi mahitaji yako ya kila siku, ili usije ukajikuta umechukua hela ya biashara katikati ya wiki au mwezi.
aina ya pili ya kujilipa kwenye biashara, ni kwa kamisheni.
Hii ni njia nzuri kama utakuwa tayari kupambana na kuweka kazi zaidi. Hii itakupa changamoto ya kuisukuma biashara yako iende viwango vya juu mara zote. kama upo tayari kwa ajili ya hii changamoto, basi hii ndiyo njia bora kwako ambayo itakufaa kujilipa.
Kwa njia hii ni kwamba, unaweka kiwango cha mshahara wako kuwa asilimia ya mauzo unayokuw aumefanya. mfano unaweza kuweka asilimia tano au kumi. Hii inamaanisha kwamba kwa kila mauzo utakayofanya, utapata asilimia tano tu. Mfano ukifanya mauzo ya milioni moja, unapata kamisheni yako ya ya asilimia tano ambayo ni sawa na shilingi elfu hamsini. Ukijisukuma zaidi, maana yake utapata kamisheni kubwa zaidi na hivyo kuwa na mshahara zaidi.
najilipaje hiyo hela nachukua tu pale ninapopaswa kuchukua au inakuwaje yani?
Utaratibu wa kujilipa jilipe kama ambavyo ungekuwa unawalipwa wafanyakazi wengine. Jilipe hela kupitia akaunti ya benki. Toa kwenye akaunti ya benki kwenda akwenye akaunti yako, na matumizi yawe ni mshahara au kamisheni.
Una swali la ziada kuhusu hii mada ya leo. Kama lipo inawezekana swali lako limejibiwa kwenye kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Hakikisha umepata kitabu hiki kizuri sana kwa kuwasiliana na +255 684 408 755. Fanya hivyo sasa hivi ili uweze kupata nakala yako,

Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755 La sivyo, mimi nakushukuru sana kwa muda wako siku ya leo. HAKIKISHA UMEJIUNGA NA WATU WANAOPOKEA MAKALA MAALUM KUTOKA KWANGU kila siku. Kujiunga, jaza taarifa zako hapa chini
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
Kanuni Ya Miezi Sita Kwenye Biashara, Na Kwa Nini Kila MfanyaBiashara Anapaswa Kuifahamu
Kuna kanuni ya miezi sita kwenye biashara ambayo wafanyabiashara wengi hawaifahamu. Ni kanuni muhimu ambayo kama mfanyabiashara unapaswa kuifahamu. Kutoifahamu kanuni hii kutakuponza sana
Kanuni hii inasema kwamba, ukianza kufanya biashara, ndani ya miezi sita ya kuanza biashara kuna watu wengine wataanzisha biashara kama hiyo.
HII kanuni inafahamika kama kanuni ya copy cat.
ikimaanisha kwamba baada ya miezi sita kuna watu watakuwa wanafnaya biashara kama ya kwako uliyoanza kufanya baada ya miezi sita.
Kuna watu watazalisha bidhaa kama hizo miezi sita baada ya wewe kuwa umeanza kufanya uzalishaji.
Kwa hiyo hakuna kitu unachofanya kwenye biashara yako ambacho kipo salama ambacho watu hawatakuja kukifanya.
sasa ili kujiweka katika mazingira ambayo watu hawataweza kukutoa kwenye biashara unapaswa kuzingatia mambo sita yafuayo
- Ni ubunifu. Yaani mara zote kuwa mbunifu kwenye kila kitu unachofanya. kuwa mbunifu kiasi kwamba watu wengine wawe mara zote wanatafuta namna ya kuweza kuendana na kile unachofanya na kile unachobuni.
- Jifunze kila mara. kuwa mtu wa kujifunza mara zote, wengi watakuwa wanaiga kwako ila siyo watu wa kujifunza. wewe kuwa mtu kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu, majarida yanayoelimisha na kuhududhuria semina na mfunzo muhimu sana.
- kuwa na mfumo ambao wengine hawawezi kuufanyia kazi. Inawezekana ni mfumo wa namna ya kuhudumia wateja kwa namna ya kipekee. Au inawezekana ni mfumo wa kuwa na wafanyakazi ambao ni bora kabisa kwenye biasahra yako. Hakikisha unakuwa na kitu ambacho hakuna mtu mwingine mwenye nacho na kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana bila ya kuacha hata kidogo.
- Kuwa mtu wa kupokea maoni kutoka kwa wateja wako. Kwa kuanzia nashauri, upokee hasa maoni kutoka kwa wateja wako. Hawa ni watu ambao wametumia bidhaa zako na hivyo wakikwambia kitu, ni uhakika kwamba wanakuwa wanamaanisha hicho wanachokisema.
- Hata hivyo, ukipokea maoni kutoka kwa wale watu ambao hata hawajatumia bidhaa zako maana yake ni kwamba utakuwa unapokea maoni kutoka kwa watu ambao hawajapata uhondo wa kile ambacho umetengeneza. na inawezekana wasije hata siku moja kununua kutoka kwako.
- Amua kufanya kitu ambacho utafahamika nacho kwacho. Ndiyo, najua kuna vitu ambavyo unaweza kufanya, lakini kwa kuanzia fanya kitu ambacho utafahamika nacho kwacho. Kifanye kwa ubora mkubwa sana
rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matano ya msingi sana ambayo unapaswa kufanya, ambayo yatakufanya uwe mbele ya watu wengine mara zote. Badala ya mara zote kuendelea kuwa unaiga kwa wengine. Yatakufanya kuwa mbunifu mara zote na kuja na vitu vya tofauti.

Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755 SOMA ZAIDI: Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati wa Kuanzisha Biashara
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
Viashiria kumi na sita (16) Kuwa Umebeba Ajira Za Watu
Rafiki yangu mpendwa salaam, ujue mara kwa mara nimekuwa nakwambia kwamba inawezekana wewe umezaliwa kuajiri na siyo kuajiriwa. Siku ya leo ninaenda kukuonesha viashiria ishirini ambavyo vinaonesha kuwa wewe umebeba ajira za watu.
Baada ya kuwa umesoma hapa sasa, kazi itabaki kwako kuhakikisha umefanyia kazi haya utakayokuwa umejifunza au la
1. Kiashiria cha kwanza kwamba umebea ajira za ni ndoto yako kubwa
Kama una malengo na ndoto kubwa, fahamu wazi kuwa haya malengo na hizi ndoto kubwa unaweza kuzikuza mpaka kufikia hatua ambapo watu watahitajika ili kukusaidia ili kuzifanikisha. Ni ukweli kuwa hakuna ndoto kubwa ambayo unaweza kuifanikisha peke yako. Ndoto kubwa zinahitaji watu pia. Hivyo, kama una ndoto kubwa hakikisha unazifanyia kazi maana hizi ndizo zitakupelekea wewe kwenye kuajiri wengine.
2. kiashiria cha pili kuwa umebeba ajira za ni kipaji chako
Kiashiria cha pili kuwa umebeba ajira ni kipaji chako. Kama una kipaji ni wazi kuwa hiki kipaji, huwezi kukifanyia kazi peke yako. Unahitaji watu kufanyia kazi kipaji chako na kukifanikisha. Hiki ni kiashiria kingine kuwa inawezekana umebeba ajira za watu.
3. kiashiria cha tatu kuwa umebeba ajira za watu hicho kitu unachopenda kufanya
Kama kuna kitu unachofanya na unaona kwamba unapenda kukifanya hicho kitu, hiki ni kiashiria kingine tosha kwamba inawezekana wewe umebeba ajira za watu. Kwenye hili unaweza kuwa unajiuliza, kivipi? Ngoja nikuelekeze vizuri ili uweze kunielewa. kama unafanya unachopenda maana yake kinaeanda kuwagusa watu wengi. Itafikia hatu ambapo utakuwa na majukumu mengi ambayo utakuwa unapaswa kuyafanyia kazi. Baadhi ya haya majukumu sasa watahitajika watu wa kuyafanya na kuyatekeleza. Na hapo ndipo utakapoajiri!
3. kiashiria cha nne kuwa umebebea ajira za ni changamoto ambazo zinaikumba jamii
Kama kuna changamoto ambazo unaziona kwenye jamii na unaona unaweza kuzitatua, hicho ni kiashiria kwamba umebeba ajira za watu. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua na kutatua hizo changamoto unazoona. na hapa siyo tu kwamba unakuwa umebeba ajira za watu, lakini pia unakuwa umebeba suluhisho la matatizo na changamoto kubwa zinazowakumba watu.
4. Kiashiria cha tano kuwa umebeba ajira za watu ni ushauri ambao watu huwa wanakuja kukuomba
Kama kuna watu wanakuja kwako kukuomba ushauri kwenye jambo fulani, fahamu wazi kuwa umebeba ajira zao. Unachotakiw kufanya ni kuhakikisha kwamba unaweka vizuri kile unachojua, ili kiweze kuwasaidia watu katika ngazi kubwa na katika viwango vikubwa. Nimeeleza hili kwa undani zaidi kwenye kitabu cha TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA.
Unaweza kupata nakala ya hiki kitabu mtandaoni moja kwa moja kupitia HAPA au kwa kuwasiliana nami kwa +255 684 408 755
SOMA ZAIDI: KITABU: TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA
5. Kiashiria cha Tano ni kuwa na Uwezo wa Kujenga Timu:
Kujenga na kuongoza timu ni sifa muhimu kwa wale wanaotaka kuwaajiri wengine. Watu wenye uwezo wa kufanya kazi na kusimamia wafanyakazi wanaweza kufanikiwa katika kuendesha biashara na kutoa ajira. Hii inamaanisha kwamba kama una uwezo mzuri wa kuwasiliana na kuwasilisha kile ambacho kimoo ndani yako kwa timu yako, kutoa majukumu yanayoeleweka kwa timu yako, kuwa na namna ya kuifuatilia timu yako na kuifanyia tathmini ili iweze kuzalisha matokeo n.k.
6. Kiashiria cha Sita ni Kuwa na Ujasiri wa Kuchukua Hatari:
Kuna hatua nyingi za hatari ambazo utapaswa kuchukua kwenye maisha yako ya kila siku.kama hiili unaona liko sawa kwako, basi huu ni muda wako wa kujiandaa kuja kuajiri siku moja.
SOMA ZAIDI: Haya Ndio Maneno Yanayotumiwa Na Watu Kujifariji Linapokuja Suala La Pesa
7. Kiashiria cha saba ni uwezo wa Kusimamia Rasilimali:
Hili somo wengi linawapiga chenga. Kusimamia rasilimali kama vile fedha, wafanyakazi, na vifaa ni muhimu katika uendeshaji wa biashara. Watu wenye uwezo wa kusimamia rasilimali hizi wanaweza kuwa na uwezo wa kuajiri na kusimamia wafanyakazi.
8. Kiashiria cha nane ni Kuwa na Mtazamo wa Muda Mrefu:
Biashara siyo kitu cha kufanya ndani ya siku moja. ni kitu cha muda mrefu, hivyo mtazamo wa muda mrefu ni kitu cha muhimu sana hasa tunapoongea biashara.
Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)
9. Kiashiria cha Tisa ni Uwezo wa Kuhamasisha Wengine:
Hiki ni kipengele kingine muhimu sana hasa unapokuwa unafanya kazi na watu. Kuna wakati ambapo utapaswa kuwa mkali, n akuna wakati ambapo utahitaji kuwahamasisha wengine kazi ifanyike. Kuna wakati watu watatakiwa kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya ule muda wa kawaida. haya yote utaweza kuyafanikisha kama utakuwa mtu wa kuhamasisha watu na kuwafanya waone maono makubwa ambayo wewe mwenyewe utakuwa unaona.
10. Kiashiria cha kumi ni kuwa na Uwezo wa Kufanya Maamuzi ya Haraka:
Katika biashara, mara nyingi kuna haja ya kufanya maamuzi haraka ili kukabiliana na mabadiliko ya haraka katika soko au mazingira ya biashara. Watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na kwa ufasaha wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi. na ukweli ni kuwa zipo nyakati nyingi ambazo utatakiwa kufanya maamuzi ya haraka. Ni nyingi zipo mbele yako. Kitu kikubwa unachopaswa kuwa tayari kuzikabili.
SOMA ZAIDI: Mambo Matano Unayopaswa Kufahamu Ili Utengeneze Marafiki Wazuri Na Wa kudumu
11. Kiashiria cha kumi na moja ni kuwa na Uwezo wa Kujifunza na Kubadilika:
Biashara mara nyingi inahusisha kujifunza kutokana na makosa na kubadilika kulingana na mabadiliko katika mazingira ya biashara. Watu wenye uwezo wa kujifunza na kubadilika wanaweza kufanikiwa katika kuendesha biashara na kutoa ajira kwa wengine.
Miaka ya nyuma mtandao wa intaneti ulipoingia mjini ni biashara chache zilikuwa tayari kubadilika na kuukumbatia huu mtandao wa intaneti, leo hii hizi biashara biashara zimeweza kukua sana. Kwa upande mwingine kuna biashar aambazo zilipuuza hii mitandao, nyingine zimetoweka kwenye biashara na nyingine sasa hivi ndio zinajikongoja kuingia kwenye hii mitandao. Ukweli ni kuwa kama mfanyabiashara unapaswa kuwa tayari kujifunza kila maa bila ya kuacha.
Wakati mwingine kujifunza kitu kimoja tu mfano kwenye kitabu unaweza kuwa ni uamuzi wenye busara sana. Hivyo, ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba unajifunza na unabadilika pale inapohitajika.
12. Kiashiria cha kumi na mbili kuwa na Uwezo wa Kufanya Kazi Kwa Timu:
Wakati shuleni wengi tunafundishwa kufanya kila kitu peke yako. Kwenye biashara hali ni tofauti, uwezo wa kufanya kazi kwa timu na kushirikiana na wengine ni muhimu katika biashara. Kama una uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na kusaidiana na wenzao wanaweza kuwa na uwezo wa kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia timu yako.
12. Kiashiria cha kumi na mbili ni uwezo wa Kufanya Mawasiliano
Mawasiliano mazuri ni muhimu katika biashara na uongozi. Watu wenye uwezo wa kufanya mawasiliano mazuri na kusikiliza wengine wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi\
Njia Tano Za kuwa na Ukuaji Kwenye Maisha, Biashara na Kila kitu unachofanya
13. Kiashiria cha kumi na tatu ni kuwa na Maono ya Ubunifu:
Ubunifu ni muhimu katika kufanikiwa katika biashara. Watu wenye uwezo wa kuona njia mpya za kufanya mambo na kubuni suluhisho mpya wanaweza kuwa na uwezo wa kuajiri na kusimamia wafanyakazi. Kiukweli ubunifu ni m oyo wa biashara na biashara yoyote ambayo haina ubunifu ni suala la muda tu hiyo biashara itatoweka kwenye soko. Unahitaji ubunifu kwenye uzalishaji wa bidhaa, unahitaji ubunifu kwenye kufanya masoko, unahitaji ubunifu kwenye kuuza. Yaani, karibia kila kitu ni ubunifu.
SOMA ZAIDI: JINSI UBUNIFU UNAVYOWEZA KUKUINUA KWENYE BIASHARA
14. Kiashiria cha kumi na nne ni kuwa na Uwezo wa Kufanya Kazi Kwa Bidii:
Biashara mara nyingi inahitaji ufanye kazi kwa bidii. Muda mwingine inahitaji ufanye kazi muda mwingi zaidi ya kawaida, na hata muda mwingine ufanye kazi siku za sikukuu. Mfano Rweyongeza hapa nipo naandika makala hii ikiwa ni siku ya pasaka saa tano asubuhi, muda ambao najua wazi kuwa watu wengine wapo wanakula bata au wanapanga kwenda kula bata.
Jack Ma kuna siku aliwahi kusema kwamba wakati mwingine unahitaji kufanya kazi kwa takribani saa 16-18 kwa siku. Hii yote ni kwa ajili ya biashara yako. Kama unaona hizi gharama unaweza kuzilipa, inawezekana siku siyo nyingi utahitajika kuajiri na utakuwa boss kwenye biashara yako. Jiandae sasa.
SOMA ZAIDI: Gharama Sita Unazopaswa kulipa ili kufikia ndoto zako.
15. Kiashiria cha kumi na tano kufanya Maamuzi Yasiyoepukika
Mara nyingine katika biashara, kunahitaji kufanya maamuzi ambayo siyo rahisi na hata wewe mwenyewe yanakuogopesha. Kwa lugha nyigine, haya ni maamuzi magumu.
wakati mwingine unaweza kufanya maamuzi kama haya, ila yakawa siyo maamuzi maarufu, watu kwenye timu yako wakayapinga, kwa sababu hawaoni kule unapoona wewe. sasa unahitaji kuwa mtu wa kufanya maamuzi na kuyasimamia. Watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na kusimamia matokeo yake wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi.
SOMA ZAIDI: KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini
16. Kiashiria cha kumi na sita ni uwezo wa Kusimamia Muda:
kWENYE biashara muda ni kitu chenye thamani kubwa sana. Kama mfanyabiashara hauna muda wa kutosha wa kufanya kile kitu. Kama mfanyabiashar aunapaswa kuhakikish kwamba umewekeza muda wako na unautumia vyema kabisa bila ya kuupoteza.
Usimamizi wa muda ni muhimu katika biashara na uongozi. Watu wenye uwezo wa kusimamia muda wao na wa wafanyakazi wao vizuri wanaweza kufanikiwa kwenye biashara
SOMA ZAIDI: Wafanyabiashara Waliofanikiwa Wanavyotunza Muda
-
UTABIRI: Kitu Kimoja Ambacho Ni Uhakika Hakitatokea Maishani Mwako
Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendelea vyema kabisa na shughuli zako za kila siku.
Siku ya leo nimekuandalia makala ya kushangaza kidogo. Na makala hii ni utabiri.
Mimi syo mtu ninayeamini sana kwenye tabiri, unabii na vitu vinavyoendana na hili.
Ila leo nimevutwa kukupa utabiri huu, na ninatoa utabiri huu nikiwa na uhakika kuwa lazima huu utabiri utatokea kwenye maisha yako. Nina uhakika kabisa wa asilimia 100.
Utabiri wangu unasema kwamba huwezi kufikia malengo ambayo hujaweka. Rafiki yangu, tuwe tu wakweli, kama hujaweka malengo, kama hauna malengo ambayo unapaswa kufikia ni wazi kuwa huwezi kufikia malengo hayo.
Kiufupi ni kuwa huwezi kufikia malengo ya kitu ambacho wewe mwenyewe hauna.
Hivyo, njia bora ya wewe kufikia malengo yako ni kuanza kuweka hayo malengo sahihi kwanza.
Kisha kuanza kuyafanyia kazi.
Nje na hapo tusidanganyane, hutaweza kufanikisha na kufikia hayo malengo ambayo wewe mwenyewe hauna.
Hivyo, kazi yako kubwa ambayo unapaswa kuifanya siku ya leo ni kuhakikisha kwamba umeweka malengo. Weka malengo ambayo utaanza kuyafanyia kazi mara moja kuanzia leo hii.
Ni hivyo tu.
Uwe na siku njema sana rafiki yangu.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli.
SOMA ZAIDI: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
-
Iga Ufe
Kuna baadhi ya vitu huhitaji kuiga kwa watu wengine. Badala yake unapaswa kuvifanya kulingana na wewe mwenyewe.
Siyo kila kitu wanachofanya wengine kinaweza kukufaa na wewe pia. VIngine vinaweza kuwa sahihi kwao, lakini siyo sahihi kwako. Ni muhimu kwako kufahamu kipi ni sahihi kwako, na kuwekeza nguvu yako kubwa hapo.
Kuna watu wanakopa na mshahara wao unapoingia tu, wanakuwa haawana kitu ambacho kimebaki, wanaenda kulipa madeni na kuendelea kukopa zaidi. Hiki kitu kinaweza kuwa sahihi kwao, lakini siyo sahihi kwako. Iga ufe.
Kuna watu wakipokea fedha, wanafanya matumizi yote unayoyafahamu hapa duniani, halafu ndiyo wanasubiri kile kinachobaki waweke akiba. Hiki kitu kinaweza kuwa sahihi kwako, ila siyo kwako. Iga ufe.
Kuna watu hawana malengo wala ndoto zozote kubwa, wanaishi tu ilimradi maisha yameenda. Wanaishi kwa usemi kwamba kesho itajipa yenyewe, hawana haja ya kuihangaikia kesho. Hiki kitu kinaweza kuwa sahihi kwao, ila kwako. Iga ufe.
Fahamu yapi ni sahihi kwako kufanya. na wekeza muda wako kwenye hayo ambayo ni sahihi kwako kwa wakati huu. Achana na yale yote ambayo siyo sahihi.
soma zaidi
- Huu Ndio Mfumo Bora Utakaokuwezesha Wewe Kutimiza Malengo Yako. mfumo huu haujawahi kufeli hata kidogo
- Jinsi ya kupata matokeo ya tofauti mwaka 2024
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
KIPAJI NI DHAHABU: Ila hapa kuna vitu vitano ambavyo kila mwenye kipaji anapaswa kufahamu
Juzi kuna mtu alinifuata kikashani kwangu whatsap na kuniuliza, mbona kijana yule mwenye kipaji ameshindwa kusaidiwa?
Nilimwuliza kijana yupi? baadaye kidogo alinitumia picha za yule kijana pamoja na kazi alizofanya.
Nilitakafari hili kidogo, ila nikaja kugundua kwamba watu wenye vipaji kuna vitu vitabo muhimu ambavyo hawafahamu.
Ningependa na wewe ufahamu hivi vitu, kuanzia leo hii, nina uhakika vitakuwa vitu vyenye manufaa makubwa sana kwako.
- kipaji ni dhahabu, ila ni ukweli kuwa kipaji hakitageuka kuwa dhahabu bila ya wewe kukifanyia kazi
- Usitegemee kamba kipaji chako kitaanza kukulipa siku hiyohiyo. Kinachukua muda.
- Ikitokea kipaji chako hakijakulipa, usikate tamaa na kuacha kukifanyia kazi. Kumbuka kwamba kila kitu huwa kina majira yake.
- Ni muhimu sana kufahamu misingi sahihi ya kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako badala ya kuanza kusubiri watu waje wakufadhili, wakudhamini. Ukweli ni kuwa ukisubiri watu wa namna hii waje, unaweza kujikuta kwamba unakata tamaa na hata unashindwa kufanyia kazi kipaji chako kwa uhakika kabisa.
- inapotokea majibu uliyokuwa unategemea yaje haraka hayajatokea, usikate tamaa wala kuishia njiani. Endelea kupambania kipaji chako bila ya kurudi nyuma. Kipambanie mpaka kieleweke
hayo ni mambo matano tu ambayo nilitaka uyajue kuhusu kipaji siku ya leo.

Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa +255684408755 sasa Hakikisha umepata kitabu changu cha KIPAJI NI DHAHABU: Ni moja ya kitabu kizuri sana ambacho unapaswa kusoma. Kimeeleza kila kitu kuhusu kipaji na jinsi unavyoweza kutumia kipaji chako kwa manufaa.
Kupata nakala ya kitabu hiki hakikisha umewasiliana na 0684 408 755 sasa
SOMA ZAIDI:
-
Kipaji chako umekiweka wapi? Umeajiriwa, umejiajiri au huna ajira?

Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa Dhahabu ni madini yenye thamani sana hapa duniani. Siku ya leo tarehe 29/3/2024 wakati naandika hapa, imabidi niangalie mtandaoni ili kuona bei halisi ya dhahabu sasa hivi kwenye soko la dunia. Ninachoona hapa ni kwmaba bei ya dhahabu kwenye soko la dunia siku ya leo ni kati ya dola 70,000 na dola 75,000 kwa kilo moja
Hii ni thamani ya hiki kitu kinachoitwa DHAHABU.
Dhahabu, kabla haijawa na thamani kubwa hivyo, huwa inapitia kwenye hatua mbalimbali, mojawapo ya hatua hiyo huwa ni KUICHOMA KWA MOTO WA KIWANGO CHA JUU SANA. Moto huu unaiunguza, ndipo baadaye tunakuja kupata dhahabu.
Ila leo hiii sipo hapa kuongelea kuhusiana na biashar dhahabu, badala yake nipo hapa kuonge ana wewe kuhusiana na KIPAJI chako.
Nimekuwa nikiongea na watu na kuwasisitiza kwambna kipaji chao ni DHAHABU.
Naam, kipaji chako wewe….
Ni dhahabu. Ni kwamba kipaji hiki hakitageuka kuwa dhahabu kwa sababu umesoma hapa. Au kwa sababu umesiki amtu akisema hivyo. Ni mpaka uwe tayari kukifanyia kazi. Na wakati mwingine kwa kutokwa na jasho, damu na machozi ndipo uje kufikia wakati wa kuvuna mavuno mazuri.
Kumbuka kipaji chako ni dhahabu, ila dhahabu hii isipofanyiwa kazi haitakuja kuleta matokeo.
Hakikisha umepata nakala ya kitabu hiki hapa, cha KIPAJI NI DHAHABU, utajifunz amengi kutoka kwenye hikitabu kuhusiana na kipaji chako na jinsi unavyowez akukinoa kwa manufaa yako ya sasa na ya baadaye.
Imeandikwa na Godius Rweyongeza
SOMA ZAIDI: KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kukitumia Kipaji Chako Kwa Manufaa
-
Acha Uvivu, Fanya Jambo Hili Kila Siku Bila Ya Kuacha
Kufikiri ni jambo ambalo tunapaswa kulifanya kila siku. Wengi hudhani wanafikiri lakini kumbe siyo. Kufikiri ni kazi ambayo hatupaswi kuikwepa.
Inapaswa kuwa sehemu aya maisha yetu ya kila siku. Hakuna mtu ambaye anawez akufanya hiki kitu kwa ajili yako. Kuna vitu unaweza kuwapa watu na wakafanya hivyho vitu ila huwezi kuifanya wewe.
Jipe kazi ya kufikiri kila siku kwa kufuata utaratibu maalumu ambao nimeuleza kwenye makala hii Ufahamu Uovu wa Lazima Kwenye Maisha Yako
Ifuatilie hii makala, nina uhakika utajifunza mengi na utanishukuru kwa hicho.
MAPAKA WAKATI MWINGINE NIKUSHUKURU SANA KWA MUDA WAKO.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391
-
Nguvu Ya Mtazamo (Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni maskini vs Ninalipwa laki mbili ndiyo maana mimi ni tajiri)
Rafiki yangu, mtazamo ni moja ya kitu muhimu sana hasa linapokuja suala la mafanikio. Mtu afikirivyo ndivyo anavyokuwa.
Hivyo, kama unataka kufanikiwa, unapaswa kubadili mtazamo wako kutoka kuwa mtazamo hasi na kuw amtazamo chanya. Unapaswa kubadili mtazamo wako na kuanza kuona uchanya kwenye kile unachofanya.
Hali na matukio mbalimbali yanayotokea kwenye maisha yako, badala ya kuona katika namna ya uhasi, uone uchanya.
Tukichukua watu wawili, ambao wanaishi maisha sawa, ila wanatofautiana tu mtazamo. Hawa watu wawili, baada ya muda watakuja kuwa na maisha tofauti, huku mmoja akiwa amefanikiwa na mwingine akiwa na maisha yaleyale ya kulalamika.
Kwa nini,
Kwa sababu ya mtazamo.
Tuchukulie hawa watu wawili wanalipwa laki mbili kila mwezi. Mmoja akawa na mtazamo kwamba sitaweza kutengeneza utajiri kwa sababu tu ya kipato ambacho naingiza. Na mwingine akasema kwamba nitatengeneza utajiri kutokana na kipato ninachoingiza.
Unadhani ni nani atatengenenza utajiri? Ukweli ni kuwa, yule ambaye ana mtazamo chanya. Mtazamo wa kuona kwamba kile kiwango cha fedha alichonacho ni sehemu ya kuanzia. Huyu ndiye atakayetengeneza utajiri ukilinganisha na mtu ambaye ana mtazamo hasi.
Ujumbe muhimu ambao nataka uondoke nao siku ya leo ni kuhakikisha unakuw ana mtazamo chanya. Fikra chanya zitakupelekea mbali kuliko utakapokuwa na mtazamo hasi.
SOMA ZAIDI:
- Kauli Yenye Nguvu: Ni bora Ufe Ukiwa unafanya unachopenda…
- Athari Ya Mtazamo Wako Kwa Vitu Vinavyokutokea
- 2024 badili mifumo yako ya kufikiri
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com