Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Kama Fedha Ingekuwa Dini

     

    Fedha ni kitu pekee duniani ambacho kinaunganisha watu wote. Hakijali jinsia, dini, rangi Wala kabila. Mwislam na mkiristo wanatofautiana kwa mamho mengu mengi kwenye dini, ila linapokuja suala zima la fedha basi wanakubaliana vizuri.

    Kwa hiyo nataka kusema Nini? Nataka kusema Mambo haya matano.

    Moja; kama fedha Ingekuwa dini, basi Ingekuwa dini yenye wafuasi wengi hapa duniani.

    Pili; kwa kuwa fedha inaunganisha watu wengi na ni muhimu sana kwenye maisha, basi hakikisha unaitafuta na unakuwa nayo.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Fursa Za Msimu

     

    Kuna fursa nyingine huwa zinatokea kwa msimu na kupotea. Ndio maana hata kwenye vyombo vya habari utasikia wanasema, msimu huu wa pasaka, krismasi n.k.

    Maana yake hicho ni kipindi ambacho huwa kinaambatana na fursa fulani.
    Kuna fursa za msimu wakati wa pasaka, krismasi, mwezi mtukufu wa ramadhani, sikukuu za kiserikali na kidini, matamasha, semina n.k.

    Mazao ya shambani pia huwa yana msimu. Kuna msimu ambao huwa yanapatikana kwa bei ya chini. Kuna kipindi huwa yanatikana kwa bei ya juu. Kipindi yanauzwa kwa bei ya chini, ni fursa. Kipindi yanauzwa kwa bei ya juu ni fursa pia.

  • Huu Ndio Ukweli Unapaswa Kuufahamu Kuhusu Wazo Bora La Biashara

    Rafiki yangu, moja ya kitu ambacho watu wamekuwa wanakosea ni Kushindwa kuanza  biashara huku wakisubiri wapate wazo bora la biashara.

    Ninachopenda ufahamu ni kuwa wazo Bora la biashara halishuki kutoka mbinguni.
    1. Wazo la biashara lipo kwenye huduma mbovu wanazotoa watu.
    2. Unaweza kupata wazo bora la biashara kutokea kwenye matatizo yanayowakumba watu.
    3. Unaweza kupata wazo bora kupitia kutembea.

    Kumbe basi, wazo la biashara halishuki kutoka popote bali lipo hapohapo ulipo. Kitu kingine ni kuwa wazo bora la biashara haliwi bora kwa sababu umeliona. Wazo  huwa  linakuwa bora kupitia kulifanyia kazi. Ila wazo Kama wazo huwa siyo bora au baya.

    Huwa mapenda kuwaambia watu kuwa wazo la kuanzisha Google halikuwa wazo bora. Ila hatua zilizochukuliwa baada ya kupata hilo wazo ndizo zililifanya liwe bora.

    Hivyohivyo kwenye wazo la kuanzisha Facebook, twitter, Coca-Cola na kampuni nyinginezo.

    Kwa msingi huo ndio kusema kuwa, ukitaka kulifanya wazo lako kuwa bora basi, lifanyie kazi.

  • Ugunduzi mkubwa kuwahi kufanyika hapa duniani

      

    Zimewahi kufanyika gunduzi nyingi sana hapa duniani. Na hata leo hii bado kuna gunduzi nyingi zinaendelea kufanyika. Hata hivyo, kuna ugunduzi mkubwa ambao ndiyo ugunduzi nambari moja kukiko ugunduzi mwingine unaoufahamu wewe. Na ugunduzi huu ni kuwa mtu anaweza kubadili maisha yake akibadili mtazamo wake.

    Hii ni kauli ya James Allen ambayo aliitoa kwa kusema; ugunduzi mkubwa katika kizazi changu ni kuwa mtu anaweza kubadili maisha yake endapo akibadili mtazamo wake.

    Looo! Ebu fikiria hili. Kumbe wewe unaweza kuwa na maisha bora endapo wewe utaamua kubadili mtazamo wako. Mtazamo wako wa sasa, ndio unaweza kutuonesha kesho yako ikoje. Ukibadili mtazamo wako unaweza kubadili maisha yako pia.

    Uko jinsi ulivyo kutokana na jinsi unavyofikiri. Anza leo kubadili mtazamo wako.
    Kuwa na mtazamo wa uwezekano. Fikiri kuwa inawezekana wewe kufikia mafanikio makubwa. Fikiri kuwa inawezekana wewe kwenda unapotaka kwenda.
    Kuwa na ndoto kubwa na kuwa na mtazamo kuwa inawezekana wewe kuzifikia hizo ndoto zako.

    Moja kati ya kitabu kitakachokufanya Sana kwenye kubadili mtazamo wako nabkusiendelea NDOTO ZAKO kubwa ni kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO pamoja na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Jinsi Habari Njema Zinavyoweza Kukufanya Upate Ushindi

     

    Soma habari njema kwanza, kabla hujasoma habari mbaya

    Tunaishi katika ulimwengu ambapo habari mbaya zinasambazwa kwa kasi kwelikweli kuliko habari njema. Hata hivyo kwenye ulimwengu huu unapaswa kuwa mtu wa kusoma habari njema zaidi ya unavyosoma habari mbaya.

    Jiwekee utaratibu wa kusoma habari njema kwanza.
    Ukiamka asubuhi, tafuta habari njema na uzisome.
    Mchana, Soma habari njema na usiku soma habari njema.

    Habari njema zinakutwa wapi?
    Habari njema zinakutwa kwenye vitabu vya hamasa,  vya ujasiriamali, vya biashara na maendeleo binafsi, pia habari njema inaweza kukutwa kwenye kusikiliza vitabu vilivyosomwa, au vitu vingine vya aina hiyo.

    Habari mbaya zimetapakaa mitandaoni, magazetini, redioni na maeneo mengine mengi.

    Kuna umuhimu wowote wa wewe kupata habari njema?
    Ndio, umuhimu upo. Habari njema zinakufanya uianze siku yako kwa namna chanya. Habari njema zinakufanya uendelee kuishi kwenye siku yako kwa namna chanya.
    Habari njema zinakufanya ufikirie vitu vizuri vyenye manufaa kwako na kwa wengine pia.

    Je, upo tayari kupata habari njema kwanza?

    Ni imani yangu kuwa mpaka hapa, utakuwa umeamua kuwa sasa unaenda kujijengea utaratibu wa kupata habari njema kwanza, kabla ya habari mbaya m hivyo Anza leo kuchukua hatua.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • PENDA MREJESHO.

     Kwenye makala ya jana nilikutahadharisha kuhusu kuepuka kujiingiza kwenye ugomvi na watu kutokana na wewe kutaka kuwaonesha njia sahihi pale unapoona hawafanyi kitu sahihi. Nilikutahadhirisha hivyo, kwa sababu watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli. Hata hivyo hali inapaswa kuwa tofauti kwako.

    Soma zaidi: Huu Ni Ugomvi Ambao Unapaswa Kujiepusha Nao

    Wewe unapaswa kuwa mtu wa kupenda mrejesho.  Penda mrejesho maana utakuimarisha.

    Muda mwingine unaweza kuuomba mrejesho kutoka kwa watu ili uweze kukusaidia kuboresha huduma zako.
    Au kuweka juhudi sehemu ambazo zina manufaa zaidi.

    Naomba nianze mimi leo. Naomba unipe mrejesho kuhusu makala au vitabu vyangu ambavyo umewahi kusoma.

    Naomba pia unipe mrejesho kwa kuniambia vitu ambavyo ungependa kuona nikiviwekea mkazo kwenye kuandika kwangu ila sasa hivi sivifanyi. Au mavifanya kwa viwango vya chini.

    Karibu

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Huu Ni Ugomvi ambao Unapaswa Kujiepusha Nao

     

    Rafiki yangu, muda mwingine watu huwa tunajikuta tumeingia kwenye Ugomvi na watu. Tena kwa kujitakia kabisa. Leo nimeona nikwambie kitu komoja kinachofanya watu waingie kwenye ugomvi na jinsi ya kukiepuka. Kitu hiki ni kuwaonesha watu kuwa wanakosea. Ni wazi kuwa unaweza kuwa unaishi na watu ambao wanafanya vitu ndivyo sivyo.
    1. Labda wanatumia fedha hovyo.
    2. Wanajihusisha na michezo ya kubahatisha
    3. Ulevi
    4. Kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii.
    5. Kuhonga n.k.

    Sasa unaweza kuona ni bora uwasiadie kwa kuwaambia kuwa wanachofanya siyo sahihi. Hapo sasa  ndio unaweza kujikuta umejiingiza kwenye ugomvi usiokuwa wa lazima. Wataanza kukwambia fedha tunazitafuta wenyewe, hatutaki shida.
    Wataanza kukwambia unawafuatilia maisha yao.

    Ngoja nikwambie kitu, watu wengi huwa hawathamini ushauri ambao unawapa tena bure. Njia bora ya kuwasaidia hawa watu ni wewe kuhakikisha unakuwa bora kwenye kile unachofanya. Kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Kiasi kwamba wakuulize wewe umewezaje kufanikiwa hivyo. Kama ni kuwa na fedha, basi zitafute za kutosha sana kiasi kwamba waanze kukuuliza umewezaje kufikia viwango vya kuwa na fedha kiasi hicho.

    Hapo sasa ndipo unaweza kuwahauri na kuwaonesha nini wanaweza kufanya.

    Kwenye hili Mahatma Gandhi amewahi kusema kwamba unapaswa kuwa mabadiliko ambayo unapenda kuyaona. Hivyo, Kama Kuna mabadiliko ambayo ungependa kuyaona kwa watu wakiyafanya, anza kuyaonesha wewe kwanza.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Wanaokwambia huwezi

     

    Wanaokwambia hujui, wanatumia mwonekano wako wa nje au wanatukua uzoefu wao juu yao. Wewe una uwezo mkubwa sana ndani yako. Anza kuutumia.

  • Tujikumbushe Dibaji Ya Kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI

    Rafiki yangu, kuna usemi kuwa kama kuna kitabu ambacho hakijawahi kuandikwa. Kiandike wewe.

    Wakati naandika kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI, nilikuwa naandika kitabu ambacho mwenyewe nilikuwa napenda kukisoma ila nilikuwa sijakipata sokoni. Cha kushangaza kuna watu wengi pia waliokuwa wanapenda kuona kitabu cha aina hiyo hiyo. Mmoja wao ni mwandishi wa Dibaji Ya Kitabu chenyewe Albert Nyaluke Sanga. Alipokisoma aliandika Dibaji ya kipekee Sana ambayo Leo nimeirudia kuisoma, nikaona siyo vibaya na wewe ukaisoma. Ebu msikilize Albert Nyaluke Sanga kwa maneno yake mwenyewe anasema;

    Nimepata wasaa wa kusoma vitabu vingi sana katika maeneo ya maendeleo binafsi na ukuaji wa kifikra hata hivyo nikiri kwamba nilipokishika kitabu hiki nikasema wawooo! Nimejikuta nakisoma tena na tena, sio ili nipate cha kukisemea bali nimejikuta ninavutiwa na kuguswa mno na mpangilio, muundo na maarifa ya kina ambayo mwandishi ameyawasilisha.

    Mwandishi, ameingia katika orodha ya waandishi wachache na adhimu sana katika lugha ya Kiswahili, wanaoandika aina hii ya maarifa. Jambo kubwa la kujivunia katika kitabu hiki ni kwamba mwandishi amefanya utafiti wa kina na kuwasilisha maarifa kwa namna yake. Naweza kusema hiki ni kitabu kilichojipambanua mno kwa maana kwamba hakikufanyiwa tafsiri ya waliyoandika wengine bali kimeleta mawazo halisi na uvumbuzi wa mwandishi. Kongole kwa mwandishi!

    Ni hakika kwamba muda huwa haubadilishi chochote, bali unachokifanya ndani ya muda ndicho huamua mabadiliko utakayoyapata. Mwandishi katika kitabu hiki ameeleza kwa namna ya kipekee namna bora ya kutumia muda.

    Katika maisha kuna namna mbili za kufanikiwa. Ya kwanza ni kujifunza kwa kukosea na ya pili ni kujifunza kutoka kwa waliotangulia. Njia ya kwanza ni ndefu mno, maana utalazimika kugundua kila kitu wewe mwenyewe na itakuchukua muda mrefu. Njia ya pili ni fupi na itakuchukua muda mfupi sana kufanikiwa.

    Hata katika Biblia, mathalani, Mungu anasisitiza kwamba ni vema kuchukua muda na kuyatazama maisha ya waliotangulia ili kujipatia raha nafsini mwetu, yaani furaha na mafanikio ya maisha. Mwandishi katika kitabu hiki ameturahisishia mno, maana pamoja na uvumbuzi wake mwingi pia anatuletea hekima zilizounganishwa kutoka kwa rundo la waliofanikiwa katika maeneo mbalimbali.

    Mimi nimeandika vitabu takribani 11 hadi sasa katika maeneo ya uchumi na familia. Kwa uzoefu wangu katika uandishi wa vitabu ninakiri kwamba kitabu hiki kina upekee mkubwa sana tena wa namna yake. Ndio maana kitabu hiki nathubutu kukiita kuwa ni hekima nyingi ndani ya kapu moja. Utakapokisoma mwanzo hadi mwisho utathibitisha hilo.

    Mwandishi amefanya kazi nzuri mno kushughulika na vile mtu unavyoweza kuboresha hatma yako. Wale ambao huwa wanadhani mafanikio ni jambo la bahati nasibu, mwandishi anawanoa huo uvimbe wa fikra kwa msumeno wa maarifa ndani ya kitabu hiki.

    Ndio maana nimependa sana alipoeleza habari ya kujiingiza katika orodha. Ohoo, kumbe mafanikio sio bahati nasibu bali ni suala la kuamua, kutendea kazi uliyoyaamua na kupata matokeo. Suala la kupata mafanikio ni uamuzi wako binafsi na mwandishi anasema hujachelewa kabisa!

    Hiki ni kitabu ambacho ninapendekezwa kisomwe kuanzia kwa vijana wadogo mpaka wazee. Kwa namna kitabu hiki kilivyo, kina hekima kwa rika zote. Kwa kuwa kina maarifa yenye chembechembe za kutengeneza na kuibua vizazi ni kitabu ambacho kinafaa kusomwa na watu wa elimu zote.

    Ingalikua amri yangu ningesema kitabu hiki kisomwe na kila mwanafunzi wa chuo kikuu, kisomwe na kila mfanyabiashara na mjasiriamali, kisomwe na kila mfanyakazi na kisomwe na kila mtu mahali popote alipo maadam anajua kusoma. Kuna mambo ndani ya kitabu hiki ambayo yakiingia na kupokelewa katika mioyo ya watu mahangaiko yatapungua sana kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja.

    Hongera kwa kushika nakala ya kitabu hiki, naamini muda utakaoutumia kukisoma pamoja na fedha uliyotumia kukinunua ni uwekezaji wa thamani sana na utakaokulipa vizuri sana maishani mwako na katika vizazi vyako vingi vijavyo

    Albert Nyaluke Sanga(SmartMind)

    Mwandishi  & Mjasirimali

    Mwandishi wa vitabu kama: Gia Kubwa, Umeiweka wapi Talanta yako? na Barua Ya Siri kwa wanandoa miongoni mwa vingi alivyoandika hadi sasa.

    Hayo ndiyo maneno ya Albert Nyaluke Sanga.

    Kama bado hujapata nakala ya kitabu hiki, kuna mengi unajikosesha sana. Gharana ya kitabu hiki ni 10,000/- tu.
    Tuwasiliane kwa 0755848391 ili uweze kukipata

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • NGUVU YA RIBA MKUSANYIKO-Utangulizi

     

    Riba mkusanyiko ni nini?

    Riba mkusanyiko ni muunganiko wa vitu baada ya kuwa vimefanyika kwa kipindi kirefu katika kuleta matokeo yaliyokusudiwa. Vitu  vikifanyika mara kwa mara kwa muda mrefu, huleta nguvu ya pamoja ambayo kwa kufanya kitu kwa wakati mmoja isingewezekana. Kwa mfano ni nadra sana kuangusha ukuta kwa kupiga nyundo moja tu. Hata hivyo, ukipiga nyundo nyingi unakuta mwisho wa siku zinapelekea kuanguka kwa ukuta. Hapa inakuwa siyo kwamba ukuta umeanguka kwa sababu ulipiga ile nyundo moja ya mwisho, bali kwa mkusanyiko wa nyundo zile nyundo kwa pamoja. Na hiyo hapo ndiyo inakuwa nguvu ya RIBA MKUSANYIKO. 

    Riba mkusanyiko inafanya kazi katika maeneo mengi ya maisha na wewe unaweza kuitumia kunufaika katika mambo mengi. Unaweza kuitumia nguvu hii kwa namna chanya kwenye kuweka akiba, kuwekeza, kusoma vitabu, kujenga mahusiano, kujenga tabia mpya mpaka kuandika vitabu.

    Nguvu hii pia huwa inatumiwa na watu kwa namna hasi kwa kujua au kutojua na hivyo kuwapelekea kupata matatizo au kuingia kwenye ubaya. Kuna watu wameingia kwenye uraibu wa kunywa pombe kwa kuanza kidogo na baadaye kujikuta wameshakuwa wanywaji wakubwa.

    Na hii siyo tu kwenye uraibu wa pombe bali karibia kwenye kila eneo hasi, Kama ilivyo kuwa unaweza kuitumia nguvu hii kujenga unaweza pia kuitumia kubomoa. 

    Kwenye kitabu hiki cha NGUVU YA RIBA MKUSANYIKO tunaenda kuona ni kwa jinsi gani utaweza kuitumia nguvu hii kwa namna chanya kwenye maeneo mbalimbali na ukapata matokeo makubwa. Je  , upo tayari kwa ajili ya safari hii? Imani yangu ni kuwa baada ya kuwa umesoma kitabu hiki, utachagua kitu kimoja ambacho utakifanyia kazi kwa kutumia NGUVU YA RIBA MKUSANYIKO. Nakutakia usomaji mwema.

    Godius Rweyongeza

    Jumatatu, 9 Agosti, 2020

    Morogoro

X